DARASA UK.5

 

DARASA UK.5

 

 

 

WANAFUNZI WA KRISTO: 

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

 

 

Prophet Joachim Francis

 

...KUTOKA UK. 4

 

+255 654 333 5**: Mtumishi wetu mimi binafsi ningeomba somo la NGUVU YA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU… Wengi wetu tunajikuta tunasoma neno lakini namna sahihi ya kulitafakari ndio inakuwa shida.

 

Vesta: Shalom!

 

+255 654 333 5**: Shalom

 

PROPHET:  Naelewa na ndio nitaelekea huko kwenye mafundisho yajayo.

 

PROPHET: Shalom Naomba mnitumie majina yenu kwa ajili ya kuwaombea binafsi kwenye maombi yangu.

 

+255 686 361 1**: Naziel Manento

 

+255 718 485 9**:

 

Vesta:                     V. J. Sam

 

+255 714 414 1**: R.

 

+255 654 333 5**: B. MWAILENGE

 

+255 654 333 5**: Z. MUSSA

 

+255 754 650 6**: A. D.

 

+255 719 513 9**: E.

 

+255 713 626 4**: Tutindaga

 

+255 713 626 4**: B.

 

+255 785 918 6**: M. Ernest

 

+255 755 543 9**: G. J. Ernest

 

Laura:                     L. Anthony

 

PROPHET: Shalom Wanafunzi!

 

Vesta: Shalom!

 

PROPHET: added +255 682 867 1**

 

+255 654 333 5**: Yesu Bwana!

 

PROPHET: Tunaendelea. Bwana Yesu asifiwe sana. Nampenda Yesu na natumaini mnampenda Yesu pia. Kabla sijaendelea na mafundisho, mawazo yoyote uliyonayo ya wasi wasi wa maisha yaweke pembeni kwanza na umuachie Mungu.

 

Haya tuendelee na somo la mara ya mwisho

 

Nilimalizia kufundisha kuhusu namna USIKIVU wetu ni muhimu katika kumsikia Mungu na kuwa usikivu ninao uzungumzia ni uwezo wa kupokea maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu...na kuwa kiwango chetu cha usikivu ndio kiwango chetu cha imani lakini ili imani iwe timilifu inahitaji UTII ambao chimbuko lake ni UPENDO na hapa ndio nawakumbusha kuwa, hatuwezi kuwa ROHONI pasipo na NIA ya KUMPENDEZA MUNGU ambayo ni matokeo ya UPENDO wetu kwa MUNGU.

 

Usikivu ni njia ya kwanza ya kuwa mtu wa rohoni. Leo naendelea na njia ya pili ambayo ni UTII.

Nataka tutambue jambo moja; kuwa, msingi wetu kama wakristo ni IMANI yetu ambayo imegawanyika katika matawi makuu haya:

 

  1. Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu
  2. Kufa kwake na kufufuka kwake

Huu ndio msingi wa imani Yetu kama waamini katika wokovu. Kama huyajui haya mambo kwa kina na huyaelewi hujaokoka bado; hauna tofauti na mpagani.

 

Huwezi itii sauti ya Mungu au kutii maelekezo unayopewa kama huna mapenzi na Mungu kwanza...kama humpendi Mungu kwa dhati huweizi kuamua kutii kile unachoambiwa kufanya na Roho Mtakatifu, upendo huu haujengeki ndani ya siku moja unajengekea hatua kwa hatua; yaani imani inakuwa hatua kwa hatua unavyozidi kumfahamu Mungu kupitia neno lake.

 

Ndio nawaleta kwenye swali lililoulizwa kuwa ni namna gani sahihi tunayoweza kutafakari neno la Mungu.

Naanzia hapa ili tupate ufahamu wa kutosha. Niseme hivi, ili neno la Mungu au maarifa ya Mungu yawe ndani yetu au sehemu ya maisha yetu lazima tuamini kile tunachokisoma ili kiwe sehemu ya roho zetu na tunaweza fanikisha hilo jambo kwa kutumia kanuni ya KULITENDA au KULIISHI neno kupitia VINYWA vyetu.

 

Joshua 1:8

‘Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,’ bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Neno la Mungu ni kama mbegu usipo fanya jitihada ya kuipalilia hiyo mbegu kwa ukiri wako ili liwe sehemu ya maisha yako na uliamini litakuwa ni neno la kawaida tu unalolisoma kila siku na halita zaa matunda katika maisha yako.

 

Kwa hiyo, tafakari nzuri na inayoleta matokeo ni kukiri au kujisemesha neno la Mungu kila siku unapolisoma na ipo hivi....katika kulifanyia mazoezi unatakiwa uchague andiko fulani moja uwe unalisoma na kulikiri kila siku hata kama hulielewi uwe unalisoma na kulikiri kwa kulirudia rudia hata wiki moja mwezi mmoja andiko la mstari mmoja mfano:  Waebrania 11:1 ‘Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.’ Ukiwa unatafakari na kukiri huo mstari kila siku...unaamka nao...unatembea nao...unalala nao...kila siku ...lazima imani ijengeke ndani yako utake usitake...tatizo ni kwamba, tunataka tusome na kuelewa mambo mengi wakati mmoja...hapana, ni hatua kwa hatua, mstari kwa mstari, andiko kwa andiko.

 

Ukianza tafakari ya namna hii, utajikuta unakiu kubwa sana ya kuzidi kumjuwa na Kumpenda Mungu wewe mwenyewe bila hata ya kulazimshwa au kusukumwa na hapo ndio hata macho yako ya kiroho yanafunguka zaidi na ndio hali ya UTII itaanza kujengeka zaidi ndani yako kwa sababu imani imeshaanza kujengeka kupitia neno la Mungu ndani yako.

Hali hiyo ikisha jengeka ndani yako, ndio inakuwa rahisi wewe kutii kile unachoambiwa na Roho Mtakatifu...Sasa hapa nataka nieleze jambo pana kidogo katika swala la Kumtii Roho Mtakatifu...ipo hivi...

 

Mungu ni roho na sio mwili...na lazima utambue kuwa MAPENZI YA MWILI HUSHINDANA NA MAPENZI YA ROHO...na ili tumpendeze Mungu ni lazima TUJIKANE NA KUYAKATAA MAISHA YETU KWANZA ndio tuishi maisha ya KUMPENDEZA MUNGU…

 

Nitaeleza mambo magumu lakini ndio uhalisia wa maisha ya kikristo:

 

6:20,22

[20] ‘Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.’ [22] ‘Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.’

 

Nataka ushike hili neno: ‘WATUMWA WA MUNGU’ Hapo watumwa au mtumwa inamaanisha ‘MTUMWA KATIKA KUTII KILE UNACHOAMBIWA KUFANYA.’

 

Mtumwa hana la kusema; kazi yake ni kutii...na kumbuka nimefundisha na kusema kazi kubwa ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza au kutuelekeza sisi kuyatii mapenzi ya Mungu katika maisha yetu...kwa hiyo, tunakuwa watumwa wa Mungu kupitia kuongozwa na Roho Mtakatifu katika hali ya kuwa Wana wa Mungu na tulikuwa watumwa, yaani watiifu pale tulipoamua kutii mafundisho ya Kristo.

 

 

6:16-17

[16] ‘Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii,’ ‘mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii,’ kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au ‘kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.’

[17]Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, ‘lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake…’

 

Kwa hiyo, ipo hivi wapendwa...kuna haki ya Mungu inayopatikana kwa ‘IMANI’...na haki ya Mungu inayopatikana kwa ‘UTII.’

 

Haki ya Mungu inayopatikana kwa ‘IMANI’ ni ile inayotuletea sisi haki mbele za Mungu na kututakasa na dhambi...haki inayopatikana kwa ‘UTII’ ni haki inayotupatia ‘UPENDELEO WA MUNGU’ hapa duniani.

 

10:34-35

[34] Petro akafumbua kinywa chake, akasema, ‘Hakika natambuwa ya kuwa Mungu hana upendeleo;’

[35] ‘BALI katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.’

 

Petro anakiri mwenyewe kuwa mtu anayempendeza na kumtii Mungu; hupata UPENDELEO kutoka kwa Mungu akiwa hapa duniani hata kama huyo mtu hajamjua Kristo na kupokea wokovu ....kwa hiyo, kuna namna tunafanyika Watumwa wa Mungu lakini utii huu au utumwa huu unategemeana na ELIMU / MAFUNDISHO unayoyapata kuhusiana na Mungu...ulifundishwa nini na unaamini nini ndio kitasabisha uwe mtumwa wa Mungu au mtumwa wa vitu vingine.

 

Kwa hiyo, utii wetu unaanzia katika kukubali kuwa WATUMWA WA MUNGU...nataka nieleweke vizuri kwanza...huwezi kumtii Mungu kama hujakubali kuwa mtumwa wake! Nikisema kuwa mtumwa wa Mungu namaanisha huna mamlaka binafsi au maamuzi binafsi ya maisha yako...nataka ieleweke kwa uwazi kabisa…yaani ni hivi, ifike mahali mapenzi yako yafe na mapenzi ya Mungu yaishi kupitia wewe. Huku ndio kunaitwa kujikana na kubeba msalaba...ndio maana yake hii.

 

Luka 9:23-25

[23]Akawaambia wote, ‘Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.’ [24] ‘Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.’  [25] ‘Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?’

 

Changamoto kubwa ni watu wakishakutana na mafundisho kama haya, hutasikia amina wa Bwana asifiwe… Kwa sababu watu wengi wanajipenda wao na maisha yao hawataki kumtii Mungu; wanataka kupata mafanikio...magari...safari za Ulaya...na mipenyo…

 

Sasa, hapa ndio kiini chenyewe cha kumjuwa Mungu… Kwa hiyo, jambo la kwanza, Roho Mtakatifu atakuja kufanya ni kukuongoza katika kuyaua maisha na mapenzi yako binafsi na tamaa zako za mwilini za kujipendeza wewe na ubinafsi wako na kuanza kukufanya uishi kwa ajili ya kumpendeza na kutimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yako...hii ndio kazi ya kwanza na maelekezo ya kwanza kabisa Roho Mtakatifu ataanza kukupa sio kukuambia utafanikiwa sijui utapata ndoa na biashara itafanikiwa, hapana.

 

8:13-14

[13] kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali ‘kama mkiyafisha(mkiyaua) matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.’

[14]Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

 

Lakini Roho Mtakatifu ataanza kufanya hivyo kama ukimruhusu kwa kuwa na nia ya kukubali kujikana na kutaka kumpendeza Mungu kwa kutimiza mapenzi yake na sio mapenzi yako…na hatua hiyo ni hatua ya kushindana na mapenzi yako binafsi kwa kujikana wewe na mambo yako yasiokuwa mapenzi ya Mungu...huko ndio kunakoitwa ‘KUUSULUBISHA MWILI NA TAMAA ZAKE.’

 

5:24

‘Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.’ Ukishafia mapenzi yako na kuanza kuishi kutimiza mapenzi ya Mungu hapo ndio unaishi pamoja na Mungu katika maisha yako...hapo ndio mtu anaweza kusema ana Mungu katika maisha yake... Kwa hiyo, bado tunaendelea na somo laa kipengele cha pili cha namna ya kuenenda rohoni cha UTII. Somo nitakalo fundisha tena litahusu ‘namna ya kushindana kutii mapenzi ya Mungu katika maisha yako’ na kuna siri kubwa nitaifundisha hapo ambayo ukiijuwa hakuna changamoto katika maisha itakayo kushinda hata mara moja!

Shalom!

+255 719 513 9**: Shalom!

Vesta: Amen!

Vesta: Merci seigneur!

+255 654 333 5**: ********   

PROPHET: Aminaa!

+255 714 414 1**: ******Amen!

+255 786 850 0**: Amen, asante kwa kuniunga na hii familia**

PROPHET: Shalom

PROPHET: Nawatakia Jumapili Baraka…

Vesta: Shalom!

+255 654 333 5**: Shalom...asante mtumishi, nawe pia. LAKINI SIO UNATUKARIBISHA MBAGALA DARAJANI KWENYE IBADA?

PROPHET: Kama kawaida…

PROPHET:  Ibada Karibu sana… Ibada inaanza saa nne asubuhi!

+255 719 513 9**: Shalom!

PROPHET: Shalom!

PROPHET: Nipo

+255 713 626 4**: Ameen!

+255 714 414 104: ******Amen Mungu akubariki…

+255 764 252 5** left

PROPHET: Shalom

PROPHET: I hope

+255 654 333 5**: Amina mtumishi...pole na jukumu la kuchunga kondoo na huduma…

+255 714 414 1**: Shalom, Mungu ni Mwema.

PROPHET:  Nitaendelea Jumamosi.

Vesta: Shalom, sawa tunasubiria…

+255 658 999 6**: Shalom…

PROPHET: Shalom! Nilikuwa nimebanwa kidogo na huduma. Now free Leo nitaendelea na mafundisho.

Vesta: Shalom, welcome back!

+255 714 414 1**: Shalom******

PROPHET: Shalom?

+255 658 999 6**: Shalom!

Vesta: Shalom, Mungu nimwema, naendelea vizuri!

+255 654 333 5**: Shalom...

PROPHET:  Naomba mnipe muda nimalizie mfungo ndio nitakuwa huru kufundisha, sasa hivi nakuwa busy na maombi na kumtafakari Mungu…

PROPHET: Nikimaliza kuanzia wiki baada ya wiki ijayo ndio nitakua huru kabisa

+255 714 414 104: Shalom, sawa Mtumishi, usituache kwa kila ombi uombalo******

Vesta: Unikumbuke kwenye maombi yako mtumishi

PROPHET: Nawaombea

PROPHET: Nawakumbuka

+255 719 513 9**: Amen!

+255 686 361 1**: Amen!

+255 714 414 1**: ***Ubarikiwe

+255 754 650 6**: Amen

+255 658 999 6**: Aminaaa!

PROPHET: Shalom!

PROPHET: Nashukuru Mungu …

+255 658 999 6**: Shalom!

+255 658 999 6**: Nimefurahi Mtumishi!

PROPHET:  Nilikuwa kwenye mfungo na maombi… Kwa sasa nimerudi. Kwa hiyo, tutaendelea kujifunza NENO na pia mwenye shida binafsi pia anaweza akanitafuta inbox, neema ya Mungu ipo kwa ajili ya kila mmoja wetu…

+255 658 999 6**: Amiiinaaaa!

Laura: Ameeen!

+255 754 650 6**: Shalom!

Vesta:  Shalom…

PROPHET: Shalom! Bwana Yesu ?

+255 686 361 1**: Amen!

PROPHET: Leo . Mara ya mwisho tuliishia kwenye somo linalohusu “KUWA ROHONI”- Ndio nitakapo endelea kwa leo.

PROPHET:  Kuwa rohoni ni jambo la muhimu kwaajili yetu hasa tukitaka kumuona Mungu katika maisha yetu kila siku. Kuwa rohoni kunatakiwa kuwe ndio maisha yetu ya kila siku. Kuwa rohoni ni lazima na ni wajibu wa kila mmoja. Kuwa rohoni kunaanzia kwenye mitazamo yetu kuhusiana na Mungu na sisi binafsi. Kuwa rohoni ni mtazamo na mtazamo huo unaanzia katika kile ambacho mtu anakiamini kuhusiana na Mungu. Imani ya mtu ndio inamfanya awe rohoni au mwilini na inategemeana na kile mtu anachokiamini kuhusiana na Mungu anayemjua na ndicho kinachoamua matokeo gani huyo mtu ayapate kwenye maisha yake ya kila siku.

Kuwa rohoni ni mtazamo unaonzia ndani ya mtu kujijua na kujifahamu yeye kwanza na uwezo alio nao ndio mtu huyo ataweza kumfahamu na kumuabudu Mungu kwa usahihi. Kwa sababu, huwezi kusema unamuamini Mungu ili hali na wewe hujiamini binafsi. Yohana 4:24 – ‘Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.’ Vile unavyovitaka vitokee katika maisha yako havitegemeani na jinsi unavyoomba au kumtolea Mungu sadaka...vinategemeana na jinsi unavyojijua na kujiamini wewe kwanza kwa sababu kila kitu unachokitaka kipo ndani yako na sio nje yako.

Mungu unayemtafuta anapatikana ndani yako na anaishi ndani yako sio nje yako. Warumi 10:2 – ‘Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.' Kumtafuta Mungu aliye nje yako ndio kuabudu sanamu kwenyewe kwa sababu sehemu ya kwanza ya Mungu kujidhihirisha kwako ni kupitia ndani yako. Nikisema kupitia ndani yako, namaanisha vile vitu ambavyo Mungu aliwekeza ndani yako na alivyokupa kama uwezo ulio nao wewe katika maisha yako ya kila siku…

PROPHET:   Kwahiyo, mambo yoyote ya mwilini yanaanzia au ni sababisho au matokeo ya mambo yanayoendelea rohoni na kila jambo linaloendelea rohoni ni mjumuisho wa yale yanayo anzia kwenye mawazo au fikra husika za mtu. Hakuna jambo utakalo lihitaji ambalo halitaanzia ndani yako. Ndio maana nimuhimu kujifunza kuwa rohoni.

PROPHET:  Sasa changamoto kubwa ya leo ni kwamba, watu wengi wanamtafuta Mungu asiye na matokeo na hiyo ni sababu Mungu aliyetambulishwa kwao ni mungu wa mwilini na sio rohoni. Mungu au matendo ya Mungu yanaonekana kwa njia ya IMANI na imani ni jambo la kiroho linaloanzia na kujengwa ndani ya mtu binafsi. Imani inaanzia ndani yako na ni jukumu lako na ni kupitia hapo Mungu anaonekana sio kwengineko.

PROPHET: Sasa, Imani …

PROPHET: Shalom! .

+255 754 650 6**: Sawa Pastor!

PROPHET:  Nitaendelea kesho kufundisha saa sita mchana, nitaanza darasa! Tutakuwa na muda wa kutosha wa kujifunza.

+255 754 650 6**: Sawa sawa kabisa mtumishi.

+255 654 333 5**: ********barikiwa !

+255 763 194 9**: Amina mtumishi na MUNGU wa Mbinguni akubariki saana!

PROPHET:   Shalom!

PROPHET:  Naendelea . Niliishia kusema ‘Imani ni Ibada.’ Na mfumo wa ibada ambao tunatakiwa kuwa nao ni wa rohoni unaofanya kazi kwa Imani. Kwa hiyo, kama imani uliyo nayo sio kwa Mungu aliye Roho...na aliyeko ndani yako ni ngumu sana kuona matokeo ya nguvu za Mungu katika maisha yako...

PROPHET:  Nieleze kitu kimoja: Waefeso 3:20 – ‘Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;’ Mungu ni Roho...na haonekani na alivyotuumba alituumba kwa namna ya kufanana na yeye katika utendaji kazi na uwezo...na huo uwezo upo ndani yetu...kupitia namna ya ‘TAFAKARI’ au ‘MAWAZO. Maisha yako yanaanza kwenye mawazo yako....au yale unayo yatafakari na kuyatamani yatokee kwako...hapo ndipo maisha yako na yangu yanapoanzia…

PROPHET:  Sasa uwezo wa kutokeza yale unayoyatamani au kuyatafakari ndio uwezo huo unaitwa ‘imani’ kwa lugha ya kibiblia, imani hiyo inakaa ndani mwetu sisi kwenye ‘fahamu zetu au mioyo yetu’ kwa lugha ya kibiblia. Kwa hiyo, ili tuwe na Imani, tunatakiwa kujua imani hiyo inakaa wapi. Imani ipo kwenye MOYO biblia imetumia lugha picha ya MOYO kama eneo ambapo imani ya mtu hukaa...na haimaanishi moyo kama moyo unao sukuma damu hapana; inazungumzia eneo katika fahamu zetu ambapo hilo ndio lina fanana na Mungu au lina uwezo wa Kiungu ndani yetu katika kutokeza yale tunayo yatamani yatokee na kuyawaza.

PROPHET:  Methali 4:23 – ‘Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndio chanzo cha maisha.’

Waefeso 3:16-17 - [16] ‘awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.’ [17] ‘Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;’ Tuliumbwa kufanana na Mungu ndani yetu...kwa hiyo, kule kufanana na Mungu kunafananishwa na uwezo wetu wa kufikiri...kwa hiyo, ukiona neno MOYO kwenye biblia lina maanisha eneo ndani ya  FAHAMU zetu

Fahamu za mwanadamu zimegawanyika sehemu mbili:

‘FAHAMU ZILIZO MACHO’

‘FAHAMU ZILIZO LALA’

Kwa kiingereza limetumika neno ‘CONCIOUSNESS’ na ‘SUBCONCIOUSNESS.’

PROPHET:  Nieleze jambo kwa kina kidogo na kwa urahisi ili tuelewane wote kwa pamoja. Ukilala na fahamu zako za kawaida zikipumzika huwa unaota ndoto. Na ndani ya hiyo ndoto unaweza ukajiona unatembea na unakula muda mwingine. Sasa, yule unaemuona kwenye ndoto alikuwa anakula na kutembea ndio wewe uliye huko rohoni...sasa kinachokufanya ukiamka ukumbuke kuwa jana usiku kwenye ndoto ulikula pilau ni ‘FAHAMU ZAKO ZILIZO LALA’ au ‘SUBCONCIOUS MIND!’ Na Mungu ndio anahusika kwa asilimia zote kushughulika na mtu huyo wa ndani sio nje. Sasa kinachotokea kwa asilimia kubwa leo ni kuwa wengi wetu tunamtafuta huyu Mungu aliye nje ya hapo.

Na hilo lina tokana na kwamba watu wengi wanafundishwa kumtafuta Mungu aliye nje na wao na Mungu asiyefanana na wao. Na hapo ndipo watu wanakosa kuwa na mahusiano na Mungu kwa kuaminishwa tofauti na uhalisia wa Mungu. Uhalisia wa Mungu unaanzia kwetu binafsi... Mwanzo 1:27- ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.’ Roho yako ndio inayofanana na Mungu. Kwa ufupi, wewe na Mungu ni kitu kimoja. Kwa hiyo, ulivyoumbwa uliumbwa kwa namna ya kufanya ibada wakati wote kwa namna ya rohoni na ibada inazungumziwa ni ‘KUMLETEA MUNGU UTUKUFU DUNIANI’ kuleta utukufu au kumtukuza Mungu duniani maana yake ni kuchukua nafasi ya Mungu duniani. Mwanzo 1:28 - ‘Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.’

PROPHET:  Kumwakilisha Mungu duniani ni ‘KUTAWALA VILE ALIVYOVIUMBA’ Na namna pekee ya kutawala vile alivyoviumba Mungu ni kuvitawala kwa Imani; yani kwa namna ya kiroho kwa sababu Mungu aliumba vyote kwa Imani; yani vilianza kwanza rohoni ndio vikadhihirika mwilini. Waebranka 11:3 - ‘Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.’ Biblia inaposema Mungu aliumba ulimwengu kwa neno lake, inamaaisha kiliocha anza kuumba ni wazo la Mungu kwanza kwa namna isiyo onekana. Kwa , lile wazo lilijenga imani iliyosababisha ulimwengu utokee.

Sasa huyo Mungu aliyeumba ulimwengu ndio akamuumba mtu atiishe vile alivyoviumba kwa maana nyingine ni kwamba jukumu la Kuishi hapa duniani na kutawala sio La Mungu aliyetuumba ni jukumu letu sisi(wanadamu)!

Kinachohitajika hapo ni MAARIFA kuhusiana na uhalisia wako binafsi!  ? Wewe sio huyo unaemuona kwenye kioo...wewe sio huyo unaeitika kwa kuitwa jina… Wewe ni mfano halisi Wa Mungu!

PROPHET:  Ukilielewa hili na ukaliamini hili utaanza kutembea kwenye viwango na uhalisia wa Kiungu.

Sasa imani zilizondani ya watu wengi ni kwamba Mungu anaweza kutenda! Sawa ni sahihi...ila nataka niwaajulishe jambo lililo sahihi zaidi ya hili… Wewe unaweza! Ukiweza wewe Mungu ameweza kwa sababu uwezo wa kutenda wa Mungu unategemeana na kadiri tunavyo amini kuwa tunaweza sisi kwanza.

PROPHET:   Wengi hawajiamini wao kama wao halafu wanadai wanamuamini Mungu.

Na ipo hivi: Maombi mengi watu wanaomba hayana majibu sababu wanamkana Mungu bila wao kujijua wakidhani ni maombi sahihi ya kujinyenyekeza na kujishusha.

Mfano: Mtu anaomba nakusema, ‘Bwana mimi siwezi bila wewe…’ Unavyokiri huwezi bila yeye; wakati huo Mungu anakuhitaji wewe ili atimize mambo fulani duniani na wewe unakiri huwezi...ndio mnaanza kupishana hapo…

PROPHET: Yanaonekana ni maombi ya kujinyenyekeza lakini ni maombi yasiyokuwa na ufahamu sahihi kuhusiana na Uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Kadiri unavyozidi kujiamini; wewe unazidi kumpa nafasi Mungu atende kupitia wewe na kadiri unavyomuamini Mungu. Kuacha kujiamini wewe ndivyo unavyozidi kupunguza uwezo wa Mungu kutenda kupitia wewe.

PROPHET:  Kwa hiyo, ukitaka uanze kuona udhihirisho wa uweza wa Mungu katika maisha yako, anza kujenga tabia ya kujiamini katika kila jambo unalofanya.

PROPHET: Shalom!

+255 713 626 4**: !

+255 713 626 4**: Barikiwa!

+255 713 626 4**: Mi nasubiria kwa hamu…

Vesta: Shalom!

PROPHET: Shalom!

+255 713 626 4**:

PROPHET:  Leo …

PROPHET:  Tutaendelea…

PROPHET:  Kuwa na Amani, mambo ni mengi ila Mungu atatupa neema!

+255 763 194 9**: Amina!

PROPHET:  Shalom ! ? Leo naendelea na somo: ‘IMANI NI IBADA!’ Nimuendelezo wa somo la KUENENDA ROHONI. Mara ya mwisho nilikuwa nazungumzia swala la ‘KUJIAMINI.’

Nikasema, kama huwezi kujiamni huwezi kumuamini Mungu; sababu, imani ni kuwa na ‘uhakika’ na mambo unayoyatamani na kuyatarajia wewe binafsi kwenye maisha yako - Waebrania 11:1. Basi imani ni kuwa na ‘hakika ya mambo yatarajiwayo’, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

PROPHET:  Leo . Kitasaidia kujenga uelewa kuhusiana na Imani

Kunatofauti kati ya kuwa na ‘IMANI’ na ‘KUAMINI.’

Imani ni tokeo la kuamini kwa mtu ila kuamini ndio kunaanza kwanza. Kuamini ‘kunahusiana na sisi binafsi katika kujiamini sisi katika kile tunachokitamka na kuomba.’ Na Yesu alifundisha na kusisitiza katika imani hii ya kujiamini ambayo inatusaidia kujibu maombi yetu husika tunayo omba au yale tunayotamani yatokee.

Marko 11:23-24 - [23] Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, ‘wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.’

[24]Kwa sababu hiyo nawaambia, ‘Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.’ Kuamini ni kanuni ya Kiungu ambayo Mungu alimuamba mwanadamu aishi kupitia hiyo ili aishi kwa kuona udhihirisho wa uweza wa Mungu katika maisha yake. Hapo ndio tunakuja kuelewa kuwa katika kuomba Mungu hajibu maombi yetu bali ‘kuamini kwetu ndio kunafanya yale tunayo yaomba yatimie.’ Kuamini kwako ndio kunatengeneza ‘UHUSIANO’ kati yako wewe na yale unayotaka yatimie. Uhusiano huo ndio ‘NGUVU’ inayosababisha maombi yako yatimie au ya dhihirike katika maisha yako.

9/13/19, 20:33 - PROPHET:  Katika kuamini kuna jambo ambalo ni lazima tuelewe ili tuweze kuamini.

Kuamini ni kujenga ‘UHAKIKA’ kwa yale unayoyatarajia au kuyatamani yatokee katika maisha yako na uhakika huo unaujenga kwa kujiamini wewe kuwa ‘UMESHAPOKEA’ yale uyatarajiayo.

9/13/19, 20:41 - PROPHET: Usipo amini kuwa umeshapokea maombi yako hata kuomba kutakuwa ni mzigo kwako kwa sababu huna uhakika kuwa unayoomba yatatokea au utapata majibu yako. Ukiwa unashaka tayari imani ipo mbali na wewe na utakuwa unaishi maisha ya kubabaisha kuomba kwa sababu hata nguvu ya maombi itakuwa mbali na wewe.

Kanuni hii ya kuamini kuwa umeshapokea unayoyaomba ni muhimu sana katika kujenga mahusiano yako na yale unayo yaomba kwa sababu usipotengeneza uhusiano au ‘mvutano’/ ‘attraction’ kati yako na yale unayo yaomba kupitia ‘Kuamini’ kwako ni ngumu kupokea kitu kwa sababu ni kanuni ya Ufalme wa Mungu hapa duniani. Mungu hahusiki kukujibu maombi yako bali wewe ndio unahusika kwa kujenga na kukuza uwezo wa kuamini kwako.

9/13/19, 21:07 - PROPHET:  Kanuni ya kuamini kwa kujiamini ndiyo inaakutengenezea Imani kwa Mungu.

9/13/19, 22:12 - PROPHET:  Mwenye ?

9/13/19, 22:16 - PROPHET:  Naweka somo fupi ili tupate uwanja wa maswali…

9/14/19, 12:48 – PROPHET:  Shalom!

9/14/19, 13:38 - Laura: Shalom , Prophet!

9/14/19, 14:06 - +255 654 333 5**: Shalom!

9/14/19, 14:25 - +255 712 090 9**: Shalom!

9/14/19, 14:36 - +255 754 650 6**: Shalom!

9/14/19, 14:36 - +255 717 930 2**: Shalom Prophet!

9/14/19, 14:56 - PROPHET: Jana Imani.

Nataka maoni na uelewa wenu kuhusu hili…

9/14/19, 15:12 - +255 763 194 9**: Nilivyoelewa mimi imani huambatana na matendo, mfano, uumwapo kisha ukamwomba MUNGU akuponye na kuamini moyoni mwako kuwa umepona baada ya maombi ukaanza hatua ya kukiri kuwa mimi siumwi na kuthubutu kufanya ambayo hukuweza kuyafanya kabla ya maombi ni hakika utapokea uponyaji kwani MUNGU hupendezwa na wanaothubutu pasipo shaka yeyote.

9/14/19, 15:25 - +255 763 194 9**: Mfano, mimi nilipata ugonjwa wa baridi ya bisi na kupooza mkono wa kulia, nikawa siwezi kabisa kushika maji ya baridi,hata nikitaka kuoga ni lazima nipeleke jiko la mkaa bafuni kukishakuwa na joto ndo nikaoge tena maji ya moto,masaa yote nilikuwa navaa soksi na nguo nzito nzito lakini bado haikusaidia ndo kwanza kifua kilizidi kubana; misuli ilikaza na kuuma,tumbo lilijaa gesi pamoja na maumivu makali ya mgongo na kiuno kiasi kwamba sikuwa naweza kufanyakazi yoyote zaidi ya kulala na kujifunika mablanketi makubwa ili angalau nipate joto, bado haikusaidia.

Nilienda hospitali za kila aina pamoja na kunywa dawa za kila aina lakini sikupona. Siku moja baada ya kusikia mahubiri kwa habari ya ‘imani’, nikaamini, nikapata hasira ya Roho Mtakatifu baada ya maombi nikaanza kukiri kuwa mimi si mgonjwa, nikaanza kuoga maji ya baridi, nikawa naweka maji kwenye friji nakunywa, nikawa nagandisha barafu nakula, nikaanza kuvaa nguo za kata mikono bila sweta na blanketi zote nikazieka mbali na kitanda na nikajizoesha kila asubuhi niamkapo baada ya kuomba maombi ya kumshukuru Mungu kuniamsha salama baada ya  hapo nakunywa maji baridi naingia bafuni na kuoga maji ya baridi na jioni tena kabla ya kuoga,HAKIKA NAMSHUKURU MUNGU HAKUKAA KIMYA HIVI NINAVYOANDIKA WARAKA HUU MIMI NI MZIMA WA AFYA HATA SIJUI HIYO STROKE NA BARIDI YA BISI ILIISHAJE,JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO WANAZARETI LISIFIWE,AMINA,Shalom prophet, shalom all group members!

Vesta: Shalom!

Vesta: Ushuhuda mzuri sana!

+255 763 194 9**: Ahsante mpendwa MUNGU akubariki sana!

Laura: Woow… ushuhuda mzuri; unazidi kutuinua na kutujenga ki-imani, barikiwa saana na Mungu aendelee kukutunza.

+255 763 194 9**: Amina!

PROPHET: Amina, ushuhuda mzuri sana na mfano mzuri wa kuamini kwa uhakika Mungu atakutetea tu!

Kuamini kwa mtu ndio kuna achilia uweza wa Mungu uonekane.

+255 754 650 6**: Hakika.

PROPHET:  Ndio maana watu wengi wanavyosema upako wa mtumishi unafanya kazi sio kweli… Ni imani yako ndiyo inayofanya kazi kupitia neno uliloambiwa sio upako wa mtumishi. Kile kinachofanyika kwa mtumishi ni ishara inayotokea kukuongezea wewe Imani, sasa changamoto ni kwamba, watu wengi wanataka kuishi kwa ishara pasipo kuelewa wanatakiwa waishi kwa imani zao binafsi. Kitakachokufanya upite salama kwenye matatizo sio upako wa mtumishi ni imani yako wewe.

+255 763 194 9**: Ni hakika na kweli kuwa ‘GOD WORKS WITH PEOPLE WHO ARE MOVING.' I MEAN Mfano ukiambiwa una vidonda vya tumbo, kwa imani kula vyote ulivyonyimwa kula, ng'oa madhaifu yote unayoyahisi mwilini mwako kwa kutumia damu ya YESU Kristo fanya maombi mara nyingi zaidi bila kuchoka; ni hakika utapokea uponyaji.

ENDELEA DARASA UK.6