DARASA UK.2

 

 

 

 

WANAFUNZI WA KRISTO 

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

https://userfiles-secure.educatorpages.com/userfiles/prophetjoachim/PROPHET%20JOACHIM%20PHOTO%202%20WHITE%20SUIT.jpg

Prophet Joachim Francis

 

2. purple world spin   AHADI ZA MUNGU NI NINI?

  

7/23/19, 16:57 - Prophet: Tunaendelea na somo la jana!

7/23/19, 17:01 - Prophet:  Jana tulikuwa tunazungumzia kuhusu maana halisi ya Mkristo na tuka pata ufafanuzi ya kuwa ukristo ni nini au Mkristo ni  nani. Tuliishia mahali ambapo nilisema ya kuwa, huwezi kurithi ahadi za Mungu pasipo kuongozwa na Roho Mtakatifu.  

7/23/19, 17:08 - Prophet:  AHADI ZA MUNGU NI NINI?   Ahadi za Mungu kwa ufupi ni ‘UZIMA!’ 

Uzima katika kila maeneo ya maisha yako kiroho na kimwili...sasa niweke wazi hili suala...Mungu hajawahi kuahidi watu wake kuwa atawafanya kuwa matajiri kifedha na mali....jambo hili halipo kabisa...na kama umekutana na mafundisho kama haya ni mafundisho potofu kabisa yatakayokufanya uhangaike kuomba kutoa sadaka ili Mungu akutajirishe. Niseme hivi, kilichoahidiwa na Mungu ni UZIMA...Lakini kuna mambo unaweza kufanya ukapata THAWABU kutoka kwa Mungu kwa sababu ya UTII wako kwa Roho Mtakatifu... Katika UZIMA ambao Mungu ameahidi kuna baraka za kiroho na za kimwili..  Baraka hizi ndiyo zinaweza kumfanikisha mtu na akawa tajiri.

7/23/19, 17:09 - +255 767 540 7**: Ni kweli waongozwao na Roho Mtakatifu hao ndio Wana wa Mungu. Mwana wa Mungu ni mrithi wa ahadi za Mungu.  

7/23/19, 17:11 - Prophet:  Sasa nitakachofundisha hapa ni cha muhimu sana sana na ndiyo kitakacho amuwa una nafasi gani katika Ufalme wa Mungu. Kufanikiwa hapa duniani kimwili na kiroho kunategemeana sana na namna unavyo mjuwa Mungu na siyo kuomba au kushiriki ibada sana. Sasa, kuna tofauti kati ya Mwana wa Mungu na Mtoto wa Mungu.

Wagalatia 4:1, 3, 5-7

[1] ‘Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;’

[3] ‘Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.’

  1. Kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ‘ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.’
  2. ‘Na kwa kuwa ninyi mmekuwa Wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.’

[7]Kama ni hivyo, ‘wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.’ Kuwa Mwana wa Mungu ni kuelewa nafasi yako mbele za Mungu; kama mtu anayestahili na syio mtu anayekirimiwa...kunatofauti kubwa mno hapa. 

Watu wengi wasioelewa hili ndiyo unakuta wanasema ni kwa rehema tu za Mungu. Mtu anayeongea kauli kama hizi ni mtu asiye elewa nafasi yake mbele za Mungu kama mtu anayestahili mambo mema kutoka kwa Baba yake.

Hapo ndiyo unakuwa mrithi...kuwa mrithi ni kwamba, unahaki na unastahili kurithi mali za wazazi wako; hivyo hivyo mbele za Mungu, ukijielewa wewe kuwa kama Mwana wa Mungu; huanzi kuomba kupewa bali unadai haki yako! 

Kumbuka nilisema huwezi rithi ahadi za Mungu pasipo kuongozwa na Roho Mtakatifu, sasa nielewe vizuri hapa:

Lazima ujifunze kuimarisha ushirika wako na Roho Mtakatifu kupitia neno la Mungu...Kivipi?  Unatakiwa umruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika kuelewa namna ya kusimamia ukweli wa neno la Mungu kwa kuliamini na kulitii ili uone matunda yake katika maisha yako.

Yohana 6:13

‘Lakini, yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.’

7/23/19, 17:27 - Prophet:  Roho mtakatifu hatakuja kukupa ufunuo pasipo kukuongoza kwenye neno. Ukiona unapewa ufunuo bila neno huyo siyo Roho Mtakatifu ni roho zidanganyazo roho chafu.

Kwa hiyo, huwezi kuwa na ushirika mzuri na Roho Mtakatifu pasipo kulijuwa neno la Mungu... Sasa, niwafundishe hiki kitu na ni cha muhimu sana. Ukitaka kumpokea Roho Mtakatifu kaa kwenye neno. KAA KWENYE MAFUNDISHO...YA KWELI NA NEEMA YA KISTO. Ni kupitia mafundisho tu unaweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa usahihi na inategemeana na mafundisho gani unapata...kama ni mafundisho potofu utapata mapepo…

Yohana 6:63

Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; ‘maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.’  Kabla hujaanza kuona matokeo mwilini lazima matokeo yaanze rohoni. Roho Mtakatifu lazima aanze kukubadilisha wewe binafsi ndiyo maisha yako ya nje yaanze kubadilika.  Tatizo watu wengi wanafundishwa kuwa Mungu anataka afanikishe biashara yako...akupe kazi...akupe ndoa..Watoto...mambo yote ya mwilini pasipo kubadilishwa namna ya mienendo yako...tabia zako.... Mambo yako ya mwilini hayawezi kubadilika mpaka Roho Mtakatifu atengeneze tabia yako kwanza na ufahamu wako. Usipo pokea matunda ya rohoni kwanza usitegemee kuvuna matunda ya mwilini.  

Waefeso 5:9

kwa kuwa tunda la roho ni ‘katika wema wote na haki na kweli;’ 

Wagalatia 5:22-24

[22] ‘Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,’  (23) ‘Upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.’  [24] ‘Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.’ 

7/23/19, 17:49 - Prophet:  Nilisema hapo juu kuwa, ahadi za Mungu katika maisha yetu ni UZIMA! Uzima katika kila maeneo ya maisha yetu...ila uzima huu ili udhihirike tunatakiwa kumtii roho mtakatifu...lakini watu wengi wanachanganya kuelewa utofauti kati ya mali na baraka za Mungu... Uzima ndiyo baraka zenyewe zinazozungumzwa kwenye biblia; ila baraka za Mungu siyo mali..bali mali ni matokeo ya hizo baraka za Mungu...kwa sababu baraka ni uwezo unaopewa kutoka kwa Mungu...lakini baraka hizi Mungu alishatupa...ila kuna kanuni ya namna ya kurithi hizo baraka. 

7/23/19, 17:51 - Prophet:  Nitakachokieleza hapa ni msingi wa kupokea baraka za rohoni ambazo ndiyo msingi; zinazosababisha turithi, tupokee na tutunze baraka za mwilini. Kilichomfanya Yesu aje kingine ni kutuunganisha na baraka alizobarikiwa pia Ibrahim. Na namna ya kupokea hizo baraka ni kwa njia ya ‘KUAMINI’ tu. 

7/23/19, 17:54 - +255 785 918 6**: Amen. 

7/23/19, 17:58 - Prophet:  Wagalatia 3:6-7,9

  1. ‘Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.’
  2. ‘Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndiyo Wana wa Ibrahimu.’

[9] ‘Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.’

Lakini uwezesho huu unakuja tu kwa kumpokea Roho Mtakatifu, yaani Mafundisho ya Neema na Kweli.

Wagalatia 3:14

‘ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.’

Waefeso 1:3

Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ‘aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; …’  Tulisha barikiwa kwa kumwamini Kristo, hatutoi ili tubarikiwe! Hizi baraka ni baraka za rohoni. Kuna baraka za mwilini ambazo pia tunapata kwa kumtii Roho Mtakatifu...baraka hizi tunapata kama THAWABU / REWARDS kwa upendo wetu kwa Mungu.  Kumbuka ni UTII unaodhihirishwa kwa UPENDO kwa sababu IMANI yako inakuwa ACTIVE kwa kutenda matendo ya UPENDO.

Galatians 5:6

Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, ‘bali imani itendayo kazi kwa upendo.’ 

Waefeso 3:17

‘Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;’ Hapa ndiyo nitazungumzia suala la UTOAJI. Wakristo hatutoi ili tubarikiwe maana tulisha barikiwa. Tunatoa kwa sababu ‘tunampenda Baba yetu wa Mbinguni.’

7/23/19, 18:22 - Prophet:  Hakikisha nia yako inayokusukuma utoe si ili ubarikiwe au ujibiwe maombi bali kwa sababu unampenda Mungu. Utoaji wa aina hii ndiyo unaoleta matokeo.  Kwa hiyo, tunamtoleaje Mungu sasa?  Ndiyo swali kuu. 

7/23/19, 18:27 - Prophet:  Kwanza kabisa, utoaji wetu Wakristo ni wa hiari na siyo kulazimishwa!

2 wakorinto 9:7-8

  1. ‘Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.’
  2. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; …Ukikutana na mafundisho yoyote yanayokueleza kutoa kwa lazima, yakimbie hayo mafundisho haraka sana, maana, yatakuingizia roho ya ukata!

7/23/19, 18:33 - +255 713 626 4**: Unafundisha vizuri sanaaa!

7/23/19, 18:39 - Prophet:   Mafundisho ya aina yoyote yanayokuelekeza utoe ili Mungu akubariki, akulinde wewe na kazi zako, biashara yako, familia yako; kuwa utoe ili ujikomboe kutoka kwenye laana za familia na za ushirikina ni mafundisho potofu yanayoleta faida kwa wanaofundisha na siyo kwa wanaofundishwa! 

2 Peter 2:1-3

  1. ‘Lakini kuliondokea Manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako Waalimu wa uongo watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.’
  2. ‘Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.’ [3] ‘Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.’ 

Wakolosai 2:8, 22-23

[8] ‘Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.’  [22](Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); ‘hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu!’  [23] ‘Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.’ 

7/23/19, 18:44 - Prophet:  Sasa kunakitu nataka nikizungumzie kabla sijagusia utoaji! Kwa sababu ya changamoto ya mafundisho hasa katika eneo la utoaji kuna mambo nitayagusia ambayo yanaweza kuonekana mapya ila ndiyo ukweli halisi wa Wakristo. Jambo la kwanza ni kuhusiana na MADHABAHU na SADAKA! Nifuatilieni kwa umakini sana mpate ufahamu. Katika Agano Jipya hatutoi sadaka. Tunatoa MATOLEO.  Tunachokitoa hakiitwi sadaka; kinakitwa MATOLEO. Katika Agano Jipya ni sadaka moja tu inayonena Mbele za Mungu, nayo ni DAMU YA YESU tu! Hakuna kitu utakachoweza toa kitakachoweza nena mbele za Mungu kikakuhesabia haki, hakuna, ni DAMU TU YA YESU basi!

Wakolosai 1:20

‘…na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.’ Na kwa sababu hii hakuna madhabahu yoyote inayoweza kuinuliwa duniani utakayo toa sadaka yako hapo Mungu aikubali kwa sababu ukurasa huo ulifungwa kupitia SADAKA YA DAMU YA YESU.

Ukiweka madhabahu, ukatoa sadaka hapo, watakao pokea hiyo sadaka ni mapepo siyo Mungu. Na ili sadaka ikubaliwe, lazima awepo kuhani. Kuhani aliyechaguliwa na Mungu ndiyo aiwasilishe hiyo sadaka na Yesu peke yake ndiye Kuhani Mkuu mbele za Mungu. Hakuna mtu mwingine anayeweza kusimama hapa duniani akajiita kuhani ili utoe sadaka kwake Mungu aikubali na ajibu.

Waebranja 9:11-12, 25

  1. ‘Lakini Kristo akiisha kuja, aliye Kuhani Mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa madhabahu iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,’
  2. ‘wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.’

[25] ‘wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile Muhani Mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake…’

7/23/19, 19:06 – Prophet:  Baada ya kuliweka hilo sawa nimalizie sasa kuhusu NAMNA YA UTOAJI WETU KAMA WAKRISTO. Hatutoi kwa lazima na fundisho kuu lililo ingia linalofanya watu watoe kwa lazima ni FUNGU LA KUMI. Nataka niishie hapa kwa kueleza NAMNA YA KUMTOLEA MUNGU FUNGU LA KUMI:

Niseme hivi, Fungu la Kumi ni kanuni ya kuweka akiba ambayo Mungu aliiweka ili tuweze kujikimu kimaisha na tupate kumtii. Katika kumtii huko, kazi zetu za mikono zibarikiwe.  Ni kanuni sio Sheria.

Kumbukumbu 14:22-23

  1. ‘Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.’
  2. ‘Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako,’ mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima.

Mungu aliagiza watu wake wahifadhi asilimia kumi ya kila kipato wanachopata kutoka kwenye kazi ya mikono yao na baada ya muda waile na kufurahi ili wapate kuona faida ya kumtii Mungu.

Kumbukumbu 14:28-29

  1. ‘Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;’
  2. na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ‘ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.’

Katika asilimia kumi ya akiba uliyohifadhi baada ya kuona imekuletea faida toa kwa ajili ya watumishi, yatima, wajane, wasiojiweza ili kazi yako ya mikono ibarikiwe. Na kumbuka, siyo kwamba hujabarikiwa, hapana, ni kwamba, baraka ulizonazo rohoni zinaanza kufanya kazi ukimtii Mungu kwa upendo.

Kwa hiyo, ukitaka uone faida ya kumtii Mungu katika maisha yako kifedha, jifunze kuweka AKIBA na hautapungukiwa!  Kutokea kwenye akiba yako toa kwa upendo si kwa lazima, si kwa kutafuta baraka na utaona baraka zikidhihirika katika maisha yako. Namna ya pili ya kutoa ili uone baraka zikidhihirika katika maisha yako kama Mkristo ni kutoa matoleo kutoka kwenye faida iliyorudisha tayari mahitaji yako...uwe unafanya kazi au biashara...

Mathayo 25:14-27

  1. ‘Maana Ufalme wa Mbinguni ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake’
  2. ‘Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.’
  3. ‘Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.’
  1. ‘Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambuwa ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;’
  2. Basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

[27] ‘Basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.’

7/23/19, 19:49 - Prophet:  Hapa Yesu alikuwa anatowa mfano kuhusu Ufalme wa Mungu unavyofananishwa na mfano huu unaelezea jinsi ambavyo Mungu anatuwezesha au anatupa uwezo kufanya vitu vitakavyo saidia kutufanya tuishi lakini katika hayo aliyotupa kama kazi ya mikono kuna sehemu ya kumrudishia. Lakini jinsi yakumrudishia Mungu ndiyo itaamua kuwa tutabarikiwa au hapana.

Mathayo 25:26-27

  1. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijuwa ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
  2. ‘basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida ubaki nayo.’   Na tunachokirudisha ni sehemu ya faida ambayo imeshatufaidisha sisi kwanza; yaani kama unafanya biashara, usitoe matoleo kutoka katika mtaji kabla ya kutengeneza faida.

Na kama unalipwa mshahara usiseme unatoa matoleo wakati unamadeni hujalipa, hujamalizia mahitaji yako na unatoa, hapana, usifanye hivyo.  Ukifanya hivyo, utoaji

wako utakuwa hauna matokeo...utalalamika kuwa unatoa ila huoni kitu… Kwa hiyo, ukitoa kwa utoaji wa aina hii hutapungukiwa!

7/23/19, 20:07 - Prophet:   Nitaendelea kesho na  somo…                                                   

7/23/19, 20:37 - +255 654 333 5**: Barikiwa sanaaa Mtumishi somo limeingia barabara…

7/24/19, 00:13 - +255 719 513 9**: Asante sana prophet somo zuri sana. Nimebarikiwa

7/24/19, 07:04 - +255 785 918 6**: Asante sana mtumishi kwa neno zuri

7/24/19, 11:08 - +255 654 333 5**: Shalom watu wa Mungu. Mimi nina swali. Huwa tunafundishwa katika maombi kumkumbusha Mungu juu ya ahadi zake kwetu au mahitaji yetu au kuombea taifa kwa ujumla. Sasa ikiwa  siyo kwamba Mungu atujuwa mahitaji yetu na Mungu anatujuwa tunayowaza, kwa nini tunaombea haya maombi?

7/24/19, 11:11 - Prophet:   Mathayo 6:7-8 [7] ‘Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.’ [8]Basi msifanane na hao; ‘maana Baba yenu anajuwa mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.’ 

Kama anajuwa kwa nini umkumbushe?

Luka 12:30-31

  1. ‘kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajuwa ya kuwa mna haja na hayo.’
  2. ‘Bali utafuteni Ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.’

7/24/19, 11:36 - +255 654 333 5**: Amina. Sasa tumeaswa tufanye maombi haya,  je ni sahihi?

7/24/19, 11:36 - +255 654 333 5**: Leo ni siku yetu ya Maombi:  

Tukizingatia maendeleo ya nchi zetu za Afrika. Napenda tumkumbushe Mungu leo (na liwe ombi letu la kila siku kwake:  

1)  

    • Atuondolee vita vya kikabila,
    • atuondolee ujinga
    • atuondolee hofu na woga
    • Atuondolee usingizi na uvivu
    • atuondolee manabii na watumishi wa uongo
    • atuondolee wachawi na Kulogana na kuamini Miujiza kama sehemu yetu
    • atuondolee ubinafsi na umimi, uchoyo , umbea usengenyaji, ufisadi na Rushwa.  
    • atuondolee roho za Kujipendelea na kupenda madaraka kuliko maendeleo
    • atuondolee kujidharau na kujiona hatuwezi
    • Atuondolee pepo la mapenzi na zinaa, ulevi, mauaji
    • Atuondolee kupenda Fedha

2)

    • Atupe kuwaona wengine kuwa bora pia
    • Atupe Upendo na uthamani kwa nchi zetu
    • atupe maarifa na bidii kubwa ya kusoma, kujifunza, kufanya kazi na kutokata tamaa,Ubunifu na kujiamini
    • atupe umoja na uzalendo
    • Atuumbie Moyo safi na uliopondeka
    • Atupe bidii sana katika maarifa na katika Neno lake na si miujiza.
    • -Atusaidie kumpinga shetani na kumshinda tusivutwe na dunia.

Isaya 62:6-7, Yer 29:11

(Mtu wa Mungu, hata kama hujawahi kabisa kuomba na hujui kuomba, naomba maombi haya utembee nayo). Tafuta mistari mingine ukiweza ila haya tumwombe Bwana akumbuke.. 

7/24/19, 11:49 – Prophet: Ndio yanaonekana ni mambo mazuri ila tukirudi kwenye maandiko neno linasemaje...Yesu amesema usirudie rudie maneno...usipayuke ukidhani

ndio Mungu atasikia...kwa sababu Mungu anajua mahitaji yetu Kwahiyo kuomba sio kumpa Mungu taarifa afanye mambo fulani hapana Ni kukiri ahadi zake kupitia neno....ndio Yesu akatupa muongozo wa kuomba.

7/24/19, 11:58 - +255 654 333 5**: Ndio maana tunatakiwa Roho Mtakatifu atuongoze katika kuomba…bila Roho Mtakatifu tutakuwa tunapayuka payuka. Wengi wetu huomba tu bila mpangilio maana hatuongozwi na roho bali tunatumia akili zetu wenyewe…

7/24/19, 12:03 -Prophet:   Yesu alitupa mwongozo wa mtazamo wetu katika kusali

Mathayo 6:9-13

  1. ‘Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,’
  2. ‘Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.’
  3. Utupe leo riziki yetu.’
  4. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.’ [13] ‘Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]’

Hii sala siyo kwamba unaitamka kama ilivyo hapana. Ni mwongozo wa mtazamo wako katika kuomba. ‘Cha kwanza, ujuwe kuwa, unaomba kwa Baba yako wa Mbinguni. Hapa ndio unatakiwa kumshukuru na kutukuza jina lake kwa maneno ya kinywa chako.’  Yesu alitupa mwongozo wa mtazamo wetu katika kusali.

Mathayo 6:9-13

  1. ‘Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,’
  2. ‘Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.’ [11] ‘Utupe leo riziki yetu.’ 

7/24/19, 12:08 - +255 719 513 9**: Amen!

7/24/19, 12:10 - Prophet:   Hiki kipengele cha hadi kufikia kuomba kupewa riziki ni kwamba unatakiwa uwe na haki mbele za Mungu na haki hiyo kupitia mapenzi yake ndiyo utapata mahitaji yako...kwa sababu neno lina sema hivi: Kuwa tukisogelee kiti cha enzi cha Mungu kwa ujasiri tupate neema wakati wa mahitaji yetu.

Waebrania 4:16

‘Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.’Huwezi kuwa na ujasiri mbele za Mungu kama hauna haki mbele zake hiyo haki ndio inakupa ruhusa ya kupokea neema wakati wa mahitaji yake...ndio maana esu anasema "utupe riziki zetu za leo" sasa huu ni mtazamo sio maneno ya kutamka.  Kwa hiyo, biblia ikisema utafute Ufalme wa Mungu na haki yake, yaani, inamaanisha unatakiwa uamini kuwa unahaki mbele za Mungu ukiamini hivyo kuna neema itakuwa inafanya kazi pamoja na wewe wakati wa mahitaji yako. Hicho ndicho kinachomaanishwa hapa kuwa ‘Ufalme wako uje!’

7/24/19, 12:13 - +255 654 333 5**: Amina...Kwa hiyo sasa... 

7/24/19, 12:15 - Prophet:   Kwa hiyo maneno yanayotakiwa kutoka kinywani mwako ni kumshukuru Mungu na kuomba kupitia Roho wa Mungu, uongozwe katika mapenzi yake, hapo ndiyo utapata neema ya kukusaidia katika mahitaji yako...ndiyo maana ya kusema, ‘mapenzi yako yatimizwe na utupe riziki zetu za leo.’ 

7/24/19, 12:15 - +255 654 333 5**: Hapo ndiyo nakuja elewa kwa nini Yesu alifundisha jinsi ya kuomba…Lakini kwa nini leo hii kuna aina ya maombi mengi ambayo ukiyatafakari yapo nje ya Bwana alivyofundisha?

7/24/19, 12:18 - Prophet:   Wafilipi 4:6-7

  1. ‘Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.’
  2. ‘Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.  

Yaani, huhitaji kujisumbuwa kuomba maombi ya kupambana sijui ya kumkumbusha Mungu kwa sababu anajuwa unachohitaji.  Mahitaji yako yapo katika kumshukuru na kuachilia mapenzi yake yatimie. Hayo maombi mengine yote ni kujichosha… Na changamoto kubwa ipo katika kuomba maombi ya kupambana. Hapo ndio kuna changamoto kubwa.  Ngoja nieleze hili mpate ufahamu jinsi Yesu alivyotufundisha kusali.

7/24/19, 12:19 - +255 686 361 1**: Mungu tusaidie, maana kutoa mapokeo kichwani na kuingiza ukweli tunahitaji roho azidi kutuongoza jamani. Prophe,t twende tararibu mpaka tutaelewa.

7/24/19, 12:21 - +255 654 333 5**: Juzi nilikuwa nikiangalia channel fulani ya dini. Watumishi wake walikuwa wakitowa mapepo waumini waliokuwa nayo. Sasa Mchungaji Mkuu wa hiyo madhabahu hakuwepo siku hiyo. Hivyo watumishi wake wakawa wanaombea kwa kusema, "Nakutoa pepo kwa jina la Mungu wa madhabahu hii ya baba yetu Mr. so and so…" na kweli waliodondoka wakapagawa mapepo na kufunguliwa. Sasa nakumbuka Bwana Yesu alifundisha wanafunzi wake kutoa mapepo kupitia jina la Yesu.’na kwa Jina langu mtatoa mapepo na mtu hawezi kufika kwa Baba yangu isipokuwa kupitia Kwangu.’ Hizo ni baadhi tu ya nukuu za neno la mungu. Sasa, hao watoao mapepo kwa majina ya miungu mingine wanatoa wapi hayo?

7/24/19, 12:24 - Prophet:   Kingine katika kuomba hakikisha hauna kinyongo na mtu na vile vile hakikisha huna nia yoyote ya kibinafsi; kwa sababu, biblia inaposema, ‘usituongoze katika majaribu’ haimaanishi Mungu anakujaribu; inamaanisha, Mungu atakuruhusu ujiingize kwenye majaribu kutokana na tamaa zako binafsi.

Yakobo 1:13-14

  1. ‘Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.’
  2. ‘Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.’

Kwa hiyo, unatakiwa kabla ya kusali uwe na moyo ambao hauna kinyongo na usio na ubinafsi.

Hapo ndipo nguvu za giza zitashindwa kukujaribu. Ukianza kusali maombi ya kukemea mapepo, sana sana utazidi kupata mashambulizi mengi kwa sababu unayaita mwenyewe. Mahali ambapo Wakristo tumeambiwa tukemee mapepo ni kwa waliopagawa na mapepo tu. Hii changamoto ngoja niielezeee kwa upana ili mpate picha kamili… 

Hili nililigusia jana kuhusiana na MADHABAHU na SADAKA. Ipo hivi: Nasema kwa uwazi, mjuwe kwa sababu ninachokisimamia ni neno la Mungu na mapokeo ya Mitume wa Yesu, siyo mtumishi fulani.

7/24/19, 12:31 - +255 719 513 9**: Sawasawa mtumishi! 

7/24/19, 12:32 - Prophet:  Kwanza, tunaomba kupitia jina la Yesu na tunatoa mapepo na kusaidia watu kwa jina la Yesu tu. Ukiona pepo linatoka kwa kutamka jina au madhabahu ya mtu Fulani, ujuwe kuna mchezo unafanyika....mchezo upi? Wa udanganyifu.... Ipo hivi, pepo siyo kwamba yanatoka hapo, yanapungwa!

7/24/19, 12:34 - +255 785 918 6**: Amen! 

7/24/19, 12:34 - Prophet:   Au yananyamazishwa na ukitaka kuamini ninachokisema, huyo mtu aliyeombewa hapo ataendelea kulipuka mapepo bado kwa sababu, pepo halitoki kwa kukemewa, linatoka kwa kuambiwa ukweli.Yanakuwa yanaaambiwa yatoke kwa muda halafu yarudi baadae.

7/24/19, 12:35 - +255 785 918 6**: Kwa kweli!

7/24/19, 12:36 - Prophet:  Ndiyo maana Yesu alisema, pepo likimtoka mtu linatafuta kurudi. Ndyio maana siwezi kumwombea mtu mwenye mapepo nikaishia hapo, lazima nimfundishe kweli ya neno la Mungu ili hayo mapepo yasirudi tena.

Mathayo 12:43-45

[43]Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

[44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

[45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya. 

Kwa sababu hikii kitu nasema hapa hata wapunga pepo wanafanya na ukiangalia unaweza dhani yule mtu mapepo yamemtoka…hatawenzetu wa upande wa pili siku hizi wanatoa mapepo kwa staili hii hii… 

7/24/19, 12:43 - +255 719 513 9**: Uwiii … Mungu tusaidie!

7/24/19, 12:43 - Prophet:   Mapepo yanatolewa kwa jina la Yesu na ili mtu awe huru anatakiwa afundishwe neno la Mungu.  Ukiona mapepo yanatolewa kwa jina la mtumishi fulani ujuwe hapo pepo halijatoka limetulizwa na hayo ni mazingaombwe ili kuonyesha watu kuwa huyo mtumishi anaupako sana na wapo mahali sahihi.

Kwa hiyo, matokeo yake ili hao watu wasifuatiliwe na hayo mapepo wataambiwa wawe wanatumia vitu kama vitambaa...mafuta… maji...sticker … alizoziombea huyo mtumishi au zenye picha ya huyo mtumishi. Na watu wanaofanya hivi wataanza kuona sura ya huyo mtumishi ikiwatokea kwenye ndoto na kuanza kuwalinda na sio kwamba huyo ni  Roho Mtakatifu anawalinda hapana, ni maroho ya kutokea baharini yanachezea watu akili na kuwatokea kwa sura ya huyo mtumishi ili kuwaonyesha ana upako sana msiondoke…

7/24/19, 13:53 - Prophet:    added +255 742 022 3** and +255 789 746 0**

7/24/19, 13:55 - Prophet:    added +255 754 650 6**

7/24/19, 12:48 -   Prophet:  Ndiyo maana lazima uombe kwa jina la Mungu wake na lazima utaje madhabahu yake na unapo anza kufanya hivyo unaji - disconnect na Roho Mtakatifu; unajiunganisha na miungu mingine.  Sasa, ambavyo ili iendelee kukulinda lazima u-renew mkataba nao kwa sadaka unazotoa kwenye madhabahu ya huyo mtumishi na huyo mtumishi ndiyo kuhani wa hiyo madhabahu.  Hivyo, lazima awe anakuombea ili uendelee kulindwa… Ukisema unajaribu kuhama hapo lazina utapata mashambulizi yasiyo ya kawaida ya kiroho, sababu unavunja agano lako na huyo kuhani.  Haya yote ni operation za kipepo, ndiyo maana kwenye madhabahu za aina hiyo wachawi lazima waonekane sana sababu wapo kwenye ufalme mmoja…

7/24/19, 12:51 - +255 713 626 4**: Aiseee, sema tupone mtumishi wa Mungu!

7/24/19, 12:52 - Prophet:  Na kwenye madhabahu kama hizo, lazima mfundishwe masuala ya laana za ukoo...mizimu...wachawi...lazima usikie maombi ya kuuwa wachawi kwa sana…

7/24/19, 12:52 - +255 719 513 9**: Tufungue macho my prophet…

7/24/19, 12:52 - Prophet:  Na lazima usikie mafundisho ya kutumia chumvi...mafuta...udongo...maji yaliyo ombewa na huyo mtumishi ili yakulinde na mashumbulizi ya kichawi…

7/24/19, 12:52 - +255 713 626 4**: Kwa kweli tufunguwe macho!

7/24/19, 12:54 - Prophet:   Na usipotoa shuhuda kumtukuza mungu wa hiyo madhabahu utapoteza muujiza wako...kama ni ugonjwa uliondoka utarudi…kama ni kazi utaachishwa …kama ni biashara itaporomoka tu!

7/24/19, 12:57 - Prophet:  Na ukitaka uchukiwe wewe abudu kwa mtumishi mwingine … Lazima tu utasikia huyo mtumishi akisema kuwa, lazima ukawe chini ya upako wake...kifuniko chake ili Mungu atende kwenye maisha yako...kwa ufupi yeye ndiyo mwenye Mungu, wewe huna!  

7/24/19, 14:26 - Prophet:   added +255 659 287 3**

7/24/19, 12:58 - Prophet:   Sasa, haya mambo yote yanatendeka kwenye huduma zenye mifumo ya namna hiyo ya kuomba kupitia jina la mtumishi fulani na siyo jina la Yesu.

7/24/19, 12:58 - +255 713 626 4**: Kwa kweli hapo utuombee sana mtumishi. 

7/24/19, 12:59 - Prophet:  Yesu hakuwa na madhabahu yoyote wala Mitume wake hawakuwa na mdhabahu zozote. Na watumishi wa hivi wote wanaanguka katika sehemu moja ya "BABA WA KIROHO." Nikuambie tu, ukweli uliowazi hakuna BABA WA KIROHO isipokua Mungu wetu wa mbinguni. Yesu alishaukataa huo mfumo...kwa sababu mtu ANAYEJIITA BABA WA KIROHO anataka akutawale, akufanye mateka wake.

Mathayo 23:9-12

  1. ‘Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.’
  2. ‘Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.’
  3. ‘Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.’
  4. ‘Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.’

7/24/19, 13:04 - +255 713 626 4**: Asante!

7/24/19, 13:10 - Prophet:  Kufanywa mateka wake ni kwamba anataka umnyenyekee zaidi kuliko kumnyenyekea Mungu na kumsikiliza Mungu.

Wakolosai 2:8, 18

[8] ‘Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.’ [18] ‘Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;’

Yaani, hawa watumishi wanaojiita mababa wa kiroho, wanajiita hivyo ili waonekane watu ‘special’ wenye maono tofauti, upako tofauti na neema tofauti inayoweza kukusaidia kuondoa matatizo yako.  Pia wanataka waonekane wao ndiyo wakisema, Mungu kasema.  Kwa hiyo, waogopwe, wanyenyekewe...

Watumishi wa hivi mara nyingi utawasikia wakikuambia malaika wa madhabahu hii au malaika wangu watakuja ukimwita Mungu wangu au ukijungamanisha na madhabahu yangu...sasa juwa kabisa hao sio malaika anaowasema ni mapepo. Kwa sababu hizo, chochote utakachofanya kwa muundo wa ibada ili kujiungamanisha na hao malaika wake ni kwamba, unajiungamanisha na ibada za miungu za kuabudu malaika ndicho Mtume Paulo kasema hapo.

7/24/19, 13:24 - +255 713 626 4**: Sisi mtumishi tufanye maombi yapi ili kujitenganisha na madhabahu hizo ambazo kwa kweli tulikuwa hatujuwi kabisa na tumetumika huko?.

7/24/19, 13:24 - Laura: …hapa tumefeli wengiiii…yaaani, tunama papaaaaa wakutoshaaa!

7/24/19, 13:26 - +255 719 513 9**: Yaani!

7/24/19, 16:46 - Prophet:    added +255 717 930 2**

7/24/19, 13:28 - Prophet:   Unatakiwa umwamini Yesu na umkiri kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, hapo utachomoka kiroho!

7/24/19, 13:29 - +255 713 626 4**: Ok Mm namwamini Mungu aliyejuu mbinguni…

7/24/19, 13:29 - Prophet:   Rudisha imani yako kwa Yesu na neno la Mungu sio wanadamu.

7/24/19, 13:35 - Laura: Ooook,asante kwa mwongozooo…

7/24/19, 13:55 - +255 654 333 5**: Nabarikiwa sana kuijuwa kweli ya Mungu siku hadi siku..

7/24/19, 14:01 - +255 764 252 5**: Fanya maombi huku umetoka kwenye hizo madhabahu....maana, ukiomba huku uko hapo hapo kwa Papaa, itakuwa ngumu kuchomoka!

7/24/19, 14:01 - +255 764 252 5**: Leo mada tamu!

7/24/19, 14:03 - +255 764 252 5**: Leo umetema madini mtumishi Joa…

7/24/19, 14:03 - Prophet:  Haya madini kuyajuwa ni mpaka Mungu akupitishe mahali fulani! Halafu akutoe! Nimepita na kusulubishwa kichwa chini miguu juu...

7/24/19, 14:04 - +255 764 252 5**: Kweli…

7/24/19, 14:15 - +255 654 333 5**: Kweli haya madini ya leo sio ya dunia hii… 7/24/19, 14:17 - +255 654 333 5**: Maana yake nilikuwa natatizwa sana na hizo madhabahu zinazotumia hayo maneno.. .’Nashukuru Mungu wa madhabahu hii ameniponya!’ Sasa nahisi hata hao wanaotoa ushuhuda wanaambiwa jinsi ya kusema...kwa nini asiseme ‘namshukuru Mungu wa Mbinguni au Yesu?’

7/24/19, 14:21 - +255 686 361 1**: Daaaah, mimi naomba haya mafundisho yarudiwe kila mara mpaka yakae kichwani na moyoni. Jamani Mimi naona mambo mengi sana mpaka nahisi kuchanganyikiwa!

7/24/19, 14:22 - +255 686 361 1**: Prophet nivumilie, nitauliza maswali. Acha nisome tena na tena…

7/24/19, 14:23 - Prophet:  Usijali hiki siyo somo la kuelewa siku moja. Ni mchakato wa kuendelea kukaa kwenye neno hadi kitu kipya kijengeke ndani yako.

7/24/19, 14:27 - Prophet:   Unajuwa ilibidi niyapitie hayo ili niweze kukaa sasa niwafundishe watu ukweli ni upi. Ni kwamba, hata mimi nilikuwa naamini hivyo vitu hapo zamani, ila neema ya Mungu ikanitoa huko.

7/24/19, 14:30 - +255 686 361 1**: Mtumishi, naomba unieleweshe vitu hivi neema, rehema…

7/24/19, 14:30 - +255 686 361 1**: Tuanze hapo… 7/24/19, 14:32 - Prophet:   Neema na rehema....

Sawa, ingawa havipo kwenye ratiba ya mafundisho, nitaweka, nitafundisha 

7/24/19, 14:38 - +255 764 252 5**: Yeah…

7/24/19, 14:38 - +255 764 252 5**: Kweli Ni neema tu!

7/24/19, 14:47 - +255 654 333 5**: Mimi ningependa mafundisho haya tungeweza ku

- print mfano kwenye PDF ni valuable sana haya…

7/24/19, 15:04 - +255 686 361 1**: Sana aisee, tuyasome Kwa utaratibu mpaka tuelewe tujue haki zetu zoote.

7/24/19, 15:06 - Prophet:   Yes nitayapanga kwa mfumo huo rasmi. Okee, ukisema neema na rehema unamaanisha kwa upande gani?

7/24/19, 15:32 - +255 686 361 1**: Mfano wanaposema ‘by the grace of…’

7/24/19, 15:33 - Prophet:  Mtumishi fulani…

7/24/19, 15:33 - +255 686 361 1**: Yes…

7/24/19, 15:33 - +255 686 361 1**: It means Sisi hatuna grace?

7/24/19, 15:34 - +255 686 361 186: Yan inasikitisha sana , wametutoa kwenye line siku nyingiiii wakatutumia jamani!

7/24/19, 15:35 - Prophet:  Okeee, grace ni kitu gani labda nianzie hapo ili muweze kuelewa -GRACE ni nini?

7/24/19, 15:35 - +255 686 361 1**: Yaani Acha tuu…

7/24/19, 15:36 - +255 686 361 1**: Kwa kifupi tu, hili kama somo, utafundisha kwa urefu…

7/24/19, 15:37 - +255 686 361 1**: Nakuombea Kwa Mungu usije badilika, usije badilishwa, usimamie ukweli jamani utaokoa wengi…

7/24/19, 15:38 - Prophet:    Grace / neema ni upendeleo unaopata kutoka kwa Mungu lakini unayostahili kwa sababu ya alichokifanya Yesu msalabani ni zaidi hata ya rehema. Hakuna mtu mwenye grace / neema ya kipekee au tofauti na wengine.  Grace / neema tunayoipata; tunaipata kupitia DAMU YA YESU tu. Grace / neema ni ZAWADI YA MUNGU tunayotakiwa kuipokea.’

7/24/19, 15:40 - +255 686 361 1**: Sawa!

7/24/19, 15:41 - +255 686 361 1**: Mercy Kwa ufupi.

7/24/19, 15:41 - Prophet:    Yohana 1:17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; ‘neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.’  Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kusema ana neema ya tofauti au ya kipekee kuliko wewe na mimi. Yohana 1:14, 16 [14] Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; ‘nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.’ [16]Kwa kuwa katika utimilifu wake ‘sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.’ Mercy / Rehema ni huruma za Mungu...yaani ukiomba Mungu akurehemu; unamaanisha Mungu akuhurumie.  Kwa hiyo, anaweza kuamuwa akuhurumie au asikuhurumie lakini huo mlango wa rehema ulishafungwa ukafunguliwa mlango mpya wa neema...unachotakiwa kufanya nikuipokea neema ya Yesu tena ni ya Yesu sio ya mtumishi yeyote kwa sababu hakuna mwanadamu mwenye neema yoyote ya kukusaidia.

Acts 15:11

[11] ‘Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu’ vile vile kama wao. 7/24/19, 16:20 - +255 686 361 1**: Sasa ukisema mlango ulifungwa unamaanisha ni kipindi cha Agano la Kale?

7/24/19, 16:21 - Prophet:   Ndiyo. Agano la Kale ndiyo watu walikuwa wanaishi kwa rehema za Mungu.

7/24/19, 16:22 - +255 686 361 1**: Nieleweshe tena, kwa hiyo, hatutakiwi kulitumia hilo Agano la Kale? Kwa maisha ya sasa? Au ni kipindi gani tunatakiwa tulitumie Agano la Kale?

7/24/19, 16:26 - Prophet:  Agano la Kale liliondolewa na ujio wa Yesu, ndiyo maana sasa hivi ni kipindi cha AGANO JIPYA.

Yeremia 31:31-34

  1. Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ‘nitakapofanya agano jipya na nyumba ya

Israeli, na nyumba ya Yuda.’ Agano Jipya

  1. ‘Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.’

[33]’*Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.’  [34] ‘Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.’

7/24/19, 16:30 - +255 686 361 1**: Asante, nitazidi kuelewa tu!

7/24/19, 16:37 - +255 713 626 4**: Sawa.

7/24/19, 18:08 - +255 654 333 5**: Dah...kweli haya yalinipita...

7/24/19, 18:22 - +255 658 999 6**: 👆kuhusu wababa wakirohooo…

7/24/19, 18:23 - +255 658 999 6**: Asante sana mtumishi!

7/24/19, 18:28 - +255 654 333 5**: Kwenye maandiko yanasema Bwana Yesu alisema "Sikuja kuitengua torati bali kuitimiliza” Hapo alimaanisha nini?

7/24/19, 19:46 - Prophet:   Okeee…Niseme, labda hilo neno linatumiwa ila changamoto ni lugha au aina ya maneno yaliotumika.

Kutimiza kitu ni kukifikisha kwenye ukomo wake ...kwa hiyo, alichokuwa anamaanisha Yesu ni kuwa, hakuja kuivunja torati / sheria bali alikuja ili ifike kikomo watu waache kuitegemea ili wahesabiwe haki / wakubaliwe kwa Mungu.

7/24/19, 21:04 - +255 654 333 5**: Dah...Mimi mwenyewe nilidhani amekuja kuitimiza...yaani kuikamilisha au kuiidhinisha…

7/24/19, 21:25 - +255 742 022 3**: Sasa mtumishi...kwa nini kuna msemo wa mtu kusema anatembelea neema ya mtu flani.... Mungu huruhusu watu kupata lift ya neema ya mtu mwingine au ni nini hasa?

7/24/19, 21:31 - Prophet:    Neema kama neema inafanya kazi kwa mtu yeyote atakaye amini jina la Yesu.

7/24/19, 21:32 - +255 658 999 6**: mtumishi samahani.kama Agano la Kale liliondolewa na ujio wa Yesu. Mbona fungu la kumi lakazaniwa na liko kwenye Agano la Kale?

7/24/19, 21:43 - Prophet:   Ahaaa! Utoaji wa zaka kwa sasa utatoa kama sehemu ya kuonyesha upendo kwa Mungu si kwa lazima. Ila ukifundishwa utoaji ki usahihi utatoa. Tatizo ni pale nikikutisha na kuanza kukuambia usipotoa utapata matatizo au unamwibia Mungu au hautabarikiwa. Hapo nitakuwa nakudanganya. Niseme hivi, fungu la kumi ni kanuni ya kuweka akiba ambayo Mungu aliiweka ili tuweze kujikimu kimaisha na tupate kumtii na katika kumtii huko kazi zetu za mikono zibarikiwe.

7/24/19, 21:49 - +255 686 361 1**: Torati ni Sheria?

7/24/19, 21:50 - Prophet:  Hapana, torati sio sheria ila ndani ya torati kuna sheria na maagizo.

7/24/19, 21:51 - +255 686 361 1**: So wakati wa Mussa kulikuwa na sheria na maagizo alipokuja Yesu tukapata neema… 7/24/19, 21:52 - Prophet: Ndiyo 

Kumbukumbu 14:22-23

  1. ‘Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.’
  2. ‘Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako,’ mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. Hili ni agizo la zaka ambalo Mungu aliagiza kwenye torati katika kitabu cha kumbukumbu. Na zaka hiyo iliyoagizwa ni zaka inayoliwa.

Kumbukumbu 14:28-29

  1. ‘Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;’
  2. na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ‘ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.’

7/24/19, 21:56 - Prophet:    Kwa hiyo, utoe au usitoe bado haikulazimishwa tofauti na inavyofundishwa kwenye Malaki 3:10.

7/24/19, 21:56 - +255 686 361 1**: Jamani, hawa wachungaji walichagua kutusomea maandiko yale yenye faida kwao tuuu… jamaniiii, mimi sasa nitasoma biblia mwenyewe kwa kweli!

7/24/19, 21:58 - Prophet:  Inavyofundishwa kwenye Malaki 3:10 inafundishwa kuwa watu wasipotoa zaka watalaaniwa kwa laana na wanafundisha kuwa kama ni mshahara ukiingia tu toa asilimia kumi haraka sana kabla hata hujaitumia!

7/24/19, 21:59 - Prophet:  Lakini hii Malaki 3:10 ilikuwa inazungumza na Makuhani…

Malachi 2:1

Na sasa, ‘enyi Makuhani, amri hii yawahusu ninyi.’

7/24/19, 22:00 - +255 754 650 6**: Kwa hiyo sisi haituhusu?

7/24/19, 22:00 - Prophet:   Kwa hiyo, usianze kutishwa tishwa kuwa usipotoa utalaaniwa kwa laaana na utakuwa umemwibia Mungu... Mungu hakudai kitu, yeye ni Baba yako.

7/24/19, 22:00 - Prophet:   Kabisa … haituhusu! Na kingine, sisi ni watu wa mataifa tumeipokea injili kama watu wa mataifa na siyo Wayahud.  Sasa inakuaje tunaanza kuiga mambo yasiotuhusu? 

Wagalatia 1:6-7

  1. ‘Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya

         Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.’

  1. ‘Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo  

7/24/19, 22:03 - +255 686 361 1**: Lakini hiyo… na sasa enyi Makuhani… hii yawahusu… hiyo haisomwi…ni marufuku kuisema na sababu sisi hatukuwa tunasoma neno wenyewe… tukadanganyika kiasi cha kwamba, hata tukiambiwa haya tunashangaa…

7/24/19, 22:05 - Prophet:     Yani kwa ufup,i ukianza kuitii sheria na torati unakuwa unajiloga mwenyewe na unajitoa kwenye neema.

Wagalatia 3:1,10

[1] ‘Enyi Watanzania msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?’ [10] ‘Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.’

7/24/19, 22:05 - +255 686 361 1**: Mungu tusaidie…

7/24/19, 22:07 - Prophet:    Yaani ukimtolea Mungu kwa kutii sheria unajilaani mwenyewe;  yaani uwe mbali na neema ya Mungu.

Wagalatia 5:4

[4] ‘Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.’

7/24/19, 22:07 - +255 686 361 1**: Biblia inachanganya au watumishi ndio walituchanganya?

7/24/19, 22:09 - Prophet:    Unatakiwa umtolee Mungu kwa upendo kwa furaha kwa moyo mkunjufu huko ndio kutowa kwa imani siyo kutowa kwa lazima. Kkwa hiyo, kama umeazimia kutoa asilimia ya kumi towa kwa sababu unampenda Mungu; usitoe kwa sababu usipotoa utalaaniwa au hautabarikiwa; huko ni kutoa kwa hofu.

7/24/19, 22:19 - +255 658 999 6**: Nandiko wengi tunapoambiwa hutapata ulinzi katika kazi yako.

7/25/19, 09:06 - Vesta:  Prophet umenifanya nicheke kipengele hiki aliyetuloga…

7/25/19, 09:07 - Vesta: Biblia haichanganyi watumishi ndio wanatuchanganya…

7/25/19, 09:08 - +255 654 333 5**: Ni kweli kabisa!

7/25/19, 09:09 - +255 785 918 6**: Kwa kweli!

7/25/19, 09:10 - +255 686 361 1**: Wanaigeuzageuza…

7/25/19, 09:10 - Vesta: Tena wanaigeuza haswa halafu tunafungwa ufahamu tusitafakari…

Mungu atusaidie kwa kweli.

7/25/19, 10:31 - +255 654 333 5**: Watumishi wa Mungu nina swali. Ikiwa Yesu hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza…na ikiwa majira haya hatuenendi katika sheria, je, zile amri 10 za Mungu zipo katika Agano la Kale nazo ni sharia? Nazo hatupaswi ziishi? Au kuna yanayopaswa kuyaenenda katika Agano la Kale na kuna ambayo hatupaswi kuyaenenda?

7/25/19, 10:32 - Prophet:   Swali zuri na nitajibu kama ifuatavyo:

Amri kumi za Mungu ni sheria...ila sisi kama Wakristo, hatuishi kwa kuitegemea sheria ili tuwe wakamilifu mbele za Mungu...hakuna anayeweza kuitii sheria awe mkamilifu kwa sababu hatuwezi ...sasa, zile amri kumi mtu unaweza ukazitii bila hata kuzivunja ila tatizo linakuja pale haki yetu mbele za Mungu haitokani na juhudi zetu wenyewe; inatokana na kuamini tu..., tukisema tunaacha kuamini na tunashika amri kumi ni kwamba tunajitenga na neema Mungu aliyoamuwa kutupa ambayo haihusiani na juhudi zetu binafsi...kwa hiyo, sheria ilitumika kama mwalimu kutuelekeza kwa Yesu ambaye baada ya yeye kuja hatuhitaji tena kuwa chini ya mwalimu ambaye ni sheria au amri kumi za Mungu kwa sababu sii kwa utii wetu bali ni kwa utii wa Yesu ambao tukiupokea tunafanywa kuwa wakamilifu mbele za Mungu pasipo juhudi zetu binafsi.

Warumi 5:19

[19] Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, ‘kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.’

Wagalatia 3:23-25

  1. ‘Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.’
  2. ‘Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.’ [25] ‘Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.’

7/25/19, 10:46 - +255 659 287 3**: Kwa hiyo, Agano la Kale lipo kwa ajili ya historia au … Niko serious unajuwa sielew  

7/25/19, 10:49 - Prophet:  Wafilipi 3:9

[9] ‘tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; …’

7/25/19, 10:50 - +255 659 287 3**: Hili nalo ni swali lisipuuzwe …

7/25/19, 10:50 - Prophet:    Ha-ha swali zuri, najibu kama ifuatavyo:

7/25/19, 10:50 - +255 659 287 3**: Okay!

7/25/19, 10:58 - Prophet:   Waebrania 8:13 [13]Kwa kule kusema, Agano Jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

7/25/19, 11:00 - +255 654 333 5**: Aisee! Kwa hiyo, wale wakristo wanaosema nyama hizi haziliwi hata maandiko yalisema...kwa hiyo, wao wameamua kuenzi yale yaliyofanywa katika Agano la Kale, ndiyo wanaliishi hadi sasa…

7/25/19, 11:04 - Prophet:   2 wakorinto 3: 14

[14] ‘ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la

Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;’

7/25/19, 11:06 - +255 654 333 5**: Mwaka huu kweli ndio wakati wa kujiliwa kuijuwa kweli… kumbe kila swali tujiulizalo majibu yapo ndani ya neno…

7/25/19, 12:02 - Vesta: Ee Mungu tusaidie wana wako!

7/25/19, 13:04 - +255 686 361 1**: Jamani acha tuu!

7/25/19, 18:14 – Prophet: 🔥🔥🔥🔥🔥🔥 

7/25/19, 18:17 - Prophet:  Shalom! Niliishia kufundisha kuhusu Maana ya kuwa Mkristo na nikaelezea umuhimu wa Kumpokea Roho Mtakatifu na namna ya kumpokea Roho Mtakatifu ili tuweze kurithi ahadi zetu kama wakristo...nikaelezea pia Imani inavyotumika  kutuhakikisha tunapokea ahadi zetu na namna Utoaji unahusishwa na imani kwa Upendo kuthibitisha kupokea ahadi zetu kutoka kwa Mungu’

7/25/19, 18:21 - Prophet:    Leo nataka niendelee kwenye kipengele cha ‘IMANI inayotufanya tuweze kuwa washikirika ndani ya ufalme wa Mungu.’

7/25/19, 18:24 - +255 719 513 9**: Yes!

7/25/19, 18:26 - Prophet:   Ahadi zako kwa Mungu zipo katika ufalme wake na nadhani hadi hapa kila mtu anajuwa maana ya Ufalme wa Mungu ni nini kama kuna mtu bado hajaelewa anaweza akanyoosha mkon  

Kwa sababu, nataka nizame deep sasa mahali ambapo tunahitaji maarifa na ufahamu wa kutosha.

7/25/19, 18:59 - Vesta: Shalom…

7/25/19, 19:05 - +255 719 513 9**: Ufalme wa Mungu ni serikali iliyopo mbinguni au mamlaka kama nimekosea nieleweshe…

7/25/19, 19:09 - Prophet:   Ndiyo ni mamlaka lakini ambayo tunayo hapa duniani kwa kumuamini Yesu. Kwa hiyo, ili tuuelewe vizuri Ufalme wa Mungu ni nini, tunatakiwa kuelewa katika taswira ya kuwa na ‘MAMLAKA’...USIPOELEWA UNA MAMLAKA ni vigumu kama Mwana wa Mungu kutumia hayo mamlaka.  Nilisema kuwa, maombi siyo kumpa Mungu taarifa bali ni kutumia mamlaka uliyopewa kupitia ufahamu wa Neno la Mungu katika kudai haki yako! Jambo la Kwanza ni kuelewa kuwa:

  1. ‘UMEPEWA MAMLAKA’ na jambo la pili
  2. ‘UTUMIE MAMLAKA ULIYOPEWA’

Unatumiaje sasa mamlaka uliyopewa na ni wapi panaonyesha kuwa tumepewa mamlaka na tunaitumia hiyo mamlaka katika mazingira gani?  Ndio mahali ninapoelekea kufafanua. Kwanza kabisa, unatakiwa kuelewa kuwa mamlaka tuliyonayo ni kupitia kulifahamu na kuliamini neno la Mungu, yaani, ‘Ahadi zake.’ Haitoshi tu kusema mamlaka ni neno la Mungu bali hilo neno unatakiwa ulifahamu na uliamini kwanza ili uwe na hayo mamlaka unayohitaji kama Mfalme katika Ufalme wa Mungu, kwa sababu, sisi ni Wafalme tukiwakilisha mamlaka ya Mungu hapa duniani.

Ufunuo 5:10

‘Ukawafanya kuwa Ufalme na Makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.’ Kwa hiyo, unatakiwa uelewe mamlaka uliyo nayo ni katika ‘KUTAWALA NCHI’; yaani kutawala mazingira yaliyo kuzunguka...usiseme au usifikiri kuwa mamlaka tuliyo nayo sisi ni ya kiroho tu, hapana. Mamlaka tuliyo nayo sisi ni kutawala ULIMWENGU MUNGU ALIOUUMBA kwa ajili yetu, nikisema ULIMWENGU namaanisha mambo yanayo onekana na yasiyoonekana kwa pamoja.

7/25/19, 19:41 - Vesta: Amen!

7/25/19, 19:44 -  Prophet:  Kama sisi ni wafalme mbele za Mungu basi tunawajibu wa kuitekeleza na kuitumia mamlaka Mungu aliyotupa na sio kuanza kumbembeleza Mungu atende katika maisha yetu...hapa ndio Wakristo wengi wanaonewa na nguvu za giza na changamoto wanazopitia kwa sababu maombi yao yanalenga katika kumbembeleza Mungu na kumtaarifu Mungu kuhusiana na changamoto zao na shida zao.

Ukifanya hivi utakuwa unalia kila siku na utaona Mungu hayupo pamoja na wewe au hasikii maombi yako. Niseme kitu kimoja… Sisi kama Wakristo, hatuishi kwa maombi ya kumbembeleza Mungu na kumtaarifu Mungu; tunaishi kwa IMANI!

Waebrania 10:38

[38] ‘Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani*; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha nay

Kuishi kwa imani kukoje?

Wakorinto 4:13

‘Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;’  Lazima ufahamu na uelewe kuwa imani inatakiwa ifanyiwe mazoezi.  

Yakobo 1:22-23, 25

[22] ‘Lakini iweni watendaji wa neno,’ wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. [23]Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. [25] ‘Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atabarikiwa katika mambo yake.’

Ahaaa kwa hiyo, kuna baraka inadhihirika katika KULITENDA NENO! Na tunalitendaje hilo neno? Tunalitenda neno kwa kupitia UKIRI WETU...tunaamini hivyo TUNAKIRI! Unatakiwa uamini kwanza na hivyo ukiri! Ukifikiri sawa sawa utaaamini sawasawa na ukiamini sawa sawa utakiri sawa sawa na ukikiri sawa sawa utapata matokeo yaliyo sawa!

Yoshua 1:8

[8] ‘Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.’

Kuamini tu haitoshi unatakiwa uifanyie mazoezi imani yako kupitia KUKIRI / KUNENA / KUTAMKA kile unachokiamini kupitia kulifahamu neno la Kristo ukifanya hivi utaanza kuona matokeo ya kile unacho kiamini...kwa sababu vinywa vyetu vina mamlaka ya kuumba na kutengeneza maisha yetu...kupitia kinywa chako unaweza bomoa maisha yako au ukajenga maisha yako...huu ni utaratibu ambao Mungu aliuweka kwa sisi tulioumbwa kwa sura na mfano wake...ukisema unafanana na Mungu ni kwamba tunasifa na uwezo wa kuumba maisha yetu kupitia vinywa vyetu 

Methali 18:20-21

  1. ‘Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; atashiba mazao ya midomo yake.’
  2. ‘Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.’

Ukitaka uone matunda / matokeo ya ahadi za Mungu katika maisha yako lazima ujifunze kutumia kinywa chako vizuri kunena / kukiri / kutamka mema katika maisha yako!  Ili Ukiri vizuri ni lazima uamini vizuri...huwezi sema utakiri vizuri pasipo kuamini vizuri na huwezi amini vizuri kama huna bidii ya kulifahamu neno la Ufalme wa Mungu kwa sababu imani huja kwa kulifahamu neno la Kristo!

Warumi 10:17

[17] Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.’  Na imani iliyo thabiti yaani imani iliyo na msingi na mizizi ndiyo inayoleta matokeo utakapo ikiri...huwezi kupata matunda pasipo kupanda mbegu...mbegu ndiyo neno la Ufalme wa Mungu. Usipo lifahamu hilo neno na ukalifanyia mazoezi kwa kukiri / kunena / kulitamka hilo neno hautapata matunda / matokeo ya hilo neno...sasa changamoto kubwa ya leo ni Wakristo wanaotaka majibu ya mambo ambayo hawajayafanyia kazi; hawajapitia mchakato wa kulifahamu neno na kulikiri hilo neno ili lilete matokeo kwa sababu hawajui kuwa wana mamlaka na wanambembeleza Mungu na kumpa Mungu taarifa wakifiri Mungu atasikia na kujibu; lakini huu sio utaratibu wa ufalme wa Mungu.

Kwa hiyo, maombi ni nini? Mnatakiwa kuelewa maombi siyo kumpa Mungu taarifa bali ni kutamka na kukiri kuwa mmepokea haja zenu sawa sawa na ahadi na mapenzi ya Mungu kupitia neno lake na sio kumbembeleza Mungu...unatakiwa ukiri hizo ahadi na kuzidai kuwa umepokea tayari hayo ndio maombi, hiyo ndio sala!

Marko 11:24

[24] ‘Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.’  Kwa hiyo, hayo yoyote tuyaombayo ni mambo gani au ni maombi ya namna gani? Tuliangalie neno sasa

Marko 11:23

[23] Amin, nawaambia, ‘Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametokea, yatakuwa yake.’ Hayo maombi ni kutamkia kuyaambia matatizo yako. Changamoto zako, shida zako ambazo ni mlima katika maisha yako kuwa zihame na kuamini kuwa ulichokitamka kimeshatokea kwa kutumia mamlaka ya kinywa chako kwa kurudia rudia, ndipo utaona hayo matatizo yakiondoka.  Kwa hiyo, kwanza kabisa tunatumia mamlaka tuliyopewa katika vinywa vyetu katika kukiri na kudai ahadi za Mungu katika maisha yetu kwa kuyaambia matatizo na changamoto tunazokutana nazo zihame na ziondoke katika maisha yetu...

Kesho nitazungumzia namna ya kujenga imani iliyo na mizizi ili tupate matokeo yaliyo sahihi. kwa leo naishia hapa. 

7/25/19, 20:31 - +255 767 540 7**: Hongera na asante!

7/25/19, 22:19 - Vesta: Amen, nimebarikiwa…

7/25/19, 22:41 - +255 719 513 9**: Be blessed!

7/26/19, 06:03 - +255 654 333 5**: …kweli nimebarikiwa sana na mafundisho haya...

7/26/19, 11:06 - +255 713 626 4**: Asante mtumishi naelewa mpaka hasira!

7/26/19, 11:16 - Prophet: laugh

7/26/19, 11:17 - +255 654 333 5**: Mimi mwenyewe naona sijui nilichelewa wapi kupata madini haya...

7/26/19, 11:18 - Prophet: Madini haya yanaitwa 'Biblioxonite', huwezi kuyapata mahali pengine popote duniani ila hapa!

7/26/19, 11:19 - +255 654 333 5**: laugh