DARASA UK. 11

 

DARASA UK.11

WANAFUNZI WA KRISTO

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

 

https://userfiles-secure.educatorpages.com/userfiles/prophetjoachim/PROPHET%20JOACHIM%20PHOTO%202%20WHITE%20SUIT.jpg

 

Prophet Joachim Francis

check bullet point red animation   ... "Narejea tena kufundisha

juu ya IMANI."

...KUTOKA UK. 10

Mfano, pengine alitakiwa kuzaa mtumishi kama Yusufu badala yake akafunga kizazi au kukilima kabisa, hivyo ukishiriki sehemu ya roho yake na hilo deni utalipa pia.

10/25/19, 19:50 - +255 714 414 1**: Mnatutisha

10/25/19, 20:37 - Vesta: Sasa Roho Mtakatifu anaanza kufanya kazi ya mimi kuelewa neno…

10/26/19, 11:21 - PROPHET: Shalom

10/26/19, 11:22 - +255 763 194 9**: Shalom

10/26/19, 11:23 - +255 744 384 5**: Shalom

10/26/19, 11:23 - PROPHET: Kesho ibada itakuwepo...ila nilitaka nitoe taarifa kama kutakuwepo na watu watakao hitaji huduma ya maombi ...kwa uponyaji au deliverance kesho watu wa aina hiyo wanaweza kuletwa.

10/26/19, 11:33 - +255 763 194 9**: Amina

10/26/19, 11:36 - +255 754 486 0**: Amen

10/26/19, 11:38 - PROPHET: Na pia kwa councelling pia tutakuwepo watumishi kumhudumia mtu atakayehitaji kuonana na prophet one on one baada ya ibada.

10/26/19, 12:04 - Vesta: Shalom

10/28/19, 09:05 - PROPHET: Shalom

10/28/19, 09:05 - PROPHET:  Mnaendeleaje?

10/28/19, 09:05 - +255 719 513 9**: Shalom

10/28/19, 09:06 - PROPHET: Vizuri! Leo nitaendele na mafundisho.

10/28/19, 09:08 - Vesta: Shalom Prophet, I'm good thanks to almighty God.

10/28/19, 09:09 - +255 714 414 1**: Shalom, Mungu ni Mwema.

10/28/19, 14:17 - +255 719 739 3**: Shalom

10/28/19, 21:20 - PROPHET:  Shalom

10/28/19, 21:33 - +255 719 513 9**: Shalom prophet!

10/28/19, 21:39 - +255 766 919 8**: Shalom!

10/28/19, 21:57 - +255 717 930 2**: Amen

10/28/19, 21:58 - PROPHET: Nitafundisha

10/28/19, 21:58 - +255 717 930 2**: Leo nimeelewa kidogo kidogo, barikiwa mtumishi.

10/28/19, 21:58 - PROPHET: Leo

10/28/19, 21:59 - PROPHET:  Ila Atajibiwa.

10/30/19, 08:21 - PROPHET: Shalom

10/30/19, 08:21 - PROPHET: Hope

10/30/19, 08:22 - +255 719 513 9**: Shalom prophet

10/30/19, 08:22 - +255 719 513 9**: Hatujambo.

10/30/19, 08:24 - PROPHET:  Namshukuru Mungu kwa ajili yenu

10/30/19, 08:35 - Vesta: Shalom!

10/30/19, 09:50 - +255 714 414 1**: Shalom

10/30/19, 11:24 - +255 719 739 3**: Shalom

10/30/19, 11:25 - PROPHET: Nitaendelea

10/30/19, 12:04 - +255 719 739 3**: Amina

10/30/19, 19:17 - PROPHET: Shalom

10/30/19, 19:18 - PROPHET: Tunaendelea

10/30/19, 19:22 - PROPHET: added +255 655 651 5**

10/30/19, 19:23 - Profet: Nilikuwa nafundisha somo la KUWA NDANI YA KRISTO, nalisimamisha kwa sasa.

Naanza kufundisha kuhusu ‘IMANI’ tena.

Kwa hiyo, narudia kwa sababu ya msingi wa mafundisho na elimu ya kumjuwa Mungu imetokea kwenye IMANI na hakuna jambo lolote mwanadamu anaweza kulifanya hapa duniani likaletea matokeo pasipo kuwa na IMANI.

Changamoto iliyokuwepo ni kwamba IMANI kama imani haifundishwi katika mtazamo wa uwezo unaoweza kutumika katika maisha yetu ya kila siku.

Imani inafundishwa katika mazingira ya kiroho zaidi kuliko katika mazingira ya uhalisia wa maisha. Na wengi ukiwatajia neno IMANI akili zao zinaanza kuwaza kanisani au Mungu bila kujuwa imani inaanzia kwa mtu binafsi na anavyoishi yeye kama yeye.

Kinachowatesa watu wengi leo ni kutokuwa na imani kwa sababu hawajui imani ni nini na inafanyaje kazi.

Kuna kipindi nilikuwa nafundisha nikasema Imani haihusiani na Mungu kwanza inahusiana na wewe binafsi...siri ya wewe kufanikiwa hapa duniani sio Mungu bali ni IMANIIli kuelewa hili nililo lisema, unatakiwa uelewe mwanadamu ameumbwa kutii kanuni zilizowekwa kwa ajili yake ili afanikiwe. Ni kanuni ambazo Mungu aliziweka na kwa kuzifuata unajiweka katika nafasi ya kufanikiwa.

Leo nitafundisha kanuni za kuwa na IMANI kwa sababu imani haiangalii wewe umeokoka; hujaokoka; wewe unaishi maisha ya kumpendeza Mungu au hapana.’ Imani ni KANUNI ambayo ukiifuata utapata matokeo.’ Kwanza, tuelewe imani ni nini hasa na inahusiana na nini?

11:1 [1] ‘Now faith is the substance of things hoped for, the evidence of things not seen.’ ‘Basi   kuwa na hakika mambo , mambo .’ Nimeweka ili tupate . Tafsiri ya neno Imani:

‘Ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana.’

Hii sentensi ukiisoma juu juu huwezi ukaelewa maana yake ni nini na wengi wanaisoma hii mistari wasipate maana ya ndani kuhusiana na kile kinachomaanishwa hapo.

10/30/19, 19:58 - PROPHET: Imani ina kanuni Tatu za msingi na ndizo ambazo nitazieleza leo.

Kanuni ya Kwanza ni ‘IMANI INAUMBIKA PALE MTU ANAPOKUWA NA MATARAJIO FULANI.’

Kanuni ya Pili ni ‘IMANI INAJENGEKA PALE MTU ANAPOKUWA NA UHAKIKA JUU YA HAYO MATARAJIO ALIYOJIWEKEA.’

Kanuni ya Tatu ni ‘UHAKIKA HUO UNAACHILIA NGUVU KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO KUTHIBITISHA NA KUWEZESHA MATARAJIO HAYO YATIMIE.’

Hili jambo halina cha Muislamu...Mkristo...Mpagani...Mchawi...Muabudu Mizimu...Mashetani...ni ‘KANUNI’ ambayo usipo ifuata haita kuletea matokeo na ukiifuata inakuletea matokeo. Kinachofanya watu wapokee wakienda kwa watumishi wa Mungu wawe wa ukweli au wasio wa ukweli...wenye upako  au wasio na upako ...kwa waganga wenye nguvu au wasio na nguvu ni IMANI huyo mtu anayokuwa nayo pindi anapoenda kutafuta suluhisho huko.

Upako sio unaosababisha mtu apokee kwa sababu upako huo au nguvu hiyo ya kiroho haifanyi kazi peke yake...inategemeana na imani ambayo tayari anayetaka apokee anayo; ndio maana kila mahali Yesu alipokuwa anaombea watu baada ya wao kuwa huru, kupona au kupokea haja ya mioyo yao huwa anawaambia kuwa imani yao ndio imewatendea hayo, sio Mungu.

Na hii ndio siri kubwa ya kufanya watu wapokee kutoka kwa Mungu kwa kujua namna ya kucheza na imani za watu ili waamini kupokea. Sasa wengi wanafikiri mtumishi fulani ndio ana upako sana wakati katika uhalisia anajua namna ya kukuza imani za watu ili wapokee. Ipo hivi, ulimwengu wa roho upo muda wote unafanya kazi....haupumziki kupokea kitu kutoka kwenye ulimwengu wa roho kudhihirika kimwili; inategemeana na imani mhusika aliyo nayo; sio maombi ...kama hakuna imani hakuna chochote kinachoweza kutokea kwa sababu lazima kuwe na uwiano na usawa pande zote mbili.

Sasa, wengi wanapenda sana wapokee kutoka kwa Mungu lakini hawana matarajio yoyote....nikizungumzia matarajio nazungumzia mlengo fulani au shabaha fulani uliyojiwekea; sasa hapa ndio maarifa ya imani yanapoanzia.

Usipokuwa na matarajio au lengo fulani unalotaka litimie hakuna namna utakuwa na imani itakayo kufikisha mahali. Lazima ufahamu ya kuwa matarajio hayo yasiwe mengi kwa sababu ni jambo linalo hitaji focus; kwa hiyo, liwe ni tarajio moja.

Matarajio huleta matumaini na matumaini huzaa uhakika wa jambo lile unalolitarajia.

5:1

‘Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.’ Unavyosoma biblia na kukutana na hizi lugha kama ‘kuhesabiwa haki itokayo’; ‘kwa imani’ unatakiwa uelewe kuhesabiwa haki kuna maanisha nini kwa sababu ni lugha za mafumbo. Haki kwa ufupi ni ‘KUSTAHILISHWA’ kwa kuwa na haki juu ya jambo fulani kuwa wewe ndio mmiliki. Lakini kustahilishwa huku ni kwa IMANI. Kwa hiyo, ni lazima uelewe imani hiyo inafanyaje kazi.

Biblia inasema, Imani ni kuwa na uhakika...na uhakika huo unatokana na kuwa na matarajio fulani...na pia nikasema matarijio huleta matumaini ila matumaini hayaji tu yenyewe kuna jambo huwa lina sababisha mtu hadi awe na matumaini au tumaini lijengeke ndani yake.

5:2-4

[2]ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. [3] ‘Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijuwa ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira;’ [4] ‘na kazi ya subira ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;’ Tatizo la leo ni kwamba watu wengi wanaotaka wawe na IMANI; hawataki kupitia mchakato wa imani hiyo kuimarika.

Hakuna namna ambavyo utataka ufanikiwe bila imani na hakuna imani isiyo na matumaini na hakuna matumaini yasiyo na subira, uvumilivu na hakuna uvumilivu kama hakuna matatizo (changamoto). Watu wengi wanataka waruke mchakato huu. Wanataka wapate tu matokeo mara moja paaa! Kama vile wanaenda kuchuma mboga tu shambani hapo zimeshaiva. ‘DON’T SKIP THE PROCESS / USIKWEPE MCHAKATO’. Na mchakato ninao uzungumzia hapa au biblia inayo uzungumzia ni mchakato wa kupitia vikwazo na matatizo ambayo ndio yanakutengenezea ‘SUBIRA na UVUMILIVU.’

Kama huna hivyo vitu viwili katika maisha; usitegemee mafanikio...uvumilivu ninao uzungumzia hapa ni uvumilivu wa kutimiza matarajio yako. Watu wote kwenye biblia unao ona wakipokea uponyaji kutoka kwa Yesu au miujiza unakuta walikaa na hayo matatizo kwa muda mrefu kabisa na Yesu anasema wazi kuwa imani zao zimewaponya sio Mungu!

Mfano mzuri ni mwanamke aliye kuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa miaka 12; alipokea uponyaji wa mara moja tu kwa kugusa pindo la vazi la Yesu na Yesu akamwambia imani yake imemponya! Unafikiri imani ya kumfanya apone mara moja aliitoa wapi kama sio kukaa kwenye hilo tatizo kwa muda mrefu? Biblia imesema wazi hapo kuwa SUBIRA / UVUMILIVU huleta ‘UTHABITI WA MOYO.’  Au kwa kiswahili chepesi ‘MSIMAMO.’

Matatizo unayoweza kupitia kutimiza matarajio yako yanakujengea msimamo katika maisha na msimamo huo unakupa matumaini usikate tamaa katika hayo malengo yako. Ukiona unapoteza matumaini mara kwa mara ni kwamba kuna namna unajaribu kukwepa mchakato wa kupitia changamoto fulani katika maisha. Au ni kwamba, unajaribu njia rahisi kutoka...kutoka kwako kuna tegemeana na kama umejifunza kutoka kwenye changamoto hiyo na kujifunza huko ni kwamba kuna kitu kipya cha ‘UVUMILIVU / SUBIRA’ kimeumbika ndani yako.

10/30/19, 21:00 - PROPHET:  Shalom!

Nitaendelea tena na mafundisho.

10/30/19, 22:00 - +255 713 626 4**:!

10/30/19, 22:38 - Laura: Shalom!

11/2/19, 22:22 - PROPHET:  added +255 763 081 4**

11/2/19, 22:33 - +255 763 081 4**: Nashukuruni Mungu awabariki sana!

11/2/19, 22:45 - +255 719 739 3**: Amina.

11/3/19, 08:07 - +255 712 400 0** left

11/5/19, 10:23 - PROPHET:  Shalom

11/5/19, 10:23 - My Son Profet: Natumaini

11/5/19, 10:23 - +255 766 919 8**: Shalom!

11/5/19, 10:43 - PROPHET: Leo kutakuwa na huduma ya councelling… Kwa atakayehitaji councelling leo unaweza kuni inbox. Shalom!

11/5/19, 10:49 - +255 714 414 1**: Shalom!

11/5/19, 10:50 - +255 719 513 9**: Shalom!

11/5/19, 11:40 - +255 744 384 5**: Shalom!

11/7/19, 09:56 - My Son Profet: Shalom

11/7/19, 09:56 - PROPHET: Natumaini

11/7/19, 09:56 - PROPHET: Leo ni siku ya maombezi na ushauri eneo letu la huduma.

11/7/19, 09:57 - PROPHET:  Kwa  inbox.

11/7/19, 09:57 - PROPHET:  Shalom!

11/7/19, 09:58 - +255 763 194 9**: Shalom! Ninamshukuru Mungu, mimi niko poa! taarifa, be blessed man of god.

11/7/19, 09:58 - PROPHET:  Amen!

11/7/19, 10:01 - +255 719 513 9**: Shalom

11/7/19, 10:01 - +255 719 513 9**: Mm

11/7/19, 10:06 - +255 714 414 1**: Shalom

11/10/19, 18:33 - PROPHET:  Shalom Mungu. !    mambo

11/10/19, 18:36 - +255 719 513 9**: Shalom

11/10/19, 18:36 - +255 719 513 9**: Tunaku-miss

11/10/19, 18:36 - +255 763 194 9**: Shalom, pole, -miss

11/10/19, 18:58 - +255 714 414 1**: Shalom, pole, - miss,  dose

11/10/19, 19:00 - PROPHET: Amina!

11/10/19, 19:00 - PROPHET: Jumatatu nitaendele na somo nililoliacha mara ya mwisho;  ila pia karibuni sana katika huduma, nawasubiria mnamisi mengi kweli!

11/10/19, 19:29 - +255 766 919 8**: Tutakaribia…

11/13/19, 14:14 - PROPHET:  added +255 654 333 5**

11/13/19, 14:14 - PROPHET: Shalom

11/13/19, 14:14 - My Son Profet: Mnaendeleaje

11/13/19, 14:15 - Vesta: Shalom, Mungu nimwema naendelea vizuri.

11/13/19, 14:17 - PROPHET: Leo nitafundisha tena… Niliishia kufundisha kuhusiana na Imani.

Ukiona unapoteza matumaini mara kwa mara ni kwamba kuna namna unajaribu kukwepa mchakato wa kupitia changamoto fulani katika maisha. Au ni kwamba, unajaribu njia rahisi kutoka...kutoka kwako kuna tegemeana na kama umejifunza kutoka kwenye changamoto hiyo na kujifunza huko ni kwamba kuna kitu kipya cha ‘UVUMILIVU / SUBIRA’ kimeumbika ndani yako.

11/13/19, 14:28 - PROPHET:  Nitaendelea kuanzia hapa.

11/13/19, 20:56 - PROPHET: Shalom

11/13/19, 20:59 - Vesta: Shalom!

11/13/19, 20:59 - PROPHET:  Wiki zilizopita niliishia hapa kwenye somo la Imani; nikielezea kuhusu namna IMANI ilivyo na umuhimu katika maishaNiliishia kuzungumzia kuhusu ‘UVUMILIVU / SUBIRA.’

Imani ni mfumo fulani wa maisha ambayo kila mtu lazima apitie ili kufanikisha jambo fulani katika maisha yetu ya kila siku....imani katika ukweli wake unahitaji kitu- kinaitwa SUBIRA / UVUMILIVU ili uweze kupokea mambo fulani katika maisha na kuona yanatimia. Ila tatizo kubwa ni watu wengi kutokuwa na huo uvumilivu wa kusubiri matokeo fulani yatokee.

Ni imani inayompendeza Mungu na hakuna namna yoyote mtu anaweza kumpendeza Mungu pasipo hiyo imani lakini unatakiwa uelewe namna gani ya imani inayoweza kumpendeza Mungu.

11/13/19, 21:04 - Vesta: Amina

11/13/19, 21:04 - PROPHET:  Biblia inapomzungumzia KWELI kuhusiana na MUNGU inamzungumzia Mungu kama ROHO. Kwa hiyo, unatakiwa uelewe biblia ikitumia neno ROHO inamaanisha nini.

Mungu anatafsiriwa kupitia maneno au misamiati miwili... ‘NENO’ ‘ROHO.’

Yohana 1:1

‘Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.’ Yohana 4:24 ‘Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika ROHO na KWELI.’

Sasa, biblia ikisema MUNGU NI NENO na ikisema MUNGU NI ROHO unatakiwa uelewe kinacho maanishwa hapo. ‘Biblia ikisema MUNGU NI NENO ni kwamba, NENO ni mfumo wa utendaji kazi aliouweka MUNGU, unaofanya kazi hapa duniani na ndio kilichotumika kumuumba mwanadamu na dunia hii kwa sababu NENO Ndio liliumba kila kitu kinachoonekana’ pasipo hilo NENO hakuna ambacho KINGEUMBWA. Kwa hiyo, NENO ni nini? ‘NENO ni ufahamu wa ufunuo wa mapenzi ya Mungu kuhusiana na maisha yetu hapa duniani.’

Biblia inaposema na NENO lilifanyika kuwa mwili; inamaanisha kuwa, mapenzi ya Mungu yalitimia hapa duniani kupitia mwanadamu. ‘Kwa hiyo, mfumo wa mapenzi ya Mungu kutimizwa hapa duniani kupitia mwanadamu ndio biblia inaita NENO.’

Yohana 1:14

‘Naye NENO alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.’ Huo ni upande mmoja wa Mungu. Upande wa pili ni pale biblia inaposema MUNGU NI ROHO ina maanisha nini? Neno ROHO lililotumika hapo linamaanisha ni  mambo yasiyo onekana katika ulimwengu wa roho; lakini pia nikisema ulimwengu wa roho, sizungumzii kitu ambacho kipo nje ya dunia hii tunayoishi, hapana, neno ROHO linalotumika hapa linatafsiri sawa na ‘PUMZI HAI.’

Mwanzo 2:7

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani ‘pumzi ya uhai’; mtu akawa nafsi hai. ‘Hii PUMZI HAI iliyo ndani ya nafsi ya mwanadamu ndio ROHO inayozumngumziwa kuwa ndio MUNGU; ambayo ndio sura na mfano wa Mungu ndani ya mwanadamu.’ Kwenye Agano Jipya inatafsiriwa kama ‘ROHO YA KRISTO.’ Kwa hiyo, biblia inaposema ulimwengu wa roho uliopo ndani ya KRISTO; inamaanisha vitu vyote ambavyo vipo katika mfumo wa mawazo au fikra ndani ya roho au pumzi hiyo ambavyo bado havionekani na kushikika ndani ya mwanadamu.

Waefeso1:3 ‘Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;’ ‘Kwa ufupi kabisa, ulimwengu wa roho upo ndani ya mwanadamu sio nje.’ Kwa hiyo, Yesu aliposema Mungu ni Roho alimaanisha kuwa Mungu ni PUMZI HAI inayoishi ndani ya mwanadamu. Hivyo, inampasa mwanadamu huyu amwabudu Mungu katika mfumo wa Roho na Kweli au Neno.

Yohana 4:24

‘Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.’ Kwa hiyo, kwa tafsiri moja nyepesi, Mungu ni ufunuo wa mapenzi au ahadi zake kuhusiana na maisha yako kupitia pumzi yake inayoishi ndani yako ambayo ndio chanzo cha maisha yako ya mwilini hapa duniani. Ndio maana biblia inasema baraka zetu zipo katika ulimwengu wa roho lakini ndani ya kristo au PUMZI hiyo ya Mungu iliyopo ndani yetu. Ili imani ifanye kazi unatakiwa uelewe kuwa imani chanzo chake ni kusikia au kuongozwa na ‘NENO LA KRISTO’ au NENO  la Mungu au kuishi kutimiza mapenzi ya Mungu kuhusiana na maisha yako. Mapenzi ya Mungu kwa ufupi ni yale yote mema ambayo ndio umeandaliwa kuyapokea na kuyapitia katika maisha kwa ajili ya faida yako.

Yeremia 29:11

‘Maana nayajuwa mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.’ Mawazo hayo ndio baraka hizo za Mungu zilizopo katika ulimwengu wa roho ndani yetu sisi. Ili hizo baraka zidhihirike IMANI ndio inayohitajiwa kufanya Baraka hizo zidhihirike....kwa hiyo, biblia inaposema PASIPO IMANI HUWEZI KUMPENDEZA MUNGU: inamaanisha, pasipo IMANI Baraka / mawazo mema ya Mungu / ahadi za Mungu kwa ajili ya maisha yako haziwezi kudhihirika.

Waebrania 11:6

‘Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.’ Hapa sasa ndio naanza kuzungumzia ‘PROCESS OF MANIFESTASTION’; ‘MCHAKATO WA UDHIHIRISHAJI WA VITU.’ Watu wanajuwa tu manifestation za mapepo ila kuna manifestation ya mafanikio pia. Mungu alipo umba dunia aliumba kitu endelevu kinachoishi na kujiongoza kwa kanuni na mfumo wake; halafu biblia inasema Mungu akapumzika...sasa nikikuambia kuanzia hapo Mungu bado anapumzika na alisha retire kutoka kwenye kazi ya aina yoyote wala hahusiki tena na hii dunia alicho kibakiza ni mfumo wa utendaji kazi unaofanya kazi...ni sawa sawa na mtu aliye tengeneza gari linaloweza endeshwa na mtu lakini huyo mtu akawa hana ujuzi wa kuendesha gari, halitamsaidia. Ndio watu wengi leo walivyo......wanamhusisha Mungu katika mambo mengi bila kujuwa Mungu alisha pumzika kitambo ila aliacha mfumo unaofanya kazi wenyewe...mfumo huo alioacha ni wazo lake au mapenzi yake kuhusiana na jambo fulani...

Mwanzo 2:2

‘Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe na kupumzika siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.’

11/13/19, 22:13 – Prophet Daniel: Huu ni ukweli usiojulikana kuwa Mungu alituachia WAZO au MAPENZI yake kama mfumo ambao ukiweza kung'amua kuna vitu vingi vinapatikana ndani yake. Watu wengi hawafahamu kuwa ulimwengu wa ROHO hauna sauti kama tunayoitumia wanadamu kwa kuwa sauti ya binadamu inahusisha mwili zaidi kutokana na mfumo wake; lakini rohoni hutumika zaidi WAZO kama mfumo wa mawasiliano.

Mwanzo 6:5

BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi ‘analowaza’ moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Sasa wengi wanafundishwa imani katika mtazamo wa maombi ...uponyaji...kutoa mapepo...miujiza....na kama ni imani basi wanafundishwa katika mtazamo wa kuombea changamoto wanayo pitia kwa Mungu ili Mungu afanye wepesi au awafanikishe katika hilo....ila niwafundisha kitu leo....sasa matokeo yake watu wanaomba sana wakifikiri ndio imani yenyewe, lakini kwa uhalisia maombi sio imani...kwa sababu haihusiani na udhihirisho wa aina yoyote...ukiomba usitegemee kuwa kuna kitu kitatendeka.

‘Imani hufanya kazi kwa MATENDO! MAOMBI!’

Yakobo 2:26

‘Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.’

‘MCHAKATO WA UDHIHIRISHAJI WA VITU / PROCESS OF MANIFESTATION.’ Ili jambo fulani litokee lazima upige hatua fulani au ufanye jambo fulani ndio jambo lingine litokee....katika uumbaji Mungu alivifanya vitu vidhihirike kwa kushaabihiana hatua kwa hatua kwa kufuata utaratibu wa tukio hadi tukio...kwa kiingereza hiki kitu kinaitwa ‘SYNCHRONIZATION’ and ‘PATTERNS.’

Mfano leo hii tunatumia vyakula mbali mbali vinavyotoka kwenye mimea tofauti...lakini hiyo mimea inatumia gesi asilia ambayo inazalishwa na hewa isiyo hitajika kutoka kwa viumbe hai pamoja na miili ya wanyama na binadamu waliokufa...madini hayo na hewa hiyo kutoka kwa wanyama walio hai na waliokufa  inatumika na hiyo mimea kutengeneza chakula na sisi tunatumia hiyo mimea kama chakula....

Vivyo hivyo biblia ikisema imani bila matendo imekufa inamaanisha pasipo kuchukua hatua fulani udhihirishaji wa mambo kutokea yanavyotarajiwa ni vigumu sana’ Kwa sababu kuna kitu kinatengenezwa kila wakati mtu anapopiga hatua juu ya kile anachokiamini. Kuna ‘UWEZEKANO / OPPORTUNITY / POSSIBILITY’ inayoumbika kwa hilo jambo analo lifanya kufanikiwa. Ila sasa wanadamu wengi wanataka kila akifanya kitu paaap! Mambo yafanikiwe, kitu ambacho sio kweli...sasa imani ndio inahusika hapa.

11/13/19, 22:24 - PROPHET:  Nitaendelea Imani. Shalom!

11/13/19, 22:25 - Vesta: Shalom, barikiwa mtumishi neno zuri sana.

11/13/19, 22:26 - PROPHET:  Amina!

11/13/19, 22:34 - Prophet Daniel: Too much blessed prophet!

11/13/19, 22:36 - PROPHET:  Amen prophet!

11/14/19, 07:47 - +255 766 919 8**: Amina!

11/19/19, 16:41 - PROPHET: added +255 653 087 ** and +255 677 896 0**

11/19/19, 16:41 - PROPHET: changed the subject from "WANAFUNZI WA KRISTO" to "VOICE OF CHRIST CENTER."

11/20/19, 15:02 - +255 767 540 7**: ** *Free scholarship for all students in any country of your choice*

*Apply here*** http://Bit.ly/2m70cSN

 **Share and help someone***

11/23/19, 09:01 - PROPHET: Shalom Mungu.

11/23/19, 09:02 - +255 654 333 5**: Shalom

11/23/19, 09:02 - PROPHET: I hope Nawakaribisha kwenye ibada yetu leo Buguruni Malapa (YWCA) kuanzia Saa 9 mchana, tutaanza. Kituo hiki ni cha muda tu. Ipo sehemu sahihi Mungu aliyotuandalia. Majira na nyakati nyatadhihirisha majira yakifika.

11/23/19, 16:57 - +255 767 520 7**: Nawatakia ibaada njema na Mungu azidi kuonekana kwenu. Amina.

11/23/19, 18:01 - PROPHET:  Amina!

11/24/19, 12:32 - +255 766 919 8**: Shalom!

Tumeumbwa au tupo duniani kwa kusudi gani?

11/24/19, 12:38 - PROPHET: Tumeumbwa kuwepo duniani kwa kutimiza kusudi la kwanza kabisa la Mungu. Kuijaza nchi na kuitawala. Hili ni kusudi general sio la binafsi kwa sababu kila MTU anakusudi lake pia binafsi duniani.

Mwanzo 1:28

[28]Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

11/24/19, 13:01 - +255 766 919 8**: Kwa namna au njia gani unaweza kuvumbua kusudi lako… Yaani kusudi uliloumbwa?

11/24/19, 13:08 - PROPHET:  Kusudi lako limefungamanishwa sana na vitu unapenda kufanya.

Msukumo unaoupata unaokusukuma ufanye vitu fulani au utimize mambo fulani katika maisha au mazingira uliyopo…

11/24/19, 15:42 - +255 654 333 5**: Kwa hiyo, kama mtu anapenda kufanya ukahaba, wizi, utapeli n.k. ina maana hilo ndo kusudi lake aliloumbwa nalo?

11/24/19, 15:43 - PROPHET:  Hakuna mtu amezaliwa anapenda ukahaba au wizi

Ukiangalia kinachomsukuma mtu kufanya hivyo ni umasikini sio kwamba anapenda.

Msukumo ninao uzungumzia sio unaosababishwa na hali ya mtu, bali msukumo unaotoka ndani ya mtu kulingana na kile anapenda kufanya.

Anayefanya ukahaba sio kwamba anapenda, hapendi hali tu ya maisha inamsukuma huko.

Ni sawa na mtu anayefanya biashara kupata hela sio kwamba anapenda.

11/24/19, 15:48 - +255 654 333 5**: Vipi wale wanaofanya ukahaba ili hali ni matajiri? Au ana roho chafu za ukahaba?

11/24/19, 15:54 - PROPHET:  ni roho!

USIKOSE WANAFUNZI WA KRISTO  'SEASON 2 -

AUDIO TEACHINGS. SEASON 3 VIDEO TEACHINGS.'    

BY Prophet Joachim Francis yes +255743238599 

 laugh

"In teaching teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages