DARASA UK.10

 

DARASA UK. 10

 

WANAFUNZI WA KRISTO: 

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

 

 Prophet Joachim Francis

check bullet point red animation  "...wewe ni mrithi na mtawala

pamoja na Mungu."

 

...KUTOKA UKURASA WA 9

Changamoto ni kuwa, wengi wanaishia kuomba pasipo kuongeza kiwango chao cha ufahamu kupitia maarifa ya kujuwa kuwa wewe ni mrithi na mtawala pamoja na Mungu.

1:17-18

[17]Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjuwa yeye; [18] ‘macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;’ Simaanishi maombi ni mabaya hapana...namaanisha maombi bila ufahamu uliosahihi ni kupoteza muda. Unachotakiwa kuongeza sio kiwango cha kufunga na kuomba. Unatakiwa kuongeza kiwango cha kupata ufunuo na ufahamu kuhusiana na uhalisa wako kiroho katika ulimwengu wa roho. Kila kitu katika Ufalme wa Mungu au uhalisia wa kiroho wa Mungu kinafanya kazi kwa maarifa na sio maombi...

Maarifa au ufunuo huo kuhusiana na uhalisia wako wa kiroho ndio ‘NENO LA KRISTO’ ambalo kwa hilo ndio unatakiwa uliishi kila itwapo leo; hilo neno ndio mkate wako wa kila siku...mkate sio riziki au chakula...mkate unao zungumziwa hapa ni Kristo ambaye ni uhalisia wako wa kiroho sasa jinsi ulivyo ndani ya ulimwengu wa roho ambayo ndio asili yako mpya.

Mathayo 4:4

[4] ‘Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ Yohana 6:35,57-58 [35] ‘Yesu akawaambia, Mimi ndimi mkate wa uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.’ [57] ‘Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.’ [58] ‘Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.’ Kila kitu Mungu alishatufanyia na akatupa kupitia Mwanae Kristo Yesu. Hivyo vitu ni vyetu ila tunatakiwa tukue katika maarifa ya kujifahamu sisi katika mtazamo wa Mwanae Kristo kama mwana wa Mungu tukiwa Wana wa Mungu pia.

Yohana 1:12 [12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; Sisi tumefanyika watawala kiroho na makuhani kiroho na wana wa Mungu pia kiroho kupitia Kristo Yesu. Ufunuo 5:10 ‘ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.’ Uhalisia wetu kiroho ni wa kifalme duniani na kikuhani kiroho. Usipo elewa hili hakuna namna unaweza kuwa mshindi katika hali yoyote kinyume na changamoto za kidunia na za kiroho pia. Unavyokimbilia kwa watumishi wa aina yoyote jukumu lao ni kukufunulia uhalisia wako kiroho kama mfalme na kuhani na sio kukufanya muumini au kondoo wake au mtoto wake kiroho...na wakristo wengi hawajitambui sababu wamefanywa watumwa kiroho na kimwili badala ya kujielewa kuwa wao ni wafalme na makuhani kiroho.

Matokeo yake unakuta wengi wapo na wanazunguka makanisani wakitafuta mababa wa kiroho na bado hawaoni matokeo ya huyo Mungu wanayemtafuta kila siku kwa sababu hawajijui wao ni akina nani kiroho na kimwili. Kwa hiyo, imani huachiliwa pale mwanadamu yeyote anapoelewa nafasi yake au uhalisia wake katika ulimwengu wa roho kiroho. Imani hiyo inaachilia uwezo au nguvu katika maisha yake ya kila siku...imani hiyo ni udhihirisho wa maarifa aliyonayo na ufahamu kuhusu Kristo uhalisia wa kiroho. Kwa hiyo, Kristo aliyefufuka wakati wa ubatizo ni Kristo aliye ndani yetu ambaye kwa huyo tunahesabiwa haki kutoka kwenye asili ya dhambi. Kristo alivyofufuka baada ya Yesu kufa kimwili na kufufuka kiroho ndio tulipata nafasi ya kuwa warithi pamoja naye katika ulimwengu wa roho.

Haya mambo yote yalifanyika kiroho na uelewa wa haya yote huleta matokeo yake tofauti. Kwa leo nilikuwa naeleza na kufundisha kuhusu ufufuo wa baada ya Yesu kufa na uhalisia wake...nitarudia kufundisha tena kutofautisha Ufufuo wa ubatizo na ufufuo wa baada ya kufa kwa Yesu ili mpate kuelewa kwa kina.

Shalom!

10/16/19, 20:48 - +255 717 930 2**: Huyu mimi kabisaaaaa…asante mtumishi kwa neno!

10/16/19, 23:21 - Vesta: Amen!

10/17/19, 10:27 - +255 719 739 3**: Ki-msingi ina maana kabla ya Yesu kufa hakuwa Kristo; amefanyika Kristo Yesu baada ya ufufuko, ambaye ni Kristo mfufuka.

10/17/19, 10:53 - PROPHET: Ndio! Alivyokuwa hai alikuwa Yesu Kristo ...Kristo akiwa ndani yake...baada ya kufa akafanyika Kristo Yesu wakati wa ufufuo.

10/17/19, 18:18 - PROPHET:  Shalom!

10/17/19, 18:19 - PROPHET: Kuna kitu Mungu kaniambia nifanye leo humu kwenye hili group. Najuwa kuna wengi ambao hawajawahi ku-experience nguvu za Roho Mtakatifu; mnasoma kwenye biblia; mnasikia kuwa kuna mtu roho kamshukia. Wengine walishawahi ku-exprerience kwa sehemu.

10/17/19, 18:21 - PROPHET:  Ila leo Mungu ameniahidi kuwa kwa wale wanaotaka waguswe na Roho Mtakatifu nafasi imepatikana kwa siku hii. Kama umepata nafasi kusoma maneno haya: (unavyosoma ndivyo Roho Mtakatifu anavyokugusa.) Roho Mtakatifu anakupa sasa hivi nguvu. Kwa pale unapohitaji nguvu ya ziada katika maisha yako. Pale unaposhindwa Roho Mtakatifu anaenda kukuwezesha sasa hivi.

Shalom!

10/17/19, 18:29 - +255 766 919 8**: Amen!

10/17/19, 18:54 - +255 714 414 1**: Amen!

10/17/19, 20:30 - +255 713 626 4**: ameeeen!

10/17/19, 20:30 - +255 717 930 2**: ***

10/18/19, 00:33 - +255 717 930 2**: Mtumishi ni kweli huu ujumbe umenikamata niliposhika simu nakusoma huu ujumbe ghafla mwili wangu ukatikisika kwa nguvu; yaaani hata sijui nielezeeje. Barikiwa!

10/18/19, 00:36 - PROPHET:  Aminaaa!

10/18/19, 00:37 - PROPHET: Ni nguvu kweli ipo ya Mungu sio utani!

10/18/19, 14:51 - Vesta: Shalom, miye ndio nasoma sasa hivi…

10/18/19, 19:39 - Profet Daniel: Amen prophet... Kuna uvuvio sio wa kawaida!

10/18/19, 19:43 - Profet Daniel: Nasikia ndimi za moto…

10/20/19, 18:51 - PROPHET: Shalom shalom!

10/20/19, 18:52 - PROPHET: Natumaini wote wazima

10/20/19, 18:52 - +255 719 513 9**: Shalom!

10/20/19, 18:52 - PROPHET: Nina habari njema.

10/20/19, 18:52 - +255 719 513 9**: Sisi wazima Mungu yu mwema.

10/20/19, 18:52 - PROPHET: Tumepata mahali pa kuabudia.

10/20/19, 18:53 - +255 766 919 8**: Shalom!

10/20/19, 18:53 - +255 766 919 8**: Mungu mkubwa!

10/20/19, 18:54 - PROPHET: Ni maeneo ya Posta Mpya ukumbi wa YWCA karibu na Ramada Hotel.

10/20/19, 18:55 - +255 658 999 6**: Amen!

10/20/19, 18:56 - +255 658 999 6**: Glory to God ni hostel anayoenda kukaa mwananguuu!

10/20/19, 18:56 - +255 658 999 6**: Haleluyaaa!

10/20/19, 18:56 - PROPHET: Aminaaaaa.

10/20/19, 18:57 - PROPHET: Nawakaribisha sana.

10/20/19, 18:57 - PROPHET: Kwa sasa hivi ibada itakuwa kila Jumapili.

10/20/19, 18:57 - +255 658 999 6**: Asante. NIMEFURAHII…

10/20/19, 18:57 - PROPHET:  Kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa mchana.

10/20/19, 18:58 - +255 658 999 6**: Amina.

10/20/19, 19:00 - PROPHET: Nawapenda sana pia nawaombea.

Kesho nitaendelea na mafundisho...

10/20/19, 19:02 - +255 719 513 9**: God is good!

10/20/19, 19:02 - +255 766 919 8**: Amina.

10/20/19, 19:06 - +255 763 194 9**: Amina mtumishi wa MUNGU, ubarikiwe saana, sasa ninauhakika hata nikifika usiku wa manane Dar es laam ninamahali pa kufikia! Nakuombea MUNGU wa mbinguni aendelee kukuinua! Uendelee kuwa juu Zaidi.

10/20/19, 19:07 - PROPHET: Aminaaa.

10/20/19, 19:11 - Vesta: Shalom!

10/20/19, 19:12 - Vesta: Amina Mungu wetu ni mwema.

10/20/19, 20:30 - +255 717 930 2**: Power!

10/20/19, 22:22 - +255 713 626 4**: Hongera sana, pakubwa!

10/21/19, 09:10 - +255 686 361 1**: Wow, hongera sana.

10/22/19, 19:51 - PROPHET: Shalom shalom! Natumaini mnaendelea vizuri. Nitaanza mafundisho  muda si mrefu.

10/22/19, 20:06 - +255 658 999 6**: Shalom

10/22/19, 20:17 - Vesta: Shalom

10/22/19, 20:38 - PROPHET: Leo naendelea kufundisha pale nilipoishia. Nilifundisha vitu vingi na vya kina kidogo ndio maana ikabidi niwe na fundisha kidogo kidogo kwa sababu ni elimu ya kina kidogo.

10/22/19, 20:40 - +255 754 650 6**: Shalom

10/22/19, 20:41 - PROPHET:  Lakini nilichofundisha wiki zilizopita kilikuwa kinaelezea tofauti ya Kristo Yesu...Yesu Kristo Na Kristo Uhalisia au Ufalme wa Mungu. Nimefanya hivyo ili tupate maana halisi ya maneno haya tunapokuwa tunasoma biblia hasa Agano JipyaWiki iliyopita nilikuwa na fafanua maana ya Yesu kubatizwa kwa maji mengi na nikagusia ufufuko wa Kristo uliofanyika kiroho. Kwa ufupi, ubatizo wa maji mengi wa Yesu uliwakilisha ondoleo la asili ya dhambi na ufufuo wa utukufu wa Mungu au Kristo ndani ya mwanadamu. Ubatizo huu ni wa kiroho ambao ndio unaitwa ‘Kubatizwa ndani ya Yesu Kristo.’

Warumi 6:4 ‘Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.’ Ubatizo huu ni ubatizo unaotendeka kwa njia ya imani na sio kwa kuzamishwa ndani ya maji...Kwa nini? Kwa sababu kuzamishwa kwake Yesu ndani ya maji mengi kuliwakilisha uhalisia wa kiroho uliokuwa unafanyika wakati anabatizwa Yesu kimwili ila haumaanishi kuwa watu ndio wabatizwe sasa kwa maji mengi.

Ndio maana ukisoma biblia yako ya Agano Jipya hakuna mahali utaona Yesu anawaagiza wanafunzi wake wakawabatize watu kwa maji mengi; utaona anasema tu wakawabatize watu kwa jina la Baba la Mwana na la Roho Mtakatifu. Sio maji mengi. Ubatizo ni tendo la imani sio la mwilini.

Wakolosai 2:12 ‘Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.’ ‘Ipo hivi, ubatizo aliokuwa anauzungumzia Yesu ni ubatizo kwa njia ya imani kwa kusadiki kuwa tulikufa pamoja na Yesu kiroho na tukafufuka naye kiroho.’

10/22/19, 20:54 - +255 754 486 0**: Shalom!

10/22/19, 20:55 - PROPHET:  Kusaidiki haya na kuamini haya ndio kunakufanya uwe ndani ya Kristo. Sasa kunatofauti hapa zinazojitokeza.Sifundishi kukosoa, nafundisha ili tujuwe ukweli. Watu wengi wanafahamu na wanafundishwa sana kuhusu kufa kwa Yesu kimwili. Ingawa mauti iliyomkuta Yesu kimwili sio yenye nguvu au ufunuo wa aina yeyote kwa sababu, aliyeenda kufa pale msalabani alikuwa ni Yesu wa mwilini. Kufa kwake pale msalabani kulikua ni kutimiza unabii ila sio kutimiza ufunuo. Nikisema kutimiza unabii namaanisha unabii uliokwisha kuwepo wa Agano la Kale.

Alivyokufa pale Yesu msalabani alikuwa anakufa kutimiza maandiko. Ila, ufunuo ulishatimia hata wakati Yesu yupo duniani; bado watu walikuwa wanaokoka kwa kumuamini Mungu kupitia yeye. Kuna watu pia walikuwa wanatoa pepo kwa jina la Yesu.  Kwa hiyo, ukisema umempokea Yesu ni sentensi ambayo haina uhalisia wa kutosha kwa sababu unayempokea ni Kristo ambaye ni roho kwa kusadiki kuwa mtu wako wa kale alikufa pamoja na Yesu na ukafufuka pamoja na Kristo kiroho. Hii ndio maana ya andiko linalozungumzia kuhusu kuzaliwa mara ya pili.

Yohana 3:5,7

(5) ‘Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.’ (7) ‘Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili.’ Kuzaliwa mara pili ni jambo la kiroho la kusadiki kupitia ubatizo wa Yesu. Ukielewa haya umekuwa kiumbe kipya kiroho. Kwa hiyo, ufufuo ni wa aina mbili: Ufufuo wa wakati wa ubatizo na ufufuo wa baada ya Yesu kufa. Hapa ndio kuna tofauti...ipi?   Lazima uelewe kuna mambo mawili Yesu aliyashinda.... ‘Nguvu ya asili ya dhambi’...na ‘nguvu za giza.’

Wakati Yesu anakufa kimwili kifo chake kilikuwa ni mlango wa kwenda kuzishinda nguvu za giza zilizokuwa zina muweka mwanadamu kifungoni’

Wakolosai 2:14-15 [14] ‘akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;' [15] 'akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.'

10/22/19, 21:28 - My Son Profet: Kwahiyo kusadiki kifo cha Yesu kimwili ni kuamini ya kuwa alizishinda nguvu za giza kwa ajili yetu...kuzishinda nguvu hizo za giza ni kuondoa uhalali wa nguvu za giza kutumiliki kiroho.

Wakolosao 1:13-14

[13] ‘Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;’ [14] ‘ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; Ukuu wa Kristo.’ Hiyo ndio maana halisi ya neno ‘UKOMBOZI’ au ‘DELIVERANCE.’ Kutolewa kwenye uhalali wa milki ya nguvu za giza kiroho kupitia kifo cha Yesu...kwa hiyo, maana yake ni kwamba, kifo cha Yesu ni gharama ya sisi kununuliwa kutoka kwenye milki za nguvu za giza.

Kwa hiyo, kuelewa ufufuo wa Yesu wakati akiwa  hai na wakati anakufa ni muhimu. Sasa, Yesu alivyokufa kimwili; Kristo alifufuka. Nataka sasa nielezee hili kwa upana na hapa nitawavuruga kabisa ila twende pole pole najuwa ni jambo jipya kwenu ila ndio ukweli. Na huu ndio msingi wa ufunuo wa mtu yeyote anaye mwamini Kristo. Nilvyokuwa naelezea maana ya neno Kristo, nilitoa tafsiri zifuatazo: ‘Kristo kama roho ambae ni kiumbe kipya.’ ‘Kristo kama uhalisia wa kiroho.’ ‘Kristo kama Mpakwa Mafuta aliyetabiriwa atazaliwa kama mwokozi.’

PROPHET: Roho Mtakatifu nisaidie nipate lugha sahihi kuelezea hili jambo… Wakati Yesu anakufa kimwili kuna jambo jipya lilikuwa linafanyika kiroho... mara nyingi watu wengi wanakiri mambo ya kuhusu Yesu bila kupata maana halisi ya kiroho iliyokuwa inafanyika; ndio maana wengi hawaoni matokeo au udhihirisho wake. Yesu alivyokuwa duniani biblia inasema, Yesu alisema, ‘anaenda kutuandalia makao’ lakini hakusema anaenda mbinguni, alisema anaenda kwa Baba. Ndio maana hata ukisoma biblia yako huwezi kuona mahali Yesu anasema mtu akiniamini mimi akifa ataenda mbinguni. Alichokuwa anasema, mtu atakaye mwamini yeye, ataishi milele...au atapata uzima wa milele.

Ukiona mahali Yesu anafundisha kuwa ukifa utaenda mbinguni, tuma humu huo mstari tutaujadili. Twende pole pole na taratibu. Kuna mambo mawili yapo.’ULIMWENGU WA ROHO’ na ‘UHALISA WA KIROHO.’

Nikisema uhalisia wa kiroho namaanisha chanzo cha mambo yote ya kiroho. Chanzo hicho au uhalisia huo ndio biblia inaliita ‘NENO.’

Yohana 1:1,3

[1] ‘Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.’ [3] ‘Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.’ ‘ULIMWENGU WA ROHO’ ni mjumuisho wa mkusanyiko wa vitu vilivyofanywa kwa hilo ‘NENO.’ Kwa hiyo, biblia imemtafsiri huyo NENO kuwa ‘KRISTO.’ Kwa maneno mengine Kristo anatafsiriwa pia kama ‘NENO la Mungu au uhalisia Wa kiroho au chanzo cha mambo ya kiroho yote.’ ’Ulimwengu wa roho upo ndani ya Kristo au ndani ya hilo NENO la Mungu.’ Neno ‘MBINGU’ au ‘MBINGUNI’ kwenye biblia limetafsiriwa kama ‘ULIMWENGU WA ROHO’ sio mahali ambapo tutaenda kukaa tukifa wala sio makao ambayo Yesu alisema anaenda kutuandalia.

Makao yetu ambayo Kristo alisema kupitia Yesu ni uhalisia wetu wa kiroho ambao ndio ndani ya Kristo au Neno la Mungu. Kwa lugha nyepesi kabisa Yesu alikuwa anasema anaturudisha kwenye chanzo chetu cha maisha ambacho ni Kristo au Neno la Mungu lililo hai. Kufuka kwa Kristo kiroho ni jambo la kiroho lililofanyika kuturejesha kwenye chanzo chetu cha maisha ambacho ni ‘NENO’ Au ‘Kuwa ndani ya Kristo.’ Kwa leo naishia hapa...nitaendelea tena… Mungu awabariki na awatunze sana, nawaombea.

10/22/19, 22:53 - Vesta: Amina Prophet, Mungu azidi kukuinua.

10/23/19, 06:07 - +255 714 414 1**: ***Amenubarikiwe mnoo!

10/24/19, 15:28 - +255 686 361 1**: Hongera Sana!

10/24/19, 16:14 - +255 767 520 7**: Shalom wapendwa wangu. Maombi yenu tafadhali, mama yangu anaumwa

10/24/19, 16:18 - Vesta: Shalom, Mungu wetu nimwema atapona!

10/25/19, 09:49 - PROPHET:  Shalom shalom!

10/25/19, 09:49 - PROPHET:  Natumaini mnaendelea vizuri.

Leo nakaribisha maswali kulingana na tulichokuwa tunajifunza na pia maswali yoyote mnayoweza kuwa nayo,

Karibuni.

10/25/19, 10:01 - +255 754 486 0**: Shalom mtumishi

10/25/19, 10:08 - +255 719 513 9**: Shalom

10/25/19, 10:08 - PROPHET: Nasubiri maswali.

10/25/19, 10:09 - Vesta: Shalom!

10/25/19, 10:42 - +255 714 414 1**: Shalom

10/25/19, 10:55 - Vesta: Nina swali, eti kabla yakuumbwa dunia kuna viumbe walikuwa wanaishi wakitambulika kama ‘majini.’ Je kuna ukweli hapo?

10/25/19, 11:04 - PROPHET:  Sawa najibu swali.Hapana, kulikuwa hakuna majini.

10/25/19, 12:40 - Vesta: Kulikuwa na nini?

10/25/19, 12:41 - PROPHET:  Ila kuna viumbe ambavyo Mungu aliviumba ambavyo vilikuwa vimeumbwa kama wasaidizi kwa mwanadamu.

Mwanzo 2:18-19

[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

[19]BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. Mungu alimuumbia Adamu wasaidizi kabla hajamuumba Hawa kutoka kwenye ubavu; biblia inasema akafanyiza kutoka kwenye ardhi mnyama wa msituni sasa tatizo kiswahili hakileti maana ya kutosha. Kwenye kiingereza neno lililo tumika ni BEAST, ukisoma king james version – ‘Beast’ hapo haimaanishi mnayama wa msituni.

Genesis 2:19

[19]And out of the ground the LORD God formed every ‘beast of the field’* and every fowl of the air; and brought them unto Adam to see what he would call them: and whatsoever Adam called every living creature, that was the name thereof.

10/25/19, 12:49 - Vesta: Sawa nimeelewa

10/25/19, 12:51 - PROPHET: Sasa walivyoumbwa hao viumbe ndio biblia inasema nyoka alikua mwerevu kuliko wanyama wote; biblia ya kiswahili imetumia neno nyoka ila kwa kiingereza neno lililotumika ni ‘Serpent’ hili neno serpent lina maanisha kiumbe mwenye muonekano wa jamii ya ‘REPTILE’ ila haimaanishi ni nyoka kama nyoka.

Genesis 3:1

[1]Now the serpent was more subtil than any beast of the field which the LORD God had made. And he said unto the woman, Yea, hath God said, Ye shall not eat of every tree of the garden? Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Huyu kiumbe alikuwa na uwezo wa kuongea…

10/25/19, 12:52 - Profet Daniel: Swali zuri na lina mlengo wa kina sana japokuwa halijawekwa sawa…

10/25/19, 12:52 - PROPHET:  Na alikuwa anafanana na Adamu yaani alikuwa ana tembea kwa miguu miwili na alikuwa na uwezo wa kuongea pia. Najuwa watu wengi wanasoma hiyo sehemu lakini hawajiulizi nyoka gani anaweza kuongea… Na kutembea kwa miguu,  Kwa hiyo, hayakuwa majini hayo ila ni viumbe vilivyoumbwa kwa namna ya kufanana na mwanadamu.

10/25/19, 12:56 - Vesta: …hapa sasa unanikoroga, alikuwa na miguu anafanana na Adam?

10/25/19, 12:56 - PROPHET:  Ndio, alikuwa na miguu sababu baada ya yale mambo kutokea alilaaniwa atembee kwa tumbo.

10/25/19, 12:58 - Vesta: Ahahaa!  Kumbe kabla hajalaaniwa alikuwa anatembea na kuongea ndipo baada ya kulaaniwa akawa haongei tena wala kutembea…

10/25/19, 12:59 - PROPHET: Ndio!

10/25/19, 13:38 - +255 766 919 8**: Mh!

10/25/19, 13:50 - Prophet Daniel:  Isaiah 13:21 - Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na ‘majini’ watacheza huko. Ni vema kufahamu kuwa dunia tuliyonayo imetokana na matengenezo ya dunia iliyokuwepo awali na kuangamizwa kwa maji na hivyo vitu vingi vilivyoumbwa baada yake vilitokeza na kupata uhai wa vitu vilivyokuwa kabla yake. Kabla ya dunia hii inayotokana na mwanzo sura ya kwanza, ifahamike ilikuwepo awali na wanadamu na viumbe vingine...mfano:

Mithali 8:22

BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale. Proverbs 8:22,26

[22]The LORD possessed me in the beginning of his way, before his works of old. [26]Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia; Proverbs 8:22,26,30-31 [26]While as yet he had not made the earth, nor the fields, nor the highest part of the dust of the world. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia; [30]Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake; [31]Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu; Na furaha yangu ilikuwa pamoja na ‘wanadamu’. Anayezungumziwa hapo kwenye Mithali 8 ni Yesu ambaye alikuwapo kwenye dunia ya kwanza sio hii ya Mwanzo sura 1 na biblia inasema aliishi na binadamu kwenye hiyo dunia kabla ya uumbaji wa pili.

Na ndio maana baada ya gharika ya kwanza kwenye uumbaji mpya BWANA akasema na ‘tufanye’ mtu kwa mfano wetu! Maana yake Mungu alikuwa na sura IMAGE ambayo aliishi nayo pamoja na wanadamu wa kwanza kabla ya Adamu; hivyo kwa sababu aliwaangamiza wote kwa maji; ilibidi uumbaji wa pili achukue mfano ambao alibaki nao mwenyewe; wazungu wanaoita PROTOTYPE - ndio aliitumia kwa Adamu.

Hata mimea haikuumbwa bali iliamriwa itokee maana ilikuwepo isipokuwa iliharibiwa na gharika. Hivyo, ulimwengu wa kwanza ulikuwa na viumbe ambao ni wanadamu wenye miili na roho ambao ni malaika nao hawa pia wana makundi manne. (kuna malaika wenye mbawa sita wanaitwa ‘Maserafi’- ‘Isaya 6:1’ hawa hukaa daima kwenye kiti cha enzi, pia kuna malaika wanaitwa ‘Makerubi’ ‘Ezekiel 10:1’ hawa wana mbawa nne na huwa wanatengeneza na kubeba uwepo wa Mungu, pia kuna malaika wanaitwa ‘Malaika  watumikao’ ‘Ebrania 1:14’ hawa huwa wana mbawa mbili tofauti na wengine;  hawa hutumwa duniani kuhudumu na kurudi mbinguni. Vile vile kundi la mwisho ni Malaika wanaovaa maumbo au miili ya binadamu; mfano Malaika 3 waliomtokea Ibrahimu kwenye mialoni ya mamre na hawa mara nyingine huitwa wana wa Mungu kama ilivyo katika Mwanzo 6. Malaika hawa wanauwezo kuvaa miili ya binadamu au maumbile kadha wa kadha ili kutimiza assignments zao na wanauwezo wa kula, kuvaa, hata kuoa au kuolewa kama binadamu wengine na kuwa watumishi pia ila hufanya kazi kwa siri sana, asili yao isijulikane mfano wa Nabii Eliya, Yonana mbatizaji, Henoko hata wale malaika wa makanisa 7 ya Asia kwenye Ufunuo wa Yohana.

10/25/19, 14:08 - Prophet Daniel: Tukirudi kwenye ishu ya ‘MAJINI’ kulingana na Isaya sura ya 13: Majini ni roho zinazoweza kuvaa maumbile au maumbo. Tofauti na mapepo na mashetani hawa majini huwa kikanda kulingana na desturi ya eneo husika. Mathalani, majini hutengenezwa na kuwepo kwa wingi ukanda wa pwani ‘Coastal Regions.’ Ukisoma tafsiri kwa kiingereza KJV   But wild beasts of the desert shall lie there; and their houses shall be full of doleful creatures; and owls shall dwell there, and ‘satyrs’ shall dance there.

Wanaitwa ‘SATYR’- maana yake roho zinazovaa miili au maumbo ya wanyama. Mara nyingi huwa Mbuzi ndio Maana kila anayemuona jini cha kwanza huona kwato au mfano wa mnyama; hii ni kulingana na asili yao.

Walawi 4:24

[24] kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi. Zamani za biblia ili mtu asamehewe dhambi lazima kuhani aweke mkono kwenye kichwa cha mbuzi ili kuhamisha dhambi ya mtu na kumwekea mbuzi kwa hiyo huyo mbuzi kuanzia hapo anavaa uhalisia wa binadamu kiroho na kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa.

Hii imekuwa sheria ya rohoni kuwa roho chafu inaweza kuwekewa umbo la mnyama ili kutimiza uovu kupitia nguvu ya sadaka ambayo ni damu ya mnyama. Ndio maana Jini hawezi kutenda bila damu hata tu ya njiwa inatosha ku-react.

10/25/19, 14:09 – Prophet Daniel: Hayo machache at least nimeongeza kitu.

10/25/19, 14:10 - Vesta: Nimeelewa vizuri!

10/25/19, 18:18 - +255 714 414 1**: Mimi naomba kuuliza swali juu ya malaika wanaoitwa 'Malaika Watumikao' ,je hao malaika ndio wale wanaokuja duniani kuchukua roho za watu wanaokata roho?

10/25/19, 18:34 - +255 763 194 9**: Amen mtumishi! Kwa mantiki hii kwa jinsi nilivyokuelewa ulivyotufafanulia na kutuelewesha ni hivi TUKISHAMUAMINI HUYU KRISTO YESU aliyendani YETU ni HAKI YETU KUWA NA UZIMA MIILINI MWETU na si muujiza wala si bahati nasibu kwa sababu ni ahadi yake tupate uzima wa milele,uzima ni afya njema, maisha mazuri, amani, furaha na mengine mengi, tafadhali, humu ndani ya group letu kama kuna mtu mgonjwa na alidake hilo ang'ang'ane nalo yeye mwenyewe. Alisema tusikae kimya tusemezane naye tumkumbushe tupate haki YETU  NI HAKIKA MUNGU WETU YUPO HAI ANAISHI NA ANATENDA,TENA ANAJIBU KWA WAKATI,KWAKE YOOOTE YANAWEZEKANA. Ameni!

10/25/19, 18:34 - +255 763 194 9**: Amekwisha pona kwa damu ya YESU KRISTO Wanazareti Mfalme wa Wayahudi!

10/25/19, 18:34 - +255 763 194 9**: Samahani mtumishi aan hapa nahisi kuchemka kwa mafundisho yako mazuri,kwa kuwa umetueleza kuwa YESU ALITUAHIDI KUISHI MILELE AU KUPATA UZIMA WA MILELE,BASI MIMI MWENZENU NIMELIKAMATA HILO SITAKI KUFA KABISA KIROHO NA KIMWILI PIA! JE NIKISEMA HIVYO KWANI NINAKUFURU?

10/25/19, 18:44 - PROPHET:  Hapana, upo sahihi kwa sababu kwa imani yako ndivyo itakavyo kuwa! Majibu yangu kwa hili swali yatakuwa ya kina kidogo, sijui upo tayari…

10/25/19, 18:47 – Prophet Daniel: Well, swali zuri.

Malaika watumikao huweza kuchukua roho ya mwanadamu inapotoka na kuingia ulimwengu wa Roho kama ilivyokuwa kwa Lazaro.

Luka 16:22

Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na ‘malaika’ mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwaAina hiyo ya malaika waliomchukuwa Lazaro baada ya kufa anaitwa ‘Aggelos’; ni aina za malaika watumikao kuwahudumia wanadamu. Hata hivyo, kwenye ishu ya kufa kwa maana ya tafsiri ya kutoka ulimwengu wa mwili na kuingia rohoni hapa hutegemea na speciality ama makusudi maalumu na kwa sababu hiyo hata aina nyingine ya malaika huweza kutumika. Mfano Nabii Eliya alipokuja kuchukuliwa kwenda mbinguni, alitumiwa magari ya moto ambayo huambatana na makerubi (ezekiel 10).

Pia Mussa alipokufa, alikuja kuchukuliwa na Mikaeli baada ya malaika wengine kushindwa kutokana na mabishano na shetani, ukisoma Yuda 1:9. Mikaeli ni malaika Mkuu pamoja na Gabriel na wengine hivyo wanakiwango sawa na makerubi maana wanasimama mbele za BWANA. Kiujumla inapotokea mwanadamu kuchukuliwa na malaika iwe ni kufa moja kwa moja au kuingia rohoni na kurudi hutegemea na makusudi na hivyo utendaji wa malaika huwa mpana sana.

10/25/19, 19:09 - +255 714 414 1**: ‘…nipo kwenye daladala ila nafuatilia.

10/25/19, 19:09 - +255 714 414 1**: ***asante!

10/25/19, 19:17 PROPHET: Ndio maana halisi ya ‘UZIMA WA MILELE.’ UKIANGALIA ELIYA, ALIKUFA LAKINI ALIKUJA KUPITIA YOHANA MBATIZAJI. KURUDI KWA MTU SIO KAMA ALIVYOKUWA BALI KUTIMIZA ‘KUSUDI’ AMBALO AWALI HAKULITIMIZA. Uzima wa milele kwa ufupi ni maisha yasiyo na mwisho; yanayo endelea. Kwa hiyo, mtu anaweza endelea kuishi lakini katika namna nyingine ila sio kama mnyama.

My brother Prophet Daniel ataendelea kutoa mwanga kidogo kuhusiana na hilo.

10/25/19, 19:27 - +255 714 414 1**: Sasa naanza kuelewa maana mtoto anaweza kuzaliwa ukasikia wanasema anafanana na mtu fulani ambaye tayari alishakufa, si ndio maana yake? Na mimi nikifa nitazaliwa tena?

10/25/19, 19:29 - PROPHET:  Hili jambo linavigezo vyake kuvifikia

10/25/19, 19:33 - Prophet Daniel: Hili swali la kina kirefu … ila nitakujibu kifupi.

Mwanadamu akifa au roho ya mwanadamu ikitoka ndani ya mwili, haiwezi kuzaliwa tena, maana binadamu amepewa kufa mara moja.

Ebrania 9:27

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; isipokuwa kusudi au assignment (mfano utumishi) uliyowekwa ndani ya mwanadamu unaweza kurudi kwa mwanadamu mwingine mfano Eliya na Elisha au Mussa na Joshua; Mungu alimwambia Joshua nitakuwa nawe kama nilivyokuwa na Mussa. Pia kama mwanadamu ndani ana roho isiyo ya binadamu na hakumaliza kusudi pia roho hiyo inaweza kuzaliwa tena kwa mwanadamu mwingine akawa ana maisha yanayofanana.

Matthayo 11:13-14

Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja. Nabii Eliya alizaliwa tena kupitia Yohana Mbatizaji sababu hakumaliza kusudi lake.

10/25/19, 19:39 - +255 714 414 1**: Oooh, ok!

10/25/19, 19:46 – Prophet Daniel: Umesema vema, Prophet Zion... Wakati mwingine yafaa kuwa makini na kitu kinaitwa ‘IMPARTATION’; maana, unashiriki roho ya mtumishi mwingine na kusudi lake ikitokea hajakamilisha inaweza kuwa shida kwako.

 

(Mafundisho yanaendelea...DARASA LA UK> 11)

 

"In teaching others we teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages