DARASA UK. 3

 

 

 

 

 

DARASA UK.3

 

WANAFUNZI WA KRISTO: 

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

             

Prophet Joachim Francis

 3.  purple world spin     NAMNA YA  KUJENGA  IMANI ILIYO NA                                               MIZIZI  ILETAYO MATOKEO  YALIYO SAHIHI

 

7/26/19, 11:19 - +255 654 333 5**: Maana sisi kwenye maombi tuliaminishwa ni maombi ya vita na kupambana tu sababu Shetani anatuwinda muda wote; matokeo yake vita na mashambulizi ndio ikawa inajiinua kweli...kila siku linaibuka jipya...mara tukiwa tunapambana ktk maombi ya vita wenye macho ya rohoni wanaona kundi la wachawi wamekusanyika wamezunguka nyumba...mara sijui vitisho kibao..kha!!!”

7/26/19, 11:31 - +255 719 513 9**: Tunapambana vita; tunachokonoa vya baharini, milimani, wakuu wa anga, khah!

7/26/19, 11:51 - +255 654 333 5**: Mimi nakwambia nina ushahidi lukuki. Tulikuwa tunabidii na hayo maombi ya vita tukichokonoa kote huko mizimu...baharini…milimani ...kuzimu...tena tunasema "enyi kuzimu sikia...ewe Shetani sikia…tumbo la kuzimu sikia…Tapika! ! Tunavunja madhabahu ya kichawi...ya kipepo...enyi ardhi ya waganga popote mliposikia...moto wa Roho Mtakatifu...siku hiyo mambo yanavyotokea kuna siku maid wangu akaona lishetani linashuka darini huku lina kwato likiwa linatisha na hasira kali likaenda taka mvamia mwana maombi mwenzetu..basi mara waone wachawi wameingia ndani mara chumbani kwao waone nyani mavitu ya kutisha tu…

7/26/19, 11:54 - +255 654 333 ***: Kuna siku tunasali hapo sebuleni mara tukaona nyoka anatoka chini ya kochi...kha…tukaanza kimbizana kuua nyoka...usiku huyo nyoka akamtokea dada wa kazi akimlaumu kwanini umenifanyia kitendo cha kinyama.

7/26/19, 12:01 - Vesta: Nishida!

7/26/19, 21:59 - +255 654 333 5**: Mtumishi leo somo uliloahidi mbona kimya?

7/26/19, 22:10 - Prophet: Shalom!

7/26/19, 22:18 – Prophet - added +255 714 414 1**

7/26/19, 22:29 – Prophet - added +255 679 078 ***

7/26/19, 22:10 - Prophet:  Nilibanwa...

7/26/19, 22:11 - +255 654 333 5**: Shalom mtumishi…yaani imefikia bila kupata neno la Mungu naona siku haijakamilika...nimepata Kiu na shauku kubwa ya kuijua kweli…

7/26/19, 22:12 - Prophet: Kwa hiyo, mpo tayari hata nifundishe wakati huu?

7/26/19, 22:16 - +255 785 918 6**: Ndiyo!

7/26/19, 22:17 - Prophet: Sawa...

7/26/19, 22:17 - +255 654 333 5**: Ndio mtumishi tena sanaaa!!

7/26/19, 22:25 - Prophet: Naendelea na somo la jana… Nataka nizungumzie ‘NAMNA YA KUJENGA IMANI INAYOLETA MATOKEO.

7/26/19, 22:26 - +255 785 918 6**: Sawa!

7/26/19, 22:27 - Prophet:  Tumejifunza namna ya kutumia vinywa vyetu kuumba matokeo tunayohitaji ila lazima tujue kuwa, Ukiri / kunena kwetu lazima kutokane au iwe ni zao la imani kwanza.

7/26/19, 22:28 - Vesta: Eeh!

7/26/19, 22:31 - +255 679 078 6**: Shalom sisters and brothers!

7/26/19, 22:32 - Vesta: Shalom!

7/26/19, 22:32 Prophet: Tunatakiwa tuwe na imani Iliyo IMARA au iliyo na misingi katika neno la Mungu; yaani chanzo chetu cha imani kiwe ni neno la Mungu, lakini hilo neno linatakiwa litengeneze kitu kinachoitwa ‘UHAKIKA’ ambao utashikilia msingi wa imani yetu. Uhakika huo ni kama ngao itakayo tushikilia kwenye misingi ili tusitoke kwenye msingi imara wa neno la Mungu.

7/26/19, 22:34 - Prophet: Waebrania 11:1 - Basi, imani ni ‘kuwa na hakika’ ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

7/26/19, 22:47 - Prophet: Sasa niwafundishe hili jambo na mlishike kwa juhudi zote…

Kwanza: Chanzo chako cha imani kiwe ni Neno la Kristo; yaani simamia ahadi za Mungu katika Kukiri kwa kudai haki zako - Warumi 10:17 ‘Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo.’

Pili: Neno hilo la Kristo linatakiwa litengeneze ‘UHAKIKA’ ndani yako...lakini uhakika huu huja tu kwa juhudi zako katika ‘kulishika na kulikumbuka na kuendelea kudumu katika hilo neno - Luka 8:15 …Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo ‘yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.’

Tatu: Imani ni bayana na mambo ya siyo onekana. Nikisema imani ni bayana na mambo yasiyo onekana namaanisha mambo ya kiroho! Sasa kunatofauti kati ya kuwa na imani na kuwa na matumaini! Kuwa na imani hakuhusiani kuamini kuwa utapata gari...nyumba...au mambo yoyote ya mwilini...hapana, kuwa na imani ni kuamini mambo ya kiroho au uweza wa kiroho utakaokupa matokeo ya mambo ya mwilini...kwa hiyo, huwezi kusema, unaimani ya kupata kazi...hapana, ila utasema una imani Ndani Ya Yesu atakayekupa uwezo wa wewe kupata kazi!

Unaweza ukawa na matumaini ya kupata kazi! Hilo nilitaka niliweke sawa ili muelewe kuwa na imani maana yake ni nini...tofauti na maana inavyofundishwa kwa sasa na wahubiri wengi kuwa imani ni bayana na mambo yanayo onekana ...si kweli… Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ‘ni bayana ya mambo yasiyoonekana.’

7/26/19, 22:53 - Prophet:  Kwa hiyo, ili tuwe na imani hayo mambo yanatakiwa kuzingatiwa ila imani iliyo ‘IMARA’ inajengwa na mambo yafuatayo:

 1. ‘USIKIVU’
 2. ‘UMAKINI’ (yaani kulishika na kudumu; nikisema kudumu namaanisha kuendelea kuliamini na kulikiri)
 3. ‘UVUMILIVU’

7/26/19, 22:58 - +255 713 626 4**: Ndiooo!!

7/26/19, 23:01 - Prophet:

 1. USIKIVU’: usikivu wa neno hapa inamaanisha kua unatakiwa uendelee kupata maarifa ya neno la Mungu kila siku..ongeza ujuzi wa kuzifahamu ahadi za Mungu kupitia neno lake kila iitwapo leo na juhudi hiyo lazima iongozwe na udadisi na kiu ya kuendelea kumjua Mungu ili fikra zako zibadilike kupitia neno lake ili upate kuelewa neno la Mungu; Waefeso 1:18 - ‘macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu   wa urithi wake   katika   watakatifu jinsi ulivyo’; Warumi12:2 - ‘Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua  hakika mapenzi ya Mungu  yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.’ Matendo 26:18 – ‘uwafumbue macho  yao,’ na kuwageuza waiache giza na     kuieleke nuru,  waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; ‘kisha  wapate  msamaha  wa dhambi zao, na   urithi miongoni mwao waliotakaswa   kwa imani iliyo    kwangu mimi.’
 2. ‘UMAKINI’:  umakini hapa inamaanisha kuwa hutakiwi kuruhusu hisia zako zitawale imani yako...mara nyingi unaweza kutana na hali au mazingira yanayoweza pingana na kile unachokiamini kuhusiana na ahadi za Mungu...usiruhusu uwaze au uwe na hisia tofauti na kile unacho kiamini...ukijiona unamawazo ya kukata tamaa au kuvunjika moyo haraka unachotakiwa kufanya ni ‘kujikumbusha na kukiri ahadi za Mungu katika hiyo hali’ hapo ndipo utaona ushindi ukidhihirika katika iyo hali unayopitia...hapa unatakiwa uwe na imani isiyo ‘BADILIKA’ kutokana na hali utakayopitia; Mathayo 17:20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, ‘Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali (yaani imani isiyobadilika katika msimamo wake)’ mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
 3. UVUMILIVU: uvumilivu hapa inamaanisha kuwa imani yako katika ahadi za Mungu lazima ipitie ‘KIPIMO’ ili ithibitike kua imani iliyo ‘IMARA’ ‘Changamoto’ ni sehemu za hivyo ‘VIPIMO’ katika kulithibitisha kupokea ahadi Za Mungu katika maisha yako...kwahiyo uvumilivu unaotakiwa ni kuendelea ‘KULISHIKA’, ‘KULIAMINI’ na ‘KULIKUMBUKA’ neno la Mungu na ahadi zake katika hali yoyote ngumu utakayo pitia...kwahiyo usiamini kitambo...endelea kuamini mpaka mwisho’; Luka 8:13 Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; ‘nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.’

Yakobo 1:2-4 [2] ‘Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; [3] ‘mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta uvumilivu.’ [4] ‘uvumilivu na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.’

1 Petro 1:7 ‘ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.’

7/26/19, 23:22 - Prophet:  Ukiyaelewa hayo niliyo yafundisha hapo juu ukayashika na kuyafanyia kazi basi wewe unaimani iliyo IMARA!

7/26/19, 23:23 - Prophet: Kesho sasa nitafundisha namna ya kutumia imani yako katika maombi kuzishinda nguvu za giza   hapa ndio wengi wanachangamoto.

7/26/19, 23:25 - +255 679 078 6**: Amen

7/27/19, 00:17 - +255 654 333 5**: Barikiwa

7/27/19, 00:20 - Prophet: Amina!

7/27/19, 01:13 - +255 679 078 6**: Mithali 20: 1 Usipende usingizi usije ukawa maskini;fFumbua macho yako nawe utashiba chakula.

7/27/19, 02:20 - +255 686 361 1**: Mungu atusaidie, mtumishi anafundisha kuhusu kutoa tuuu kila kitu anachofundisha lazima aunganishe, achomekee na sadaka ,dhabihu, au mmepiga fire freshhh Ila mwisho anaunganisha ili upokee lazima utoe ... Hapo Mimi nilikuwa natolewa kabisa uweponi; nilikuwa najiambia hapa tumeombaaa lakini maombi hayajafika sababu sina sadaka au sina kile kiwango kikubwa kilichotajwa, vinauma sana…

7/27/19, 04:34 - Vesta: Amen

7/27/19, 04:36 - Vesta: Pole sana mpendwa wengi tulikuwa na maswali kuhusu mahubiri hayo …

7/27/19, 08:30 - +255 686 361 1**: Yaani mm nilikuwa nasoma haya mafundisho jamani hata ukiri wangu umebadilika,pia nikamsikia tbjoshua anahubiri same ingawa yeye hakutoa reference nyingi,Mungu akubariki Prophet.

7/27/19, 08:32 - Prophet:  Amina!

7/27/19, 09:30 - +255 679 078 6**: Eheeee ni kwel kabxa Kumbe nilikuwa sijiulizi peke yangu?

7/27/19, 09:33 - +255 654 333 5**: Mimi juzi kuna Mchungaji aliniambia kuwa, nikitaka nipate kibali kwa Mungu au kuweka ulinzi katika maisha yangu; inabidi niwe natoa zaka katika kanisa ninalosali; hapo baraka zitaanza kuonekana.

7/27/19, 09:36 - +255 679 078 6**: Aahhhhaa!

7/27/19, 09:36 - Pasta Kinuka: Uongoo.... .

7/27/19, 09:36 - +255 686 361 1**: Nikawa nazidi kujiuliza na kujisemea mwenyewe, madhabahu kasema tutoe tupokee means mimi siwezi kupokea, sina sadaka, maana kukomaa kusema sina nantapokea nguvu hiyo nilikuwa sina, sababu sikuwa na neno na hata kama ningekuwa na neno, nilikuwa naona Ile madhabahu ishasema utoe ili upokee, najikuta hiyo siku kama sijaenda kanisani,  natoka empty…

7/27/19, 09:39 - +255 679 078 6**: Mhhhh! People tufunguke jamani maana kiukwel kila mtu anatafuta pesa kwa njia yake yoyote Ile...mmmhhhhh pale wasio na pesa maombi yao hayajibiwi…

7/27/19, 09:40 - +255 679 078 6**: Oh hello Pastor... Shalom!

7/27/19, 09:53 - Pasta Kinuka: Shalom!

7/27/19, 16:32 - +255 767 540 7**: It needs Grace of God.  Mimi hapa sijaelewa ila Yesu alisema Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu. Akasema NIRA yangu ni laini na mzigo wake n**: Vipi kuhusu Hebr 5:12-14

7/27/19, 18:10 - Vesta: why?

7/27/19, 20:16 - +255 654 333 5**: Shalom watumishi wa Mungu!

7/27/19, 20:16 - +255 686 361 1**: Shalom!

7/27/19, 20:21 - Prophet:  Shalom!

7/27/19, 20:21 - Prophet: Mpo watu wa Mungu?

7/27/19, 20:22 - Prophet:  Nataka nianze kutuma madini ya Neno!

7/27/19, 20:26 - +255 654 333 5**: Binafsi nipo tayari.maana leo tumeshinda bila umeme ndio umewaka, nimechaji cm kwa ajili ya madini...

7/27/19, 20:28 - +255 686 361 1**: Am here!

7/27/19, 20:45 -: Prophet:  Haya!

7/27/19, 20:50 - +255 654 333 5**: Bila kusahau lile somo la ‘JINSI YA KUPAMBANA NA FALME ZA GIZA.’

7/27/19, 20:51 - Prophet: Ndio...

7/27/19, 21:12 - Prophet: Nivumilieni Kuna...

7/27/19, 21:12 - Prophet:  Ila ngoja nianze kidogo… Kwa hiyo, jana nilikuwa nafundisha kuhusu IMANI ILIYO IMARA, Sasa maswali mengi yanaangukia eneo la kukemea mapepo na kuvunja nguvu za giza.

Je, hili swala likoje kwenye NURU YA NENO LA KRISTO? Ndio nataka tuangalie leo…Ilinibidi niwajenge kwanza kwenye msingi wa kuelewa Mkristo ni nani na imani ili tukifika huku tuweze kuwa na ufahamu wa kutosha. Baada  ya kufundisha maombi ni nini, nataka sasa tukazie kuelewa kuwa tunawezaje kutozuiwa na nguvu za giza katika maombi yetu au inawezekanaje maombi yetu na maisha yetu kutoathiriwa na nguvu za giza kwa imani…

7/27/19, 21:20 - Prophet: Tunatakiwa tuelewe kuwa, kinachotulinda tusishambuliwe na nguvu za giza ni imani na sio maombi ya vita. Waefeso 6:16 ‘zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.’ Ukianza kuomba maombi ya vita ni ishara tosha kuwa huna imani na hujui unacho kiamini au unayemwamini ni nani...kwa sababu Shetani au mapepo au nguvu za giza hazitafuti kuharibu mambo yako au maisha yako; Shetani anacholenga ni imani yako kwanza, akiweza kukutoa kwenye imani haya mengine atayapuliza tu na utapeperuka kama unyoya!

Mathayo 13:19 ‘Kila mtu alisikiapo Neno la Ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.’ Kinachomtisha shetani au kuzishinda nguvu za giza au mashambulizi sio maombi ni IMANI.

Sasa ni kufundishe siri hapa: Unatakiwa uelewe hila au mbinu za Shetani au mapepo katika kukushambulia na hila yake kuu na ya kwanza ni HOFU.

Warumi 8:15 ‘Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana,’ ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Ili ushambuliwe, kitakachofanyika ni kuwa utaletewa mazingira yatakayo jaribu kuingiza hofu ndani yako...na hayo mazingira yanaweza kuwa ni ndoto...maneno ya kukutishia kupitia watu...mafundisho yanayoingiza hofu kuogopa nguvu za giza na kazi za kichawi...na hali yoyote inayoweza kukutokea kukutia hofu.

 

Daudi hakuwa na roho ya woga, hakumwogopa

Goliati bali alimwamini Mungu.

 

Prophet: Katika kuzijua hila za Shetani lazima uelewe kwanza kuwa kinyume cha hofu ni UJASIRI...Ukijikuta unaishiwa ujasiri tu ujue kuna mawazo unainuliwa yanayojaribu kukutoa kwenye imani na hapo ndipo unapotakiwa kuelewa silaha za kiroho ni zipi...Wakristo wengi wanadhani silaha za kiroho ni maombi ya kushindana. Kuna silaha za kiroho; Silaha zetu ni za kiroho - 2 wakorinto 10:3-4 [3] ‘Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;’ [4] ‘(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;…)

7/27/19, 21:44 - +255 679 078 6**: Mhhhh... !

7/27/19, 21:44 - Prophet:  Silaha zinazozungumzwa hapa ni za kiroho zenye uwezo katika Mungu hata katika kuangusha ngome...ngome zinazotajwa hapa sio ngome za kichawi au madhabahu za waganga au mizimu; hapana, ni ngome ambazo ni fikra.,.mawazo...au elimu / mafundisho yanayojiinua au kupingana na kweli ya Neno la Kristo. !

2 wakorinto 10:5 ‘tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo;’ Ndugu zanguni kinacholengwa kupigwa vita ni ‘IMANI’; kariri hili kuanzia leo na usidanganyike kuwa Shetani anatafuta ndoa yako...biashara yako...afya yako, hapana, ni imani!

7/27/19, 21:47 - +255 679 078 6**: Amen!

7/27/19, 21:51 - +255 719 513 9**: Amen!

7/27/19, 21:51 - +255 719 513 9**: Asante prophet!

7/27/19, 22:07 - Prophet:  Bado

7/27/19, 22:41 - Prophet: …hizo silaha tunaweza anza fanya vituko tukidhani ndio tupo sahihi sasa. Silaha za kiroho ni kama hizi zifuatazo:

Waefeso 6:11: ‘Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.’ Silaha hizi ni maalumu kwa ajili ya kuzipinga hila za Shetani sio mashambulizi...kwa sababu kinachoanza ni hila au udanganyifu ili uwe mateka wa HOFU usiwe na IMANI...na kama nilivyokufundisha hila ya kwanza kuu ni hofu....hivyo tunakiwa kufahamu tupambana na nguvu za giza katika ulimwengu wa roho kwa hiyo silaha zetu zinatakiwa ziwe za rohoni pia.

Waefeso 6:12-13: [12] ‘Kwa maana, kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.’ [13] ‘Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.’

7/27/19, 22:49 - Prophet:  Sasa

Waefeso 6:14-17[14] Basi simameni, ‘hali mmejifunga kweli viunoni’, na ‘kuvaa dirii ya haki kifuani,’ [15]na kufungiwa miguu utayari tupatao ‘kwa Injili ya amani;’

[16]zaidi ya yote ‘mkiitwaa ngao ya imani,’ ambayo kwa hiyo ‘mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.’ [17] ‘Tena ipokeeni chapeo ya wokovu,’ na ‘upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;’

7/27/19, 22:52 - +255 719 513 9**: Amen…

7/27/19, 22:53 - Prophet: Silaha

 1. Kweli ya Neno la Kristo
 2. Haki ya Mungu kupitia Yesu
 3. Lazima uhusike katika kueneza injili
 4. Imani
 5. Uwe
 6. Uwe na upanga wa roho yaani ujue namna ya kuzikiri ahadi za Mungu kupitia NENO lake.

7/27/19, 22:54 - Prophet: Usipo kuwa na hizi silaha wewe tegemea kushambuliwa na mapepo kila kona ya maisha yako; yaani mapepo yatakaa hadi kwenye kucha.

7/27/19, 22:55 - +255 679 078 6**: Barikiwa!

7/27/19, 23:02 - Prophet: KWELI:

 1. Ni lazima uwe na juhudi kuifahamu na kuitendea kazi kweli ya Neno la Kristo;
 2. Ni lazima uamini kuwa wewe ni mwenye haki mbele za Mungu; hivyo umesamehewa ila ukianza kuomba maombi yako ya rehema ya kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha nne na dhambi zako binafsi unafungua mlango wa mapepo kukushambulia;
 3. Kwa namna yoyote lazima ujihusishe katika kuhubiri na kuwaelezea watu ukweli kuhusiana na Yesu na wokovu;
 4. Lazima uwe na imani iliyo imara kama nilivyofundisha ili hila za muovu zisikushinde;
 5. Ni lazima uwe umepokea uzima wa milele yaani wokovu ila hapa nitafundisha kwa undani zaidi nini maana ya kuokoka ili muelewe wokovu ni nini.
 6. Ni lazima utumie kinywa chako kukiri ushindi katika kila hali au changamoto unayopitia au mashambulizi unayo yaona...kutumia kinywa chako kukiri huko ndiko kuwa na upanga yani UKIRI WA AHADI ZA MUNGU kupitia Neno lake.

UKIZITENDEA KAZI HIZI SILAHA, HAKUNA NGUVU ZA GIZA ZITAKAZO KUSHINDA!

7/27/19, 23:05 - +255 754 650 6**: Amen

7/27/19, 23:08 - Prophet: Sasa hapa mafundisho mengi ni watu watafundishwa maombi ya kuombea ardhi...kuvunja madhabahu za umasikini...madhabahu za magonjwa...madhabahu za mauti...maombi ya kuua roho za uchawi....kukatakata kamba za mauti; utafundishwa hadi kutumia mafuta ya upako… udongo...chumvi kuwa ndio silaha, hayo yote yanafanya uzidi kushambuliwa!

7/27/19, 23:12 - Prophet: Sikiliza, hauanzi kutaja hivi vitu kwa sababu havina uhusiano na wewe kabisa. Kinachotakiwa kutoka kwenye kinywa chako ni UKIRI WA AHADI ZA MUNGU TU kwa sababu imani yako inathibitishwa kwa UKIRI wako. Ukiri na kutaja mapepo yatakufuata, ukikiri uzima utakufuata. Ndio maana wanaoomba sana maombi ya kushindana wanashambuliwa sana na mapepo kwa sababu wameamini kuwa wao sio washindi bali wanashindana.

7/27/19, 23:15 - Prophet: Sasa kesho nitafundisha kuhusu ‘SIRI YA USHINDI AMBAYO NI WOKOVU WETU’; hapo ndio nitaeleza maana halisi ya WOKOVU au KUOKOKA...

7/28/19, 01:10 - +255 654 333 5**: Amina mtumishi Mungu akubariki sana!

7/28/19, 08:44 - Vesta: Shalom!

7/28/19, 08:45 - +255 719 513 9**: Shalom!

7/28/19, 08:52 - Vesta: Hadi kwenye kucha?!!

7/28/19, 08:55 - Vesta: Aisee kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa duuu! Hatari

7/28/19, 17:41 - +255 654 333 5**: Shalom!

7/28/19, 18:01 +255 754 650 6**: Shalom!

7/28/19, 20:02 - Vesta: Shalom kimya leo!

7/28/19, 20:05 - +255 754 650 6**: Naona mtumishi anaandaa somo...

7/28/19, 20:22 - +255 654 333 5**: Yaani tunalisubiri kwa hamu sana!

7/28/19, 20:34 - +255 754 650 6**: Acha

7/28/19, 20:48 - Prophet:  Shalom

7/28/19, 20:48 - Prophet:  Ndio kwenye huduma. ?

7/28/19, 20:49 - +255 713 626 4**: Vemaaa!

7/28/19, 20:51 - Prophet: Mpo kwa mafundisho?

7/28/19, 20:55 - +255 754 650 6**: Ndiooo…

7/28/19, 20:57 - +255 654 333 5**: Ndiooo…

7/28/19, 20:58 - Prophet: Haya!

7/28/19, 20:59 - +255 654 333 5**: Pia ningependa kujua watoto wadogo miaka miwili hadi mitano na kuendelea wanaruhusiwa kufunga na kukaa katika mikesha ya watoto?

7/28/19, 20:59 - My Son Profet: ???!!!

7/28/19, 21:03 - Vesta: …hiyo ya sabasaba?

7/28/19, 21:04 - Prophet:  Leo  naendelea kufundisha kuhusu WOKOVU NI NINI.

7/28/19, 21:04 - Vesta: Nipo nimejaa tele…

7/28/19, 21:04 - Prophet: Ha ha kwa utukufu wa Bwana!

7/28/19, 21:05 - Prophet: Hili somo litagusa pia swali la @2557675407** kuhusu kitabu cha Waebrania kuwa kulishwa maziwa na kuhusu Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu. ? Kwa ufupi, wokovu ni kuelewa na kuamini kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. Katika kuelewa hili jambo; ndipo kwenye siri ya Deliverance na Uhuru wa kutoka kwenye mashambulizi ya kipepo.

Deliverance Deliverance sio kutumia mafuta…maji...chumvi...udongo au kufunga siku saba.

Katika wokovu tunapata kitu kinaitwa ‘Deliverance’ na deliverance huja kwa kuambiwa ukweli wa Neno la Mungu na kuliamini Neno.

 

 

Kwa hiyo wokovu ni kuamini kuwa Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili yetu na pia tulikufa na kufufuka pamoja na yeye. Kwa hiyo, Yesu alikufa kwa ajili ya makosa yetu tuliyorithi kwa Adam na ya kwetu binafsi na alifufuliwa ili tuhesabiwe HAKI.

Warumi 4:25 ‘ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.’ Lishike hili ili tunapoelekea tupate picha kamili.

7/28/19, 21:51 - Prophet: Kwa sababu, wengi wanafikiri unaokoka tu ukikiri ile sala ya toba...hapana, unaweza ukakiri sala ya toba na bado mapepo yakakuandama tu. Kwa hiyo, ni lazima tuamini katika nguvu ya MAUTI ya Yesu na nguvu ya UFUFUO wa Yesu ili tuanze kuona matokeo ya hivyo vitu katika maisha yetu.  Lakini kwanza, tunatakiwa tuelewe namna ya kujiambatanisha na hizo nguvu ili zitende kazi katika maisha yetu kama Wakristo.

7/28/19, 21:57 - Prophet: Nikizungumzia MAUTI na UFUFUO wa Yesu na kukumbushia kuhusu swala la Ubatizo pia. Ili uweze kuokoka au kupokea wokovu yaani uzima wa milele; hizi nguvu mbili ni lazima zianze kutenda kazi ndani ya maisha yako LAZIMA UFE KWANZA halafu UANZE KUISHI MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO.

Sasa usishtuke nikisema lazima ufe. . Kwa hiyo, tunaunganishwaje au tunajiunganishaje kwenye kifo na ufufuko wa Yesu?

Nianze na upande mmoja…Upande wa mauti kwa sababu sitaki kuharakisha hili somo. . Warumi 6:6-7 [6] mkijua neno hili, ‘ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;’ [7] ‘kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.’

Kinachokufa au anayekufa ni MTU WETU WA KALE au ASILI YETU YA DHAMBI au YAKUPUNGUKIWA UTUKUFU WA MUNGU NA KUKOSA USHIRIKA NA MUNGU.

Sasa kufa huku kunatokea pale tu ukiamua KUAMINI kuwa Kupitia Yesu dhambi zako zilikufa pale msalabani! Na sio kwa kuomba rehema au kusali sala ya toba. Warumi 6:11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.’ Amini ya kuwa Yesu alivyokufa msalabani dhambi zako zilikufa pamoja naye; hapo ndipo inamaanisha kuwa tulikufa pamoja na Kristo.

Warumi 6:8 'Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;'

7/28/19, 22:21 - Prophet: Ukiamini sasa kua dhambi zako zilifia pale msalabani amini sasa kua ulifufuliwa pamoja na Kristo!

Warumi 6:5 'Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;'

7/28/19, 22:27 - Prophet: Ukiamini wewe sio mdhambi tena kupitia umauti wa Yesu unatakiwa uamini sasa kua ulifufuka pamoja naye ...katika kuamini kua ulifufuka pamoja na Yesu ndio tunapokea UZIMA WA MILELE yani AHADI ZA MUNGU kwa sababu ya hiyo imani tunafanyika kua watumwa wa haki na sio watumwa tena wa dhambi...kumbukua hivi vitu ni vitu vya kiroho vinavyohusiana na mabadiliko ya asili ya anguko la mwanadamu na urejesho wa ushirika wa Mungu na mwanadamu.

Warumi 6:18, 22 [18] ‘na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.’ [22] ‘Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.’

Katika kuamini kua Yesu alifufuka tunakiwa tujiambatanishe na ufufuo huo kwa njia ya imani ...na huwezi kuamini pasipo kuelewa Yesu alifufuliwaje na alifufuliwa ili iweje...tumeshajua alifufuliwa ili tuhesabiwe haki kwa hiyo tuangalie Yesu alifufuliwaje na hapa ndipo panashugulikia shida zozote za kiroho za mashambulizi ya kipepo.

7/28/19, 22:36 - Prophet:  Yesu alivyofufuliwa aliketishwa juu sana zaidi ya Falme na mamlaka za giza upande wa kuume wa Mungu baba yetu sio tu kwamba alifufuliwa na kuketishwa peke yake..hapana tulifufuliwa na kuketishwa PAMOJA NAE katika ULIMWENGU WA ROHO NDANI YA UFALME WA MUNGU.

Waefeso 2:6 [6] ‘Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;’ Waefeso 1:20-22 [20] ‘aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;’ 21] ‘juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;’ [22] ‘akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;’ hapa ndio MCHAKATO WA DELIVERANCE unaanza katika maisha ya mtu ya kiroho katika kuelewa na kuamini UHAMISHO wa kiroho uliotokea kutoka kwenye UFALME WA GIZA na kuelekea katika UFALME WA MUNGU. Usipo elewe na kuamini uhamisho wa aina hii huwezi sema you are DELIVERED! Kwa sababu, Deliverance sio kutolewa mapepo au kutapishwa au kuombewa maombi ya kuzuia nguvu za giza; DELIVERANCE NI KUAMINI UKWELI KUHUSU UHAMISHO WA KIROHO KUTOKA UFALME WA GIZA NA KUINGIA KWENYE UFALME WA MUNGU.

Wakolosai 1:13 ‘Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;’ Kwa sababu Deliverance ni kuambiwa Kweli ya Ahadi za Mungu katika Neno lake.

Luka 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. ‘Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao’, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, … Ndio maana wanao hangaika kwenda huku na huko kuombewa mapepo yawatoke na nguvu za giza ziwaachie hawawi huru kwa sababu hawajaambiwa kuhusiana na huu ukweli wakaamini ili huo ukweli udhirike na uwaweke huru.

Yohana 8:32 ‘tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.’

Na wale wanaojihusisha na maombi ya kupambana sana sana wanayachokoza hayo mapepo yazidi kuwashambulia; sasa ukiambiwa kupambana huko ndio kuuteka Ufalme wa Mungu kama mtu mwenye nguvu basi umefundishwa ndivyo sivyo na mafundisho yanayo kufundisha kupambana sio mafundisho sahihi kwa sababu imani yetu inatuambia sisi ni washindi na kupambana kwetu ni kwa kutumia silaha za kiroho na sio kuomba maombi ya kupambana.

7/28/19, 22:50 - Prophet:  Habari njema , YOU ARE DELIVERED!

Amini hili na uliishi hili kwa imani na utaona matokeo yake kinyume na hapo utaomba sana ila hutapata matokeo labda kwa neema na huruma za Mungu.

7/28/19, 22:51 - Prophet: Kwa hiyo, mtu yeyote au DELIVERANCE I AM DELIVERED ALREADY!

7/28/19, 22:52 - +255 654 333 5**: !

7/28/19, 22:55 - Prophet: Na mambo mambo . Najibu swali la mama hapa +2557675407** haya ndio maziwa yenyewe yaani misingi ya Mkristo ya imani.

Waebrania 5:12-13 [12] ‘Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.’

[13] ‘Kwa maana, kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.’

7/28/19, 23:33 - +255 654 333 5**: Tunakushukuru sana mtumishi kwa madini mazito…

7/28/19, 23:40 - +255 714 414 1**: Barikiwa !

7/29/19, 10:46 - Prophet: Shalom!

7/29/19, 11:05 - +255 754 650 6**: Shalom!

7/29/19, 11:09 - Prophet:  NaKaribisha

7/29/19, 11:09 - Prophet:  Mwenye swali kwa …

7/29/19, 11:29 - Prophet: added +255 712 090 9**

7/29/19, 12:59 - +255 654 333 5**: Sa.wa, . Sema kwa kuwa nipo ofisini, kwenye kitabu cha ufunuo kumesisitizwa sana "tubuni dhambi zenu; “ sasa hii ni kwa ajili ya watu gani? Ikiwa dhambi zetu zilishasafishwa kwa damu ya Yesu?

7/29/19, 13:08 - Prophet: Okee, , ...

?  Na toba ni nini? Kwa jinsi .

7/29/19, 13:46 - +255 654 333 5**: Nitajibu nangoja nitoe wateja…

7/29/19, 14:29 - Vesta: Nimeipenda hii inabidi nikariri na mistari yakumpa ukweli.

7/29/19, 20:05 - Prophet: Kwa hiyo ?

7/29/19, 20:09 - +255 654 333 5**: Mi ninayo mengi lakini mpaka nifike home!

7/29/19, 22:35 - +255 654 333 5**: Dhambi ni hali ya nafsi, hali ya rohoni ambayo mtendaji huwa nayo juu ya kitu, mtu au hali nyingine yenye dhamira ya kujeruhi na kuharibu. Ni hali ya giza ya kukosa nuru.

7/30/19, 21:33 - Vesta: Shalom, wanafunzi wa Yesu, poleni namajukumu, Leo kimya!

7/30/19, 21:34 - +255 654 333 5**: Shalom watumishi.Naona kimya kweli kweli…

7/30/19, 22:01 - +255 719 513 9**: Shalom!

7/30/19, 22:08 - Prophet: Shalom!

7/30/19, 22:08 - Prophet:  Nilikua kwenye maombi.

7/30/19, 22:11 - Prophet:  added +255 754 370 2**

7/30/19, 22:12 - Prophet: Nataka ni-type haya mafundisho niyapange.

7/30/19, 22:12 - +255 754 650 6**: Sawa mtumishi.

7/30/19, 22:13 - Prophet:  Ila nitaendelea na mafundisho….NILIISHIA KUFUNDISHA KUHUSU ‘MAANA HALISI YA WOKOVU’; Nikamalizia na kueleza MAANA HALISI YA DELIVERANCE. Ndio maana nikaruhusu muda wa maswali.

Mwenye swali aulize. Anayehitaji ufafanuzi pia ruksa.

Kwa hiyo, hadi nilipofundisha sasa nataka niitoe kwa mfumo wa soft copy - pdf ili iwe ni mjumuisho wa yote niliyofundisha. Ninachoomba, nikitu kimoja tu, najua mafundisho yangu yapo against  mapokeo mengi. Ninachofundisha ni mafundisho ya kwenye biblia yaliyosahihi. Mafundisho haya yatakusaidia sana katika kusimama na kumjua Mungu katika usahihi.

7/30/19, 22:36 - Vesta: Haya ndio mafundisho ninayoyataka hata hoja ikitokea najua nasimamia vifungu gani kwenye biblia.

7/30/19, 22:58 - +255 686 361 1**: Mungu atakulipa, tunashukuru sana…

7/31/19, 01:06 - +255 654 333 5**: Umeitwa na Mungu kuja kutufungua macho na akili. Barikiwa sana mtumishi…

7/31/19, 09:28 - Prophet: Shalom Wana wa Mungu!

7/31/19, 09:30 - +255 679 078 6**: Shalom mtumishi

7/31/19, 09:31 - Vesta: Shalom

7/31/19, 09:46 - +255 659 287 3**: Shalom

7/31/19, 09:46 - +255 654 333 5**: Shalom

7/31/19, 10:22 - +255 686 361 1**: Shalom

7/31/19, 10:41 - +255 719 513 9**: Shalom

7/31/19, 11:08 - +255 713 626 4**: Shaloom

7/31/19, 11:10 - +255 713 626 4**: Ameeen

8/1/19, 10:14 - Prophet: Shalom watoto wa Mungu!

8/1/19, 10:33 - Vesta: Shalom mtumishi wa Mungu

8/1/19, 10:33 - Prophet:  Leo nitaendelea kufundisha…

8/1/19, 10:34 - +255 686 361 1**: Can't wait prophet

8/1/19, 10:37 - +255 713 626 4**: Shaloom!

8/1/19, 10:49 - Prophet: Me too!

ENDELEA DARASA UK.4

 

laugh"In teaching others we teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages