DARASA UK.9

 

DARASA UK.9

 

WANAFUNZI WA KRISTO

Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

 

 

Prophet Joachim Francis

check bullet point red animation "...ni lazima uelewe uhalisia

wako wa kiroho

katika ulimwengi wa roho

katika Kristo..."

 

10/7/19, 19:59 - +255 766 919 8**: Shalom!

10/7/19, 20:58 - PROPHET: Kuna mahali niliishia kufundisha kwenye somo lililopita.

10/7/19, 21:02 - PROPHET:  Niliishia kufundisha kuwa...

"ni lazima uelewe uhalisia wako wa kiroho katika ulimwengi wa roho katika Kristo..."

Na nilieleza maana tofauti za tafsiri za Kristo....narudia tena ili tuelewe kwa umakini.

Kristo anatafsiriwa katika maana tatu ambazo mbili ni kuu.

Maana ya kwanza ni maana ya Kristo Mwokozi aliye tabiriwa kuwa atazaliwa kuukomboa ulimwengu kutoka kwenye dhambi.

Hii ni maana ya kwanza ambayo ipo common kwa wengi na wengi wanalifahamu hili...kwa hiyo, Kristo huyu akitajwa kwenye masikio ya wengi, anatafsiriwa kama Yesu Kristo ambayo ni kweli kwa mtazamo mmoja.

Mathayo 16:16 – ‘Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.’

Huyu ni Kristo aliyetabiriwa kwenye maandiko kuwa ataziliwa.

Maana ya pili ni Kristo kama roho!

Kristo huyu ni tofauti na Yesu Kristo...Kristo huyu ambaye ni roho; ndiye ambaye Yesu aliagiza wamwamini....ndio maana hata katika kusoma maandiko utaona kuna Kristo Yesu na Yesu Kristo...haya maneno hayajageuzwa kwa sababu mwandishi alijisikia kuyageuza, hapana, yamegeuzwa ili kuonyesha tofauti kati ya Yesu aliyezaliwa na Kristo aliye roho! ‘KRISTO ANAYEZUNGUMZWA HAPA NI KRISTO ALIYE ROHO NA SIO ALIYEZALIWA.’

Warumi 8:9 – ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwuufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.’

Roho huyu wa Mungu anayezungumzwa hapo sio Roho Mtakatifu hapana! ‘Ni roho ya mwanadamu iliyokwisha hesabiwa haki kwa imani katika Kristo aliyekuwa ndani ya Yesu,’ sasa, kuhesabiwa huko haki ndiko kunamfanya awe mrithi pamoja na Kristo Yesu, yaani Mwana wa Mungu.

8:14-17

[14] ‘Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.’

[15] ‘Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.’

[16] ‘Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;*

[17] ‘na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Utukufu Ujao.’

Kwa hiyo, katika maana hii ya Kristo kama roho tunapata tafsiri ya Kristo kama Mwana wa Mungu. Sisi tunafanyika wana wa Mungu / watoto wa Mungu kwa imani ndani ya Kristo aliyekuwa ndani ya Yesu.

Maana ya Tatu na ya mwisho ambayo ndio muendelezo wa somo la leo ni Kristo kama ‘UHALISIA WETU WA KIROHO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.’

10/7/19, 21:36 - PROPHET: Ukiwa unasoma biblia, penda kufuatilia mambo madogo madogo ambayo ukiyapuuzia unaweza ukakosa usahihi wa kile unachokisoma...halafu ukikutana na mafundisho kama haya ndio unaanza kujiuliza mbona ni tofauti na kile unachokijuwa…

Ukikutana na neno kama ‘Ndani ya Kristo,’ ‘Kristo ndani yangu’, ‘katika Kristo’; pigia mstari kwa sababu hayamaanishi kitu kimoja.

10/7/19, 21:37 - Vesta: Ok…

10/7/19, 21:40 - PROPHET:  Ndio maana bado kuna wanafunzi ambao wanapata shida kuelewa kwa nini haya maneno ni tofauti na tofauti ipo wapi...ndio sababu narudia rudia ili twende pamoja nisije wachanganya…

Ukielewa kuwa Neno Kristo lenyewe linatumika katika maana tofauti tofauti na katika tafsiri tofauti utaelewa kuwa biblia ikisema ‘Ndani ya Kristo,’ nini inamaanishwa hapo.

Hadi sasa hivi nimewapa maana tofauti zinazotumika kuelezea neno KRISTO.

Nimeeleza maana mbili ambapo ya tatu nitaeleza baada ya kuweka sawa hizi maana mbili zieleweke vizuri.

Kwenye biblia ukikutana na neno ‘Ndani ya Kristo,’ unatakiwa ujiulize maswali kabla hujakurupuka kuelewa hilo andiko.

Swali lako la kwanza linatakiwa liwe, "Kristo anayetajwa hapo ni Kristo wa maana ipi au mtazamo upi?" Ukijibu hilo swali, utaelewa sasa mwandishi anaposema ‘ndani ya Kristo,’ anamaana gani.

Ukikutana na neno ‘NDANI YA KRISTO’ popote kwenye biblia elewa kuwa Kristo anayezungumzwa hapo sio Yesu Kristo sio Kristo kama roho...sio Kristo Yesu.

Ni Kristo kama ‘UHALISIA WA KIROHO.’

10/7/19, 21:47 - Vesta: Itabidi nirudie kusoma tena ndio nitaelewa. Tena niandike kwenye notebook ndio nitaelewa. Hivi hivi natoka kappa!

10/7/19, 21:48 - Vesta: Ooh!  Sasa zinaanza kuingia kumkichwani.

10/7/19, 21:50 - PROPHET:  Na changamoto kubwa ni watu wengi kujaribu kufananisha haya maneno hama vile yana maanisha mtu mmoja au kitu kimoja.

Ndio maana unaposoma maandiko soma kwa makini na pole pole ukirudia rudia.

Mstari mmoja unaweza kuwa ni kichaka kikubwa ambacho unaweza pata maana zaidi ya kumi hapo hapo.

Sasa, haya ninayoyaandika ni mafunuo yanayotokana na maana zilizo jificha nyuma ya kila andiko unaloliona.

‘Kwa hiyo, ukikutana na andiko linalosema ‘ndani ya Kristo’ maana unayotakiwa kupata ni kuwa ni ‘UHALISIA WA KIROHO wa wanaomwamini Kristo jinsi ulivyo katika ulimwengu wa roho.’

10/7/19, 21:54 - Vesta: Sawa mtumishi.

10/7/19, 21:56 - PROPHET: Kwahiyo, biblia ikisema mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya; unatakiwa uelewe kuwa biblia inamaanisha mtu akielewa uhalisia wake wa kiroho amekuwa kiumbe kipya.

10/7/19, 21:57 - Vesta: Sawa sawa nimeelewa.

10/7/19, 22:00 - PROPHET:  Kwa hiyo, changamoto kubwa ni pale watu wengi wanapopata ufahamu wa mtazamo mmoja kuhusiana na huyu Kristo....ndio maana nikasema, ukiishia kumjua Yesu Kristo na kufahamu habari za Yesu kuwa alizaliwa akafa kuna vitu utavi-miss kwa sababu kuna vitu vigumu hapo unatakiwa uvifahamu ili uishi maisha ya ushindi kiroho na kimwili pia.

10/7/19, 22:01 - Vesta: Yaani nilikuwa naelewa ukiwa ndani ya Yesu wewe nikiumbe kipya…

10/7/19, 22:01 - PROPHET:  Sasa biblia haimaanishi hilo…

Ndio maana nasema twende pole pole ili twende kwa pamoja.

Sasa turudi kwenye UHALISIA WA KIROHO.

10/7/19, 22:03 - Vesta: Sawa Pastor, kwa leo ishia hapa maana ukiendelea itakuwa ngumu Zaidi…

10/7/19, 22:05 - Vesta: ***, utaua bendi Pastor, ngoja kwanza nielewe maana naona nipo Mwenyewe ninaye fuatilia somo…

10/7/19, 22:08 - PROPHET: Sawa, tutaenda pole pole…

10/7/19, 22:09 - PROPHET: Kwa leo niishie hapa, najuwa mnaanza sasa kuelewa kile ninachokisema…

10/8/19, 06:40 - +255 766 919 8**: Unatambuaje uhalisia wako wa kiroho?

10/8/19, 06:40 - +255 766 919 8**: Shalom

10/8/19, 10:17 - +255 754 486 0**: Mmh tunaelewa pole pole…

10/8/19, 21:28 - +255 682 867 1** left

10/9/19, 12:44 - PROPHET:  Shalom shalom!

10/9/19, 12:44 - PROPHET: Leo tutaendelea na mafundisho…

Pale ambapo utapata shida kuelewa upo huru kuuliza kwa sababu tunajifunza kila siku.

10/9/19, 12:56 - +255 763 194 9**: Amina, ila nakuomba usiendelee kwanza mpaka jioni, kwa sababu wiki hii nimekuwa busy sana. Sijatulia nikafuatilia kwa umakini hivyo ukiendelea utaniacha mbaali!

10/9/19, 19:26 - PROPHET:  Wiki hii nilizungumzia kuhusu namna ya kuwa kiumbe kipya na pia nikarudia kufafanua kuhusu tofauti kati ya Yesu Kristo...Kristo ndani yetu....na Kuwa ndani ya Kristo.

Leo naendelea na somo nililo anza nalo ni la kuwa ndani ya Kristo.

Nilisema, ili uwe kiumbe kipya, unatakiwa uwe ndani ya Kristo na nikasema kuwa ndani ya Kristo ni kuelewa UHALISIA WAKO WA KIROHO ndani ya ulimwengu wa roho kupitia kumwamini Kristo.

‘Ni kupitia kufahamu uhalisia wako katika ulimwengu wa roho kupitia maarifa / neno/ ufunuo wa Kristo ndio utakuwezesha wewe na mimi kuwa viumbe ‘vipya!’

Uhalisia wako wa kiroho uliopo katika ulimwengu wa roho ni upi?

i) Lazima ufahamu kuwa umekufa na umefufuka pamoja na Kristo

Warumi 6:5, 8

[5] ‘Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;’

[8] ‘Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;’

ii) Lazima ufahamu ya kuwa umeketishwa katika kristo pamoja nae upande wa kuume wa Mungu.

Waefeso 1:20

[20] ‘aliyotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;’

Waefeso 2:6

‘Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;’

iii) Lazima ufahamu ya kuwa umeinuliwa juu zaidi ya falme, jina, mamlaka na nguvu za giza zilizopo katika ulimwengu wa roho.

Waefeso 2:6

‘Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;’

Waefeso 1:21

[21] ‘juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;’

Kwa hiyo, leo tutapitia vipengele vitatu ambavyo ukivielewa na ukawa na ufahamu na maarifa kuhusu hayo utakuwa kiumbe kipya.

Ufahamu wa kwanza kabisa ambao unatakiwa uwe nao ni kuelewa na kuamini kuwa ‘ULIKUFA NA KUFUFUKA PAMOJA NA KRISTO.’

Sasa ili muelewe hili jambo ni nini, natakiwa nirudie kuwaelezea na kuwafafanulia maana halisi ya kifo cha Yesu...kwa nini alikufa...kwa nini alifufuka...alifufuka kama nani...haya yote ni maswali ambayo ni lazima ujiulize...usipo elewa hapa ni bora usijiite hata Mkristo kwa sababu hapa ndio kumebeba maana nzima ya Ukristo au kumuamini Kristo.

Sasa twende pole pole na taratibu...sina haraka kwa sababu najuwa haya mambo nisipo enda taratibu nitaacha wengi nyuma na wengi hamta nielewa.

10/9/19, 19:36 - +255 763 194 9**: Amina!

10/9/19, 19:37 - PROPHET: Jambo la kwanza ambalo nataka niliweke wazi na pia muelewe ni kuwa kunatofauti ya kusema namwamini Yesu Kristo na kusema namwamini Kristo aliye ndani yako.

Kama nilivyokwisha kusema kuwa, Kristo maana yake ya kwanza ni roho na Kristo sio jina.

Yesu aliyekufa msalabani alikufa Yesu wa mwilini lakini hakufufuka Yesu wa mwilini tena.

Najuwa hapa ndio kuchanganyikiwa kunapoanzia…

Twende taratibu pamoja na maandiko.

1wakorinto 15:35 – ‘Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?’

10/9/19, 19:44 - PROPHET:  Tuangalie hapa maana halisi ya ufufuko. 1 wakorinto 15:39-40

[39] ‘miili yote haifanani; ila mingine ni ya wanadamu, mingine ya hayawani, mingine ya ndege, mingine ya samaki.’

[40] ‘Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.’

1 wakorinto 15:42-44

[42] ‘Kadhalika na ufufuo wa watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;’

[43] ‘hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;’

[44] ‘hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.’

1 wakorinto 15:45-47

[45] ‘Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.’

[46] ‘Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.’

[47] ‘Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni, naye ni roho.’

Biblia ikizungumza kuhusu Adamu wa pili haimzungumzii Yesu, inamzungumzia Kristo ambaye ndio roho anaye huisha miili yetu.

Warumi 8:10-11

[10] ‘Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.’

[11] ‘Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.’

Neno mauti kwenye biblia linamaanisha kutengwa na utukufu wa Kiungu ndani yetu ambayo ndio sura na mfano wa Mungu ndani yetu na kuwa katika hali ya uharibifu wa asili ya dhambi.

Kwa mujibu wa hayo maandiko tunapata ufahamu kuhusiana na maana ya ufufuo...na maana yake ni kwamba kinacho kufa ni mwili na kinacho fufuka ni roho sio mwili.

Kwa hiyo, tukisema Yesu alikufa na akafufuka tuna maanisha mwili wa Yesu ndio uliteseka ukafa msalabani kisha akafufuka Kristo ambaye ni Roho iliyokuwa ndani ya Yesu.

Na ‘kufufuka’ hapa hili neno linatumika kuwakilisha kutoka kwenye hali ya mauti na hali ya kutoka kwenye asili ya dhambi...

Sasa kwa nini Yesu alikufa?

Yesu alikufa ili abebe dhambi za ulimwengu mzima kwa kuingia gharama ya kufa kwa sababu yeye ndiye aliyebeba uzima wa milele ndani yake...na uzima huo ni roho wa Mungu yaani Kristo ndani yake.

1 yohana 2:1-2

[1] ‘Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,’

[2] ‘naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.’

10/9/19, 20:11 - PROPHET:  Yeye ndiye aliye beba hiyo roho ya uzima na ili abadilishane uzima huo na hali yetu ya mauti ilibidi afe kimwili kabisa...

Yohana 3:16

[16] ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.’

Alizaliwa kama mwanadamu, alivyobatizwa akafanyika kuwa Mwana wa Mungu.

Marko 1:10-11

[10] ‘Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;’

[11] ‘na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.’

Kwa hiyo, alivyokufa kimwili, Roho iliyokuwa ndani yake ikafufuka pamoja na sisi kutoka kwenye asili ya dhambi na kupungukiwa utukufu.

Sisi sasa tunapokea asili hiyo mpya kwa kumwamini yule aliye fufuka ambaye ni Kristo roho, sio Yesu mwili uliokufa.

Yohana 1:11-12

[12] ‘Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;’

Ndio maana nilisema hatumwamini Yesu aliyetembea Galilaya na Yerusalem, tunaliamini Jina lipitalo majina yote...na kwenye mafundisho ya jina la Yesu; nilifundisha.

Yesu alikufa ili tumpate Kristo ambaye ni uzima wa milele kwa sisi kufanyika Wana wa Mungu.

Tuna mwamini aliyekuwa ndani ya Yesu ambaye ni Kristo nuru ya ulimwengu mzima.

Yohana 1:7,9

[7] ‘Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.’

[9] ‘Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.’

Yesu alikuja ili kupitia yeye tupate kumwamini Kristo sio tumwamini yeye...ndio maana tunaliamini jina lake ambalo alipewa baada ya kufufuka; yaani jina la Kristo Yesu sio Yesu Kristo.

Kufa kwa Yesu kulisababisha tupatanishwe na Mungu kupitia Kristo aliye fufuka.

Kupatanishwa huko ndio kunatufanya tuwe warithi wa ahadi njema za Mungu katika maisha yetu kiroho na kimwili.

1 Timotheo 2:5

[5] ‘Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;’

Waebrania 9:14-15

[14] ‘basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?’

[15] ‘Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.’

Kwa hiyo, usipo elewa kuwa Yesu alizifia dhambi za ulimwengu mzima utadhani kuwa wewe bado ni mdhambi kwa sababu tu bado kuna vitabia fulani hujaviacha. ...hapana...yesu alikufa kuondoa mzizi wa dhambi ambao ni asili yake; sio matokeo ya dhambi...

Kwa hiyo, kunatofauti kati ya kuondoa mzizi wa mti na matunda ya mti...Yesu aliondoa mzizi kwa kutupa sisi nafasi ya kuamini kuwa mzizi huo umeeondolewa.

Unachotakiwa kufanya ni kutambua na kuishi uhalisia huo kuwa dhambi iliondolewa kupitia kifo cha Yesu Kristo.

Wale wanaoshindwa kuamini hivyo wanakosa uwezo wa kushinda matokeo ya dhambi kwa sababu hawamwamini Kristo ndani yao ambaye ni uhalisia wa Mungu / utukufu wa Mungu uliopo ndani yao.

10/9/19, 20:51 - PROPHET:  Matokeo ya dhambi yanaondoka pale ambapo umeshaanza kujitambua au kutambua uhalisia wako kuwa utukufu wa Mungu upo ndani yako na umeshafanywa kuwa mtakatifu kupitia kufufuka kwake Kristo.

Kupitia kifo chake tumekombolewa kutoka dhambini na kupitia ufufuko wake tuna hesabiwa haki na utakatifu.

Warumi 4:24-25

[24] ‘bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;’

[25] ‘ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.’

Haya niliyoyafundisha leo ni namna ufufuko ulivyo tokea....namna, maana, sababu na matokeo ya kufa kwake Yesu...kesho nitafundisha maana ya kufufuka kwake Kristo...mwenye swali anaweza kuuliza. Mweneye maelezo zaidi juu ya nilichofundisha anaweza kuelezea pia.

Shalom!

10/9/19, 21:02 - +255 766 919 8**: Ubarikiwe!

10/9/19, 23:04 - PROPHET:  Amina.

10/10/19, 21:51 - PROPHET: Shalom!

10/10/19, 21:51 - PROPHET: Mnaendeleaje?

10/10/19, 21:51 - PROPHET: Nawaombea…

10/10/19, 21:54 - +255 754 486 0**: Shalom!

10/10/19, 22:16 - +255 766 919 8**: Shalom!

10/10/19, 22:23 - +255 717 930 2**: Kwa kweli hapa nilichanganyikiwa!

10/11/19, 10:10 - +255 744 384 5**: Shalom!

10/11/19, 10:11 - +255 744 384 5**: I greet you people God!

10/11/19, 10:13 - Vesta: Shalom shalom!

10/11/19, 10:13 - +255 754 650 6**: Shalom!

10/11/19, 10:14 - +255 763 194 9**: Thank you very much! Am great and feeling good!

10/11/19, 10:22 - +255 744 384 5**: I'm fine thank you my dear Stellah. Be blessed.

10/11/19, 10:30 - +255 763 194 9**: Amen,be blessed Lorraine, nalipenda jina lako.

10/11/19, 10:30 - PROPHET:  Shalom natumaini wazima…

10/11/19, 10:31 - +255 763 194 9**: Exactly tunamshukuru mungu kwa hilo.

10/12/19, 08:02 - PROPHET:  Shalom shalom!

Natumaini ni wazima na mmeamka vizuri…

10/12/19, 08:52 - +255 714 414 1**: Shalom

Mungu ni Mwema.

10/12/19, 09:01 - PROPHET:  Leo tutaendelea na masomo.

10/12/19, 09:20 - +255 763 194 9**: Amen!

10/12/19, 09:29 - +255 717 930 2**: Sawa mtumishi…

10/12/19, 09:36 - Vesta: Shalom!

10/12/19, 09:37 - +255 719 513 9**: Shalom

10/12/19, 19:58 - PROPHET: Shalom!

10/12/19, 19:59 - +255 754 650 6**: Shalom

10/12/19, 20:02 - PROPHET:  Tunaendelea na masomo.

Mara ya mwisho niliishia kufundisha kuhusu mambo yafuatayo...maana ya kufa kwa Yesu na namna ya ufufuo wa Kristo ulivyotokea.

Leo naendelea kuhusiana na uhalisia wetu wa kiroho ulipoanzia kupitia ufufuo wa kristo...kwa hiyo nagusia maana ya ufufuo wa Kristo.

Kwa ufupi, nilichokuwa nafundisha ni kwamba,

Yesu aliye zaliwa sio Yesu aliyefufuka.

Na Kristo sio jina.

Kristo ni nafasi ya kuwa Mwana wa Mungu.

Yesu alikuja kama Kristo, yaani Mwana wa Mungu ili kupitia kuliamini jina lake tufanyike kuwa Wana wa Mungu.

Alikufa Yesu akafufuka Kristo ambaye ni roho.

10/12/19, 21:02 - PROPHET:  Kuhusu ufufuo ...tunatakiwa tutambue maana halisi ya ufufuo jinsi ulivyotokea na maana yake ni nini.

Jambo la kwanza kabisa tunatakiwa tuelewe ni namna ufufuo unavyotokea na uliwakilishwa na tendo gani Yesu akiwa hai.

Kabla ya Yesu kufa na kufufuka alikufa akafufuka kwanza akiwa duniani kwa sababu ufufuo ni jambo la kiroho sio la kimwili.

Yesu alikufa na Kristo akafufuka wakati wa ubatizo wake...kwa sababu ubatizo unawakilisha kufa na kufuka kwa namna ya kuzama na kuibuka kutoka kwenye maji...hilo tendo linawakilisha kufa na kufufuka kiroho.

Warumi 6:3-5

[3] ‘Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?’

[4] ‘Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.’

[5] ‘Kwa maana, kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;’

Sasa naomba tuangalie kwa umakini mstari wa 3:

Warumi 6:3  ‘Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?’

Nilifundisha nikasema, ukiona andiko linaanza na Kristo Yesu badala ya Yesu Kristo tambua kuwa anayezungumziwa hapa sio Yesu aliyezaliwa...wala sio Kristo roho bali ni Kristo uhalisia wa kiroho katika ulimwengu wa roho.

Tukisha elewa hilo tuelewe maana ya ubatizo! Ubatizo unafafanua na kutafsiri mambo mawili makuu ambayo siyo ya kimwili bali ni ya kiroho.

Kufa na kufufuka kiroho.’

Nikisema haimaanishi kufa kimwili...hilo neno kufa linamaanisha ‘kuvuliwa na kuondolewa kwa asili ya dhambi; yaani mtu wa kale na kuwa kiumbe kipya ambayo ndio asili mpya ya kiungu.’

Warumi 6:6 ‘mkijuwa neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;’

10/12/19, 21:22 - PROPHET:  Kwa hiyo, Ubatizo aliofanyiwa Yesu ulikuwa ni ubatizo uliobeba na kuwakilisha maana ya kiroho zaidi ya maji yale aliyozamishwa ndani.

Biblia inaposema tuliobatizwa katika Kristo tumebatizwa katika mauti yake; haimaanishi mauti ya kifo cha kimwili; inamaansisha mauti ya kifo cha asili ya dhambi au mtu wa kale.

Kwa hiyo, tunabatizwaje katika Kristo Yesu? ‘Kubatizwa katika Kristo Yesu ni kuelewa na kuamini katika maana ya kufa na kufufuka kwa Kristo kulikotokea kiroho wakati Yesu anabatizwa na maji mengi.’

Wakati Yesu anabatizwa ndipo roho aliposhuka juu yake na ndipo alipoanza kuhubiri kuhusu Ufalme wa Mungu.

Yesu aliitwa au alitambulika kama Kristo baada ya ubatizo wake.

Kuzamishwa kwake kwenye maji kuliwakilisha kuvuliwa kwa utu wa kale wa asili ya dhambi ya mwanadamu kwa sababu alivaa mwili wa mwanadamu...kupitia uelewa wa hilo tendo tulizamishwa au tulikufa pamoja naye kwa kuvuliwa utu wetu wa asili wa dhambi kupitia ubatizo wa maji wa Yesu.

Kwa kuinuliwa kwake Yesu kutoka kwenye maji; kunawakilisha kufufuliwa kutoka kwenye wafu... *nikisema kutoka kwenye wafu namaanisha kutoka kwenye hali ya asili ya dhambi na kwa kuamini na kuelewa hilo unakuwa sasa kiumbe kipya hapo ndio unakuwa ndani ya Kristo*

Pasipo kuamini uliuvua utu wako wa asili ya dhambi kupitia kuzamishwa na kuinuliwa kwa Yesu kutoka majini huwezi kuwa ndani ya Kristo kwa sababu kuwa ndani ya Kristo ni kuwa kwenye uhalisia wa kiroho wa Mungu kwenye ulimwengu wa roho.

Hayo mambo ni ya kiroho na ndio maana wakati Yohana anamtambulisha Yesu; alimtambulisha kama Mwana Kondoo aondoae dhambi za ulimwengu.

Kupitia kitendo cha yeye kubatizwa kulitupa sisi nafasi ya kuweza kuuvua utu wa kale kwa kuamini katika hilo tendo la yeye kubatizwa.

Hapa ndio tunarudi kwenye swala la matokeo au matendo ya dhambi kwamba, inakuwaje mtu anaweza kuendelea na tabia zile zile?

Pia changamoto kubwa ni lugha zinazotumika kwenye maandiko huwa zinahitaji tafsiri za kiroho kwa sababu ni mafumbo ya kiroho.

‘Kwa hiyo, kupitia Yesu Kristo tunabatizwa katika Kristo Yesu ili tuwe ndani ya Kristo.’

Sasa nifafanue hili nililolisema, maana najuwa nisipofafanua hapa hamtaelewa.

‘Kubatizwa katika Kristo Yesu ni kuelewa kuwa kupitia mwili wa Yesu tulikufa na tukafufuka pamoja naye...lazima usadiki katika hili ili asili yako ya dhambi ife...inakufa kupitia mwili wa Yesu na lazima pia uelewe umefufuka au umeinuliwa kuwa Mwana Wa Mungu kupitia kuinuliwa kwake kutoka kwenye maji na umekuwa mrithi pamoja naye kiroho kwa kuhesabiwa haki kama Kristo.’

Waebranja 10:10,20

[10]Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.

[20]njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;

Kwa hiyo, bila kuelewa hilo, kuiacha asili ya dhambi ni ngumu kidogo.

Nimefundisha jambo la kina kidogo...kama kuna mtu ambaye hajaelewa anaweza kuuliza.

Shalom, nitaendelea Jumatatu.

10/15/19, 06:01 - +255 766 919 8**: Shalom!

10/15/19, 06:03 - +255 714 414 1**: Shalom!

10/15/19, 11:05 - +255 719 739 3**: Shalom, asante kwa mafundisho mazuri, umenifungua kwa kujuwa Yesu Kristo na Kristo Yesu pia kwa ufasaha Kristo,, barikiwa!

10/15/19, 11:26 - PROPHET:  Amina!

10/15/19, 11:51 - +255 719 513 9**: Shalom!

10/15/19, 22:12 - +255 713 626 4**: shalom!

10/16/19, 13:12 - PROPHET: Shalom shalom! Natumaini wote ni wazima… Leo nitaendelea na mafundisho baadae jioni…

10/16/19, 13:13 - +255 714 414 1**: Shalom!

10/16/19, 13:13 - +255 714 414 1**: Aleluyah!

10/16/19, 13:13 - +255 763 194 9**: Shalom!

10/16/19, 13:13 - +255 744 384 5**: Shalom! Amen…

10/16/19, 13:37 - Vesta: Shalom!

10/16/19, 14:03 - +255 754 486 0**: Shalom!

10/16/19, 18:54 - +255 658 999 6**: ✋

10/16/19, 19:14 - PROPHET:  Tunaendelea… Mara ya mwisho nilifundisha kuhusu maana ya ubatizo unaotafsiriwa kama kufa kwa Yesu wa asili na kufufuka kwa Kristo wa rohoni.

Ni katika kuelewa jambo hili pekee asili ya dhambi inaondolewa...hapa Yesu alibatizwa ili kutuwezesha sisi kushinda dhambi kupitia Yeye.

Hii ndio maana halisi ya Ubatizo... ‘Kuelewa fumbo la kufa kwa Yesu wa asili ya mwanadamu na kufufuka kwa Kristo roho ambaye alifanyika kuwa Mwana wa Mungu kwa asili.’

‘Kabla ya Yesu kufa kimwili asili yake ya kibinadamu ya dhambi ndio ilianza kufa.’

‘Kabla ya Kristo kufufuliwa kwenye ulimwengu wa roho alifufuka kutoka kwenye asili ya dhambi.’

Ufufuo wa kwanza nilio uelezea ni ufufuo wa Kristo kuinuliwa kutoka kwenye maji baada ya ubatizo wa Yesu.

Ufufuo wa pili ni ufufuo ambao ulitokea pale Yesu alivyokufa na Kristo kufufuliwa kutoka wafu.

Nifuatilie kwa makini:

Agano Jipya lilipata nguvu baada ya Yesu kufa...na lilianza baada Kristo kufufuliwa.

Yesu ni yule aliyezaliwa kwa asili ya mwanadamu ya dhambi.

Wafilipi 2:5,7-8

[5] ‘Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;’

[7] ‘bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;’

[8] ‘tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.’

Kristo ni yule aliyezaliwa kwa asili ya Mwana wa Mungu

Yohana 1:13 ‘waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.’

Kwa hiyo, baada ya Yesu Kristo kufa Kristo Yesu akafufuka.

Leo ndio tunaangalia maana ya kufufuka kwa huyu Kristo.

Kufufuka kwa Kristo kumeleta mambo ya fuatayo:

i) Nafasi ya kuwa warithi, watawala pamoja na Mungu; yaani Wana wa Mungu.

Waefeso 1:11

[11] ‘na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.’

ii) Nafasi ya kuwa juu ya falme, mamlaka na nguvu zote za giza

Waefeso 1:21

[21] ‘juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;’

Uhalisia wetu wa Kiroho katika ulimwengu wa roho ni kuwa sisi ni warithi wa ahadi zote za Mungu...na kuwa sisi tupo juu zaidi ya falme na mamlaka za giza zote.

Hivi vitu havifanyi kazi kwa maombi...vinafanya kazi kwa kadiri ya ufahamu ulionao kuhusiana na maarifa haya.

Hukemei mapepo kwa maombi ndio yakuachie...haukemei matatizo ndio yakuachie, unachotakiwa kufanya ni kutambuwa na kujuwa upo juu ya hivyo vyote na wewe unastahili kupokea ahadi zote za Mungu katika maisha yako.

 

"In teaching others we teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages