DARASA UK.8

 

 

DARASA UK.8

 

 

WANAFUNZI WA KRISTO: 

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

 

 

 Prophet Joachim Francis

...KUTOKA UK. 7

9/14/19, 16:41 - PROPHET:  Tunapokea sio kwa sababu tunaupako kuliko nyinyi; mnapokea kwa sababu tunahamasisha imani zenu kuwa imara kupitia neno la Mungu.

Na source ya huo uponyaji ni jina la Yesu.

9/14/19, 16:43 - +255 763 194 9**: Ni kweli imani ndio kila kitu kwetu Wanafunzi wa Kristo,’YOTE YANAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE.’

9/14/19, 16:44 - PROPHET:  Na leo nataka nifundishe kuhusu Kuamini kwa Matarajio ya Kupokea.

Njia sahihi ya kupokea ni ipi na kwa kutumainia nini?

9/14/19, 16:44 - Vesta: Kweli

9/14/19, 16:45 - PROPHET:  Changamoto ipo hapo ...watu wengi wanataka kupokea lakini point of contact wanazo tumia hazina uhalisia wa Mungu ndani yake...wanapata matokeo ya muda...au wanabahatisha kupata au hawapati kabisa. Kumbuka, nilisema kuna tofauti kati ya ‘Kuamini’ na kuwa na ‘imani.’ Bado nazungumzia ‘kuamini.’

Kuamini ni kujijengea ‘uhakika’ katika kile unachokitarajia kitokee...na uhakika huo unaujenga kwa kujiamini wewe kwanza kuwa una uwezo wa kusababisha yale matarajio yako yatokee.

Uwezo au nguvu hiyo ipo ndani yako na sio kwa mtumishi.

Naomba niliweke sawa kwanza hilo.

9/14/19, 16:51 - Vesta: Amina mtumishi nakuelewa.

9/14/19, 16:53 - PROPHET:  Kwa hiyo, uhakika unaokuwa nao ni kwa ‘kujishawishi kuwa tayari umeshapokea.’ Hapa ndio watu wengi wanafeli kwa sababu gani? .

Kuna kitu Yesu aligusia akasema, ‘hakuna kisichowezekana kwa yule aaminiye.’

Mathayo 17:20 - Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; ‘wala halitakuwako neon lisilowezekana kwenu.’

9/14/19, 17:00 - +255 763 194 9**: Ni

9/14/19, 17:04 - PROPHET: Imani sio jambo linaloanza...kuamini ndio jambo linaloanza na imani ni tokeo la kuamini kwako. ‘Imani huja kwa kusikia au kupata ufunuo wa Kristo ndani yako au Mungu au uwezo ulio ndani yako.’ Lakini ‘kuamini huja kwa kujipa uhakika na kujishawishi kuwa yale unayoyatarajia yametimia kabla hayajatimia.’

Kwenye kiingereza ‘Faith’ imetofautishwa na ‘Belief.’

Kwenye biblia ya kiswahili yanaweza leta maana zinazofanana na yaka shaabihiana katika matumizi lakini yanautofauti.

9/14/19, 17:10 - +255 763 194 9**: Oooh! Exactly!

9/14/19, 17:14 - PROPHET: ‘Imani kwa uhalisia wake ni UHAKIKA unaokuwa nao baada ya kujishawishi vya kutosha kuwa umepokea yale unayoyatarajia kabla hujapokea.’

Leo watu hawana hata uhakika na wanavyoviomba hawana uhakika wowote wanamatarajio ya vitu wasivyoamini wamepokea wanapewa mafuta, maji, picha za watumishi na matokeo yake ni kwamba uhakika wanaoujenga upo nje ya uwezo wao wa kutokeza yale wanayoyatarajia.

Kwa ufupi wanafungamanisha nguvu za Mungu katika vitu na sio wao binafsi.

Bila kuelewa, wamebadilisha utukufu wa Mungu kuwa vitu na wasione matokeo yotote. Hapo ndio unakutana na wale wanaopenda ishara na mazingaombwe, ndio mtu anatumia mafuta leo anapata nafuu hali inazidi kuwa mbaya baada ya siku mbili tatu… Anaanza kujiuliza kwanini? Anatoka hapo anaenda kuoga mafuta kabisa sasa ya mtumishi mwingine kwa sababu yale aliyopaka yana upako kidogo!

Huyu mtu anapata tena kaunafuu halafu hali inarudi pale pale...anaenda kutafuta nabii mwingine. Matokeo ya huyu mtu ataishia kukata tamaa; atarudi kwa waganga au duniani kabisa Kwa sababu hana cha kusimamia au kutumainia. kwa ufupi, anakuwa hana Mungu katika maisha yake binafsi.

Usipojua kuwa uwezo upo ‘ndani yako;’ utapelekwa na upepo wa kila aina ya mafundisho kwa sababu utataka matokeo bila kupata msingi ulio sahihi. Utaambiwa toa sadaka, utatoa na hutaona kitu...utaambiwa nunua sticker, mafuta, toa sadaka ya kujimaliza, utanunua na kutoa na hutaona kitu...utaambiwa jiambatanishe na mafuta ya mtumishi umtumikie; utakuwa unapangusa hadi jasho la mtumishi ila utaambulia patupu...kwa nini? Kwa sababu unachokitafuta hakina uhalisia na Mungu.

Yale unayoyatamani yapo yanakusuburi endapo ‘utajishawishi kuwa tayari umeyapokea!’

Marko 11:24 - Kwa sababu hiyo nawaambia, ‘Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.’

9/14/19, 17:41 - Laura: Ameeen, kweeeli kabisaa.Tupe aiseee tupone!

9/14/19, 17:46 - PROPHET:  Kazi unayoitaka, jishawishi kuwa tayari unafanya kazi!

Mtaji unaoutaka, jishawishi kuwa tayari umeupata na umeanza biashara!

Ndoa unayoitaka, jishawishi kuwa tayari umepata ndoa.

Kila unachohitaji na kukitarajia, jishawishi kuwa tayari unacho!

Unavyojishawishi unajenga uhakika ndani ya ‘moyo’ wako au ‘subconcious mind’ yako na uhakika huo unatakiwa uanze kujengeka huko sio uhakika unaofikirika, hapana, bali uhakika ambao ni uhalisia wako tayari.

Ule uhakika ambao ndio ‘imani’ yenyewe ndani ya moyo wako sio akili zako ndio kisababishi cha kuvuta na kujibu / kudhihirisha yale unayoyatarajia wewe.

Nilipokuwa nafundisha kuhusu ‘UKIRI,’ hapa ndio ukiri unapotumika kujishawishi wewe kuwa umeshapokea yale unayo yaomba..sio kutumia maombi kutoa taarifa ya mahitaji yako kwa Mungu asiye ndani yako na usiye mjua hapana, hayo sio maombi huo ni udini na kupoteza muda.

9/14/19, 19:10 -PROPHET: Lengo kubwa la kuomba ni kuimarisha hali yako au uwezo wako wa kuamini. Pale ambapo imani imeanza kujengeka; yaani uhakika ndio matokeo yataanza kutokea kwako.

9/14/19, 20:40 - Mashallah: Shalom Prophet. Mimi ni mama yake na Francis. Naomba uniunge kwa namba yangu 07675207**.Amina.

9/14/19, 20:42 - PROPHET: Added +255 767 520 7**

9/14/19, 21:17 - +255 767 520 7**: Shalom … Shalom. Asante Baba yangu…

9/14/19, 22:40 - Vesta: Amen mtumishi!

9/14/19, 23:23 - +255 654 333 5**: Amina… mtumishi...nakuelewa sana…

9/15/19, 08:44 - PROPHET: Shalom, nawakaribisha kwenye ibada ya leo… Na muwe na Jumapili njema.

9/15/19, 08:44 - My Son Profet: Amina mama…

9/15/19, 08:46 - Laura: Ameen…

9/15/19, 09:07 - +255 754 650 6**: Amen Pastor

9/17/19, 00:33 - +255 654 333 5** left

9/17/19, 12:05 - PROPHET:  Shalom shalom!

9/17/19, 12:05 - +255 767 520 7**: Shalom

9/17/19, 12:05 - +255 754 650 6**: Shalom

9/17/19, 12:27 - +255 763 194 9**: Shalom

9/17/19, 13:03 - +255 714 414 1**: Shalom

9/17/19, 13:10 - Vesta: Shalom!

9/17/19, 13:10 - PROPHET:  Mnaendeleaje?

9/17/19, 13:38 - +255 763 194 9**: Namshukuru MUNGU mi kwa upande wangu niko poa…

9/17/19, 13:58 -PROPHET: Mungu mwema. Nitaendelea na mafundisho leo…

9/17/19, 14:02 - +255 763 194 9**: Amen, nasubiria kwa hamu…

9/17/19, 14:03 - Vesta: Amina, nasubiria kwa hamu…

9/17/19, 16:05 - +255 713 626 4**: shalom!

9/17/19, 16:05 - +255 713 626 4**: tunasubiria…

9/17/19, 17:49 - PROPHET:  Shalom shalom!

9/17/19, 17:50 - +255 763 194 9**: Shalom

9/17/19, 17:52 - PROPHET: Nilikuwa nafundisha kuhusu Imani lakini kipengele cha ‘Kuamini.’

Nikaweka wazi namna ya kuamini na kwa nini kuamini ni muhimu na pia nikasema imani ni tokeo la kuamini kwako.

Leo naendelea kufundisha kuhusiana na ‘chanzo cha Imani.’

Au kinachosababisha imani iwepo… Mafundisho hayatakuwa marefu ya leo ila lazima utatoka na uelewa fulani wa tofauti.

Imani chanzo chako ni ‘KUSIKIA.’ Lakini kusikia huku huja kwa ‘NENO LA KRISTO.’

Warumi 10:17 – ‘Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.’

Nataka uweke tofauti baina ya maneno haya: ‘KUSIKIA’ na ‘NENO LA KRISTO.

Imani ni kuwa na uhakika...lakini chanzo au sababisho la uhakika huo ni hali yako ya ‘usikivu’ ambayo ni hali endelevu ya kusikia ‘neno la Kristo.’ Niseme kitu sasa hapa cha muhimu sana:

Wakati nilikuwa nafundisha kuhusu namna ya ‘kuamini’ kama hatua ya kujenga Imani, nilisema, kuamini ni kujishawishi kuhusiana na jambo unalotarajia litokee kwako ama ulipokee. Na nikasema, kujishawishi huko ni kwa kujiaminisha kuwa lile unalolitarajia tayari umelipokea.

Sasa, kujishawishi huko ni kwa njia ya ‘UKIRI.’

‘UKIRI’ wako ndio biblia inatafsiri kama MAOMBI au SALA unazofanya.

Na umuhimu wa ukiri wako sio kwamba Mungu anasikia unachosema ...hapana ni kwamba, unavyokiri unakuwa unasikia kile unachosema ili ujishawishi na kujiaminisha kuwa umepokea yale unayoyatarajia - ndio lengo kuu hasa la maombi; kujishawishi wewe juu ya matarajio yako!

9/17/19, 18:18 - +255 763 194 9**: Amina

9/17/19, 18:22 - PROPHET:  Kwahiyo maombi yana nguvu kama unavyoomba unaomba katika hali ya kujiaminisha wewe...na kwanini maombi au ukiri una nguvu? Una nguvu kwa sababu hii tuu...fuatilia kwa makini.

Sio kila kitu mtu atakacho omba kitakuwa na matokeo. Hii inatokana na kwamba hana imani juu ya kile anachokisema...nikisema hana imani juu ya kile anachokikiri au kuomba namaanisha ya kuwa hajajishawishi vya kutosha juu ya uhalisia wa kile anachokiomba au kukikiri; kwa hiyo kuna kuwa hakuna matokeo kwa sababu hakuna imani iliyojengeka.

Na nguvu ya kile mtu anachokikiri au kuomba kwa imani ipo katika uhakika na hali yake ya kujiamini huyo mtu...na uhakika alionao sasa unatokana na ufunuo wa kile anacho kisikia kila anapojishawishi kwa maombi na sala...uhakika wake huyu mtu unakuwa jambo halisi ambalo chanzo chake ni cha kiroho na sio kimwili.

Kwa nini ipo hivi? Ipo hivi kwa sababu kila kitu kiliumbwa kwa chanzo cha ‘NENO!’ Na ili hivyo vitu vilivyoumbwa kwa neno vitokeze, ‘IMANI’ ilihusika.

Kwa hiyo, kuna uhusiano mkubwa kati ya NENO na IMANI.

Yohana 1:1,3 - [1] ‘Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.’

[3] ‘Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.’

Waebrania 11:3 - [3] ‘Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.’

9/17/19, 18:34 - +255 763 194 9**: Ameni,sema baba tupone…

9/17/19, 18:36 - PROPHET: Neno ni nini? Neno sio maandiko unayosoma kwenye biblia... ‘NENO ni wazo  unalolitamka kwa kinywa chako kwa kukiri / maombi ambalo uhalisia wake ni wa kiroho.’

Warumi 10:8 - [8] ‘Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.’

Yohana 6:63 - [63] ‘Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.’

Mawazo mema uliyanayo kuhusiana na maisha yako ndio UZIMA wenyewe ambao ukianza kuukiri linakuwa NENO lako katika maisha yako...hilo NENO usipo jiaminisha kwa kujishawishi ili uwe na IMANI kwenye hilo hakuna namna mawazo yako yatakuja kutimia katika maisha yako.

Na hilo halitegemeani na kumuomba Mungu linategemeana na IMANI yako.

Kwa hiyo, nikisema simamia neno la Mungu, simaanishi simamia mistari kwenye biblia, hapana! ...ipo hivi, na naomba mjaribu kunielewa...naeleza ushirika kati ya NENO na IMANI pamoja na wewe:

Neno la Mungu ni yale mawazo yako mema kuhusiana na maisha yako...hilo ndio Neno (lako) La Mungu...kwa nini nasema hivyo? Biblia inasema IMANI chanzo chake ni kusikia NENO LA KRISTO. Kristo hapa ni roho iliyo ndani yako au ule uhalisia wa Mungu ambaye ndio roho yaani pumzi yake ndani yako...Huyo ndiye Kristo anaye zungumziwa!’

Mwanzo 2:7 – ‘BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.’

Kwa hiyo, ukikutana na jina ‘Kristo’ kwenye biblia, maana yake ni mfanano wa Mungu ndani yako, ambayo ndiyo roho yako wewe.

Wakolosai 1:27 - [27] ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, ‘nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.’

Watu wengi wanapenda kutumia maandiko kwa kuyakiri wakitegemea ndio yana nguvu bila kuelewa mchakato wa kutamka neno kwa Imani wakidhani maandiko ndio neno la Mungu.....maandiko ni muongozo wa kulifikia neno halisi la Mungu ndani yako.

Kwa hiyo, ili upate matokeo ya uzima katika maisha yako lazima uumbe kwanza huo uzima kupitia neon; lakini pia ili uzima huo udhihirike katika ulimwengu wa mwili ni lazima ujenge imani katika hilo neno ndio uzima utokeze.

Kwa hiyo, uhusiano kati ya NENO na IMANI ni kwamba, NENO linaumba na IMANI INADHIRISHA MATOKEO ya kile ulichokiumba rohoni kupitia NENO lako.

9/17/19, 19:03 - +255 763 194 9**: Amina kubwa!!

9/17/19, 19:03 - PROPHET: Shalom!

9/17/19, 19:04 - +255 763 194 9**: Shalom mtumishi, ubarikiwe na KRISTO!

9/17/19, 19:04 -PROPHET: Amina!

9/17/19, 19:47 - +255 754 650 6**: Asante mtumishi kwa mafundisho. Barikiwa sana!

9/17/19, 22:19 - +255 712 090 9**: Barikiwa sana Pastor J!

9/17/19, 22:28 - Vesta: Amen!

9/18/19, 00:43 - +255 767 520 7**: Mungu akubariki. Ila nina swali?

9/18/19, 00:43 - PROPHET:  Sawa unaweza uliza…

9/18/19, 00:55 - +255 767 520 7**: Swali: Sio kwamba Mungu anasikia unachosema? Unamaanisha, Mungu hasikii tunachoomba ila tunajiridhisha, Mungu hatusikii?

9/18/19, 01:02 -  PROPHET: Waebrania 11:6 – ‘Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; *kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,’ na kwamba, huwapa thawabu wale wamtafutao.

Nikisema Mungu hasikii tunachoomba namaanisha hivi...mtazamo wako katika maombi au kile unachokiomba ni muhimu sana...ukiomba kwa kuamini kuna Mungu mbinguni anayesikia, hutaomba kwa imani kwa sababu utafikiri matokeo ya maombi yako yanategemeana na Mungu unayemuomba wakati matokeo ya maombi yako yanategemeana na imani uliyonayo...

Kwa hiyo, kama matokeo ya maombi yanategemea imani uliyonayo, hivyo, Mungu hasikii maombi yako bali imani yako ndio inayoleta matokeo ya maombi yako.

9/18/19, 01:02 - +255 767 520 7**: Asante Baba yangu. Nimekupata.

9/18/19, 04:01 - +255 714 414 1**: ***Amen

9/19/19, 23:11 - PROPHET:  Shalom … Shalom!

9/19/19, 23:11 - PROPHET: Kesho nitaendelea na mafundisho.

9/19/19, 23:12 - PROPHET: Mungu anawapenda sana! Nawaombea Mpate mguso wa tofauti wa kiungu katika maisha yenu na muone Mungu kwa namna ya tofauti.

9/19/19, 23:49 - +255 717 930 2**: Amen mtumishi!

9/20/19, 01:02 - +255 713 626 4**: Ameeeen!

9/20/19, 01:04 - +255 714 414 1**: Amen!

9/20/19, 10:18 - Vesta: Amen!

9/21/19, 11:17 - PROPHET: Shalom  shalom!

9/21/19, 11:17 - PROPHET: Jana nilibanwa na huduma kidogo. Leo nitapata nafasi ya kufundisha. Mungu awainue zaidi na Zaidi.

9/21/19, 11:40 - Laura: Amen!

9/21/19, 12:38 - Vesta: Shalom, amen!

9/21/19, 12:51 - +255 717 930 2**: Amen!

9/21/19, 13:04 - +255 767 520 7**: Amina Baba!

9/21/19, 19:06 - PROPHET: Shalom shalom! Naendelea na mafundisho.

9/21/19, 19:08 - Laura: Shalom prophet, habari ya w-end?

9/21/19, 19:08 - PROPHET: Nzuri tu sijui ninyi mmeshidaje?

9/21/19, 19:09 - Laura: Tuko poa na tumebarikiwa saaana!

9/21/19, 19:17 - PROPHET: Amina Mungu mwema… Nilifundisha nikamalizia kuzungumzia kuhusu uhusiano kati ya imani na Neno la Mungu.

9/21/19, 19:22 - Vesta: Shalom!

9/21/19, 19:27 -PROPHET: Leo nataka nifundishe Neno la Mungu lililopo ndani yako na unavyoweza kulitumia kufanya kazi kwa njia ya Imani.

Leo kidogo nataka nitoe mawe na mifupa. Ndio maana nahitaji maswali yenu kwa sababu kuuliza ni kutaka kuelewa Zaidi.

9/21/19, 19:29 - Laura: …sawa prophet.

9/21/19, 19:31 -PROPHET: Kwanza kabisa nataka mjifunze na kuelewa kile nilichoanza kufundisha mwanzo ya Kuwa, neno la Mungu lipo ndani yako na sio ndani ya biblia.

Hapa sasa nitaonekana napingana na biblia! Hapana. Simaanishi hivyo...biblia imejaa maandiko yaliyovuviwa na Roho Mtakatifu ila haimaanishi biblia ni neno la Mungu lililo hai!

Neno la Mungu sio maandiko lakini maandiko yanaweza kukuelekeza kwenye neno la Mungu lilipo.

Maandiko yanaleta ufunuo na ufunuo huo lazima ukuelekeze kwenye neno husika kwa sababu neno ndio chanzo cha yote kufanyika. Neno la Mungu linapatikana ndani yako sio nje yako.Sikiliza unaweza ukapewa unabii...unaweza ukapewa ufunuo kuhusiana na tatizo lako lakini ufumbuzi halisi hautokani na unabii unaopewa; unatokana na Neno la Mungu linalotoka ndani yako.

Mengine yote yanayoweza kutokea nje ya wewe yanakuja kukuza imani yako ya kumuamini Mungu

Tuingie kwenye maandiko:

Yohana 1:1,3,10-11 - [1] ‘Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.’

[3] ‘Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.’

[10] ‘Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.’

[11] ‘Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.’

Neno la Mungu ni hai na ndio lilihusika kuumba kila kitu na hilo neno lipo ndani yetu kwa sababu Neno ni mfanano halisi wa Mungu ndani yetu; hilo ndio neno la Mungu lenye nguvu; kwa namna nyingine; huyo neno anaitwa Kristo- Ndani yetu, utukufu wa Mungu!

Wakolosai 1:27 - [27]ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni ‘Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.’

9/21/19, 19:56 - Laura: Mtumishi ☝ ndio! Sijapapatapata, naweza pewa unabii usitokee kwa hiyo natakiwa nikiri ndio utokee au nifunge na kuomba au? Tafadhali naomba nichambulie, maana, ninaona maunabii yanajaa kontena tu!

9/21/19, 19:57 -PROPHET: Neno la Mungu lipo ndani yetu siku zote kwa sababu tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu.

Sisi tu wake na ni uzao wake kiroho kama tukiamini hivyo...ili tuone udhihirisho wake ndani yetu lazima tuamini kuwa sisi ni uzao wa Mungu kiroho.

Yohana 1:11-12 - [11]Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake…

Kupokea unabii ni kupokea taarifa kuhusiana na mtazamo wa Mungu kuhusiana na maisha yako; yaani mapenzi ya Mungu kuhusiana na maisha yako.

Mara nyingi ni maelekezo...maonyo...kukutia moyo...na kukutaarifu mambo yajayo na jinsi ya kujiandaa kuyapokea au kuyaepuka.

Ila ili unabii huo utimie, unatakiwa umuamini yule aliyenyuma ya huo unabii, yaani Mungu aliyesababisha huo ujumbe uje...na lengo la huo ujumbe ni kuendelea kuimarisha imani yako.

Sasa, unachotakiwa ni kuondoa shaka yoyote uliyokuwa nayo kabla ya kupokea huo unabii, ndio lengo la kupokea unabii ili uamini Zaidi.

Kwa hiyo, utimiaji wa unabii huo unategemeana na jinsi unavyoendelea kuamini.

9/21/19, 20:04 - Laura: Ooooh … okay,nashukuru saaana kwa kunifahamisha vizuri, nimekuelewa sana. Asante sana.

9/21/19, 20:05 - PROPHET: Sawa tuendelee sasa…

9/21/19, 20:06 - Laura: Sawa!

9/21/19, 20:06 -PROPHET: Lazima ifike mahali ujitambue wewe ni nani wanza na MUNGU ni nani kwako na ana nafasi gani kwako.

9/21/19, 20:08 - +255 658 999 6**: Mtumishiii leooo umeamua kutupa Mawe.Kumbuka kuna slow learners!

9/21/19, 20:09 -PROPHET: Tunaenda pole pole na nimeruhusu maswali kwa wingi.

9/21/19, 20:09 - +255 717 930 2**: Dah, nabarikiwa sana na hili neon, endelea kutupa mawe mtumishi!

9/21/19, 20:10 - Kuna viwango vya kumtambua Mungu ni nani kwetu na Viwango vya kujitambua sisi ni nani kwa Mungu.

Tuanze kwa kumtambua Mungu ni nani. Mungu ni roho. ‘Na hiyo roho haipo mahali panapoitwa mbinguni.’

Ukilielewa hili utaanza kumjua Mungu ni nani!

9/21/19, 20:11 - +255 658 999 6**: Amiiinaaaaa!

9/21/19, 20:11 - +255 717 930 2**: Sawa! swali langu ni kwamba: unaweza ukapewa unabii na ukaamini na ukamuamini Mungu na kuwa na imani kabisa, sasa kwa nini unabii hautimii?

9/21/19, 20:12 -PROPHET: Yohana 4:24 - [24] ‘Mungu ni Roho,’ nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Haiwezekani uweke imani katika jambo lisitimie. Labda umeamini kwa hisia na sio kwa roho.

Inategemeana na namna ulivyojengewa hiyo Imani. Kwa ufupi, imani ni kupokea jambo kabla halijatokea; kuishi uhalisia wake kabla halijatimia. Imani sio kutarajia jambo litimie na kulisubiria hapana.

imani yako uliyoweka ni kusubiria jambo litimie ndio ulivyofundishwa kuhusiana na Imani, kwa hiyo, lazima utegemee vitu viku-boost kupandisha imani yako!

Imani ni katika mambo yasiyoonekana ....Huweki imani katika kupata kazi, unaweka imani kwa Mungu na kupata kazi inakuwa siyo matarajio inakuwa uhakika kwako.

+255 717 930 2**: Nimesoma Mara 5 hapa na Zaidi, kama sielewi hivi any way nitarudia tena. Sasa mtumishi ni vitu gani hivyo vinatakiwa viku-boost?

9/21/19, 20:20 -PROPHET: Hujaelewa vizuri.

Ngoja nitoe mfano. Umefundishwa ukitoa sadaka Mungu atatenda, sio?

Hiyo sio Imani. Sasa, hayo ni matarajio!

9/21/19, 20:21 - +255 658 999 6**: Amen!

9/21/19, 20:21 - +255 717 930 2**: Ndio…

9/21/19, 20:22 - PROPHET: Changamoto za watu wengi leo ni kwamba, wanafundishwa kuweka matarajio na sio kuwa na Imani. Unatarajia kupokea kitu kutoka kwa Mungu kwa sababu umetoa sadaka…

Na nakwambia, hiyo ni kama kucheza Tatu Mzuka!

9/21/19, 20:23 - +255 717 930 2**: Kweli kabisa nimesoma zaid ya Mara 6 ila nimeanza kukuelewa, tatizo mawe yako mazito!

9/21/19, 20:24 - PROPHET: Imani sio matarajio imani ni uhakika…

Na Mungu alivyomuumba mwanadamu; amemuumba katika namna ya kuwa chochote atakachoweka imani kwa hicho kitatimia…

Ndio maana nikakuambia hakuna jambo ambalo utaamini na lisitimie hata ukiamini katika uongo utatimia tu!

9/21/19, 20:24 - PROPHET: Imani ina nguvu hiyo!

9/21/19, 20:25 - PROPHET: Nimeeleza kwa ufupi, nitaeleza zaidi ila nirudi kwenye somo maana hapo nilikuwa ninajibu swali na somo litafika hadi huko tena…

9/21/19, 20:27 - +255 717 930 2**: Amen!

9/21/19, 20:29 - PROPHET: Mungu ni roho! Ukielewa Mungu ni roho unatakiwa uelewe kuwa huyu roho siyo roho ambae yupo eneo linaloitwa mbinguni. Watu wengi wanamuabudu Mungu ambaye yuko mbali na wao.

Nikisema hivi, namaanisha wengi hawana Mungu pamoja nao wana Mungu aliye mbinguni yani mbali sana nao. Ndio maana kuna hizi lugha zinaonekana ni nzuri lakini zinakufanya upishane na uwepo wa Mungu,kusema: namngojea Bwana: ni kana kwamba huyo Bwana hayupo pamoja na wewe.

Kusema Nautafuta uso wa Bwana: ni kana kwamba huyo Bwana haonekani kwako.

Hayo yote sio kweli ni lugha zinaonekana ni za unyenyekevu lakini sio lugha za wanaomjua Mungu wao.

Yesu alibishana na mwanamke kwenye kisima kuhusiana na hili; ambaye alikuwa anajua kuwa Mungu anapatikana Israel tu. Yesu akamwambia, anaabudu asichokijua. Kwa nini? Kwa sababu anamfungamanisha Roho  wa Mungu na eneo Fulani; wakati Mungu ni roho na yupo kila mahali na ndani ya kila kitu.

Yohana 4:22-23 - [22] ‘Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.’

[23] ‘Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.’

Yesu alivyosema wokovu unatoka kwa Wayahudi hamaanishi Wayahudi wa dini wale walioko Israel, hapana. Anamaanisha watu wenye mitazamo ya kiroho katika kumuelewa Mungu; sio kwamba Mungu anapatikana kwa Wayahudi.

Kwa hiyo, mtu mwenye mtazamo wa kiroho anaelewa Mungu ni roho yupo ndani yake na yupo kila mahali.

Ukianza kujifungamanisha na mtazamo wa kuwa Mungu anapatikana madhabahu fulani umekwishakuwa wa kimwili, hauna tena connection sahihi na Mungu.

9/21/19, 20:49 - +255 717 930 2**: Hapa sasa ndio pakuelewa Zaidi…

9/21/19, 20:50 - PROPHET: Sawa!

9/21/19, 20:50 - PROPHET: Niseme kitu…

9/21/19, 20:51 - PROPHET: Narudia tena nilichosema: Mungu ni roho na yupo kila mahali; hafungamanishwi na eneo na anaabudiwa kwa roho na kweli.

Ukielewa hili hutakuwa unalazimika kugusa madhabahu fulani ili uamini Mungu ametenda kwa sababu hata hapo ulipo Mungu yupo! Mungu ni roho. Tatizo wengi hawaamini hili kwa sababu hawafundishwi hivi. Wanafundishwa tofauti ili kufungamanishwa na eneo Fulani.

Sikia, ukianza kumfungamanisha Mungu kwenye kaeneo Fulani, unakuwa haupo rohoni, yaani, humuabudu Mungu rohoni.Hilo ni moja.

Ukishamkosa Mungu wa rohoni; umeshaingia mwilini, kwa sababu, mtazamo ni lazima uwe na uelewa wa kuwa, Mungu ni roho na yupo pamoja na wewe mahali popote hata ukiingia chooni yupo kwa sababu ni roho.

Ukishajenga mtazamo huo na ukaishi katika huo lazima uelewe kuwa pia Mungu ni kweli.

Kweli ni nini? Kweli ni kujuwa kuwa Mungu anaishi ndani yako. Hii kweli ndio Kweli inayoenda ku activate Lile Neno la Mungu, yaani, uweza Wa Mungu ulio ndani yako.

Kwa hiyo, ukishajuwa Mungu ni nani, lazima uelewe Mungu ni nani kwako.

Yesu alifundisha kuwa, Mungu ni Baba kwetu.

Mathayo 7:11 - [11] Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajuwa kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana ‘Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?’

Nikisema Mungu ni Baba, hii haimaanishi mtazamo wa Kimwili, hapana, ni mfano unaomaanisha kuwa Mungu ni chanzo cha maisha na kila kitu-ndio maana anaitwa Baba.

Ukimwelewa na kumjuwa Mungu kwa mfano wa Baba, yaani chanzo cha maisha yako na kila kitu utaweza kujenga uhusiano mzuri na huyo Baba au chanzo cha maisha yako.

Sasa nieleze kitu hapa:

Ndipo nitaishia hapa kwa leo. Biblia inaposema ombeni nanyi mtapewa, kwenye kiingereza neno liliotumika sio ‘pray and you shall receive. ’Limetumika neno ‘ASK.’

Ask sio kuomba...ask ni kuuliza swali. Tuko pamoja?

Yesu aliposema Ask and you shall receive, alimaanisha- Uliza na utapewa majibu, sio omba nanyi mtapewa.

Nimesema, Mungu kama Baba ni chanzo au source ya kila kitu katika maisha yako. Kumuuliza huyo Baba maswali ni ku-provoke attention yake kwako.

Mathayo 7:9 - [9] ‘Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?’

Jenga tabia yakumuuliza Mungu kuhusiana na jambo fulani katika maisha yako.

Lazima upate majibu.

Uliza kile unachotaka kupokea sio kuomba kile unachotaka kupokea. Uliza… Jibu utakalo pata ndio mapenzi ya Mungu kuhusiana na hilo unalolitaka.

Kwa leo naishia hapa.

Shalom!

9/21/19, 23:49 - Vesta: shikamoo … kizungu!

9/21/19, 23:50 - Vesta: Hapa sijaelewa!

9/22/19, 00:50 - Laura: Ameeen…barikiwa saaana!

9/22/19, 10:22 - +255 767 520 7**: Amina. Asante kwa Neno la uzima!

9/24/19, 11:46 - PROPHET: Shalom watumishi… Mnaendeleaje?

Natumaini wote wazima.

9/24/19, 11:48 - +255 714 414 1**: Mungu ni mwema***

9/24/19, 12:08 - +255 712 090 9**: Shalom tunaendelea vyema. Sijui wewe?

9/24/19, 12:09 - +255 678 827 4**: Tuko vyema!

9/24/19, 12:11 - Vesta: Mungu nimwema sana…

9/24/19, 12:12 - +255 763 194 9**: Shalom man of God! For God’s sake, I'm extremely ok!

9/24/19, 12:13 - PROPHET: Amina, nafurahi kusikia hivyo!

Nina maombi kwa ajili yenu.Natuma kwa voice note!

9/24/19, 12:15 - Vesta: Waiting…

9/24/19, 12:15 - +255 714 414 1**: Amen***

9/24/19, 12:18 - +255 763 194 9**: Amina

9/24/19, 12:18 - +255 682 867 1**: Amen!

9/24/19, 12:21 - PROPHET:

9/24/19, 12:27 - +255 682 867 1**: Amina!

9/24/19, 12:28 - +255 763 194 9**: Amina MUNGU wa mbinguni akubariki sana, nimepokea yote katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI! Amen!

9/24/19, 12:53 - Vesta: Amina mtumishi nimepokea!

9/24/19, 14:26 - +255 714 414 1**: Amen ***nimepokea katika Jina la Yesu.

9/24/19, 14:53 - +255 717 930 2**: Ameeeeeeeeeen!

9/26/19, 20:20 - PROPHET: Shalom shalom!

9/26/19, 20:20 - PROPHET: Mnaendeleaje! Leo naendelea kufundisha.

9/26/19, 20:33 - PROPHET: added +255 744 384 5**

9/26/19, 20:27 - +255 719 513 9**: Shalom

9/26/19, 20:27 - +255 719 513 9**: Hatujambo

9/26/19, 20:29 - My Son Profet: Kuna kitu nilikuwa nafundisha… Nilikuwa nafundisha kanuni ya mathayo 7:7 ya ‘ASK AND IT SHALL BE GIVEN.’

Kanuni hii aliifundisha Yesu lakini akilenga mtazamo wa kumtegemea Mungu kama Baba au chanzo cha maisha yako.

Nje ya kumtegemea Mungu kama chanzo cha maisha yako unaweza sema unamwamini Mungu lakini kama humtambui kuwa ni chanzo cha maisha yako itakuwa ni vigumu kuona udhihirisho wake katika maisha yako.

Na ili uelewe hivyo, ni lazima umwelewe Mungu katika mtazamo wa kiroho na kuwa yeye ni roho.

Kwa hiyo, ukimwelewa Mungu kwa mtazamo wa kuwa ni Baba, utaelewa kuwa Mungu anakupenda na anawajibika katika kutunza maisha yako kama vile Baba yako wa mwilini alivyowajibika kukutunza na kukupenda.

Ukiwa nje ya mtazamo huo ni ngumu kumjua Mungu katika roho na kweli.

9/26/19, 20:39 - PROPHET: Leo nataka tutazame Kanuni ya Mathayo 7:7 ambayo Yesu aliifundisha.

 

"In teaching others we teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages