DARASA UK. 4

 

 

 

 

DARASA UK.4

   

 

 WANAFUNZI WAKRISTO:

 Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo

               

Prophet Joachim Francis

 

4. purple world spin   IMANI  INAYOTUSHIDIA VITA  

 

8/1/19, 13:35 - Prophet: NILIMALIZA KUFUNDISHA KUHUSU WOKOVU...tukaangalia kuwa wokovu ni nini na tukaangalia pia maana halisi ya DELIVERANCE leo NATAKA NIENDELEE KUFUNDISHA KUHUSU ‘IMANI INAYOTUSHINDIA VITA’

8/1/19, 13:37 - +255 686 361 1**: Kabla hujaendelea Baba hebu nisaidie ule mlango unaosema , 'eleza shida zako upate haki yako,' means tunatakiwa kumweleza Mungu shida zetu...

8/1/19, 13:38 - Prophet: Tufahamu kuwa kinachopigwa vita ni IMANI yetu...na kinachotumiwa kupambana vita ni 'IMANI.’ Okeee, niseme kwa ufupi: Inategemea na aliye andika hayo maneno aliandika akiwa kipindi gani cha ufunuo wa kumjua Mungu. Yanatoka kwenye biblia ndiyo; ila huwezi fananisha Ufunuo wa Agano la Kale na Ufunuo wa Agano Jipya. Mungu ni Baba yetu; hivyo katika kumwambia matatizo yetu tunapata utulivu wa akili ila siyo kwamba ukimwambia ndiyo ata-solve hapo hapo bila wewe kutumia imani yako.

8/1/19, 13:41 - +255 686 361 1**: Sawa, tuendelee…

8/1/19, 13:41 - Prophet: Mueleze Mungu shida zako...ila tambua pia imani inanafasi yake. Sawa, imani nilishaelewa kabisaaa... Adui anacholenga  ni msimamo wako katika Kumtegemea Mungu. Akiweza kuondoa msimamo wako katika kumtegemea Mungu basi ataweza kukushambulia ipasavyo. Kwa hiyo, tunatakiwa tuelewe IMANI INAYOTUSHINDIA VITA NI IPI.

8/1/19, 13:44 - +255 686 361 1**: Natafuta njia muafaka nitakavyokua nasali ili nipate

8/1/19, 13:47 - Prophet:  Kwanza kabisa IMANI YA KIKRISTO NI IMANI GANI?

Maana kuna imani nyingi ambazo msingi wake sio Kristo Yesu... Wako watu wana imani na watumishi wao au miujiza. Wapo watu wana imani katika mafanikio na wapo watu wana imani katika uponyaji. Wapo watu wana imani katika miujiza, halikadhalika wapo watu wana imani katika kukanyaga mafuta; Wapo watu wana imani katika kunywa maziwa na asali; Wapo watu wana imani katika utoaji wao; Wapo watu  wana imani katika kutumia chumvi ....vitambaa...na maji wa upako. Ila hizi zote siyo imani, ni kujitaabisha.

8/1/19, 13:47: Prophet:  ‘IMANI YA KIKRISTO NI IMANI GANI?’

Imani ya Kikristo ni imani ilIyoanza siku ya Pentekoste na watu wa mataifa wakawabatiza jina wenye imani hiyo ya kwanza kuwa ni WAKRISTO. Kuna siri au maana ya sisi kuitwa wakristo.

 

 

SOMA ZAIDI HAPA

Warumi 16:25-26 [25], Sasa na atukuzwe yeye awezaye ‘kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri’ iliyositirika tangu zamani za milele, [26] ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya Manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ‘ili waitii Imani.’ Katika Kumuamini Mungu, kuna utaratibu wa jinsi ya kumuamini Mungu kupitia Yesu Kristo...jinsi Mungu alivyomfunulia Yesu ni kuwa tunamuamini Mungu kupitia Yesu na hakuna namna nyingine zaidi ya hiyo... Ila kuna namna unatakiwa uelewe imani yako inakua imesimamia wapi kwa sababu, Yesu hayupo na huwezi sema unamuamini Mtu usiye muona ndio maana alisema anaondoka ila hatuachi yatima anatuachia Roho Mtakatifu.

Kristo alituachia Roho Mtakatifu. Ukristo ulianzia siku ya Pentekoste aliposhuka Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza na hakuwahi kuondoka....niseme hivi, Roho Mtakatifu ni Ufunuo wa Mungu kupitia Yesu Kristo. Niseme hivi, Yesu hakusema analeta roho ya Petro...Paulo...Au Eliya, bali alisema anatuletea Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, kama huamini kama kuna Roho Mtakatifu au kama huamini kuwa huna Roho Mtakatifu, nataka uanze kuamini kuanzia leo kuwa una Roho Mtakatifu.

8/1/19, 14:02 - Prophet: Na nilifundisha kuwa kumpokea Roho Mtakatifu siyo kuwekewa mikono au kunywa mafuta au kufanyiwa impartation ya Roho Mtakatifu...kuna impartation ya Karama za Roho Mtakatifu; ipo ila siyo kuwekewa Roho Mtakatifu.

8/1/19, 14:03 - Prophet: Roho Mtakatifu tunampokea kwa imani kupitia mafundisho sahihi. Kwa hiyo, siri ya ufunuo wa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo ni siri ya IMANI na kusudi lake ni kuwa, tuwe watii au tuitii hiyo imani na siyo kutii mapokeo ya kibinadamu au ibada zilizotungwa. 1Wakorinto 2:1,4-5,7 - [1] Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, ‘sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.’ [4] ‘Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,’ [5] ‘ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Hekima ya Kweli ya Mungu’;  [7] ‘bali twanena hekima ya Mungu katika siri’, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; … Nifuatilie kwa makini:

8/1/19, 14:16 - Prophet: Imani yetu haipo katika hekima za Wanadamu bali katika NGUVU ZA MUNGU...sasa biblia ikisema imani yenu iwe katika ‘NGUVU ZA MUNGU’; haimaanishi nguvu za uponyaji...miujiza...unabii...hapana, inamaanisha, ‘HEKIMA YA KWELI YA MUNGU’ inayopatikana katika kuifahamu ile ‘SIRI.’ Ni katika kuifahamu na kuiamini hiyo SIRI ndio utakapoona nguvu za Mungu zikidhihirika. Kwa hiyo, hii siri ni siri ipi ambayo inazungumziwa hapa – 1Wakorinto 2:10,12-13 [10] ‘Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.’ [12] ‘Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.’  [13] ‘Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.’

8/1/19, 14:28 - Prophet: Sasa hekima hiyo ya Mungu inatoka kwa  ROHO MTAKATIFU, Kwa hiyo, ni muhimu sana kuamini umempokea tayari Roho Mtakatifu na anaishi ndani yako. Achana na mafundisho potofu kuwa unahitaji kufunguliwa. Ukiamini Roho Mtakatifu anaishi ndani yako ndipo utakapoanza kufunuliwa na Roho Mtakatifu na kupewa hekima ya namna ya kuishi kama Mkristo lakini hili linaanza kwa kupata ufahamu wa kuwa Ufalme wa Mungu yaani KRISTO NDANI YAKO NI TUMAINI LA UTUKUFU.

Wakolosai 1:27 [26] ‘siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;’ [27]ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo ‘utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu,�� tumaini la utukufu. Ukiamini kuna Ufalme wa Mungu ndani yako, yaani umebeba Utukufu wa Mungu ndani yako hapo ndipo utakapoanza kuona Nguvu za Mungu zina dhihirika kila mahali ulipo. Hutahitaji kutembea na upako wa mtumishi yeyote...huhitaji kutembea na vitambaa vya upako au mafuta au vifaa vya aina yoyote kwa sababu Mungu atakuwa ndani yako na wewe ndani yake.

8/1/19, 14:35 - +255 679 078 6**: Amina!

8/1/19, 14:39 - Prophet: Ukiwa na msimamo huu ni vigumu kupatwa na mashabulizi ya nguvu za giza na kukushinda kwa sababu unaujua ukweli na umeusimamia ukweli utaona Nguvu za Mungu zikikutetea kwa sababu siyo maombi pekee yenye nguvu bali imani sahihi inayokupa msimamo. 1 Yohana 5:4-5 (4) Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; ‘na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.’ [5] ‘Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?’ 1 Yohana 4:4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, ‘kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.’

 

8/1/19, 14:41 - Prophet:  Kwahiyo ukitaka kujua roho ya mpinga Kristo nikuangalia kua mafundisho unayofundishwa yanakuelekeza kumuamini Kristo aliye ndani yako au Kristo aliye kwa Mtumishi...kitambaa...udongo...chumvi...madhabahu....maji? Ukiona unaimani ndani ya Vitu vingine zaidi ya Kristo aliye ndani yako ujue roho za mpinga kristo zimeshakamata akili yako na kuanza kukutumikisha

8/1/19, 14:43 - My Son Profet: Unaamini Au uliaminishwa uamini nini? Hili linaamua kama wachawi na mapepo wataweza kukusumbua au hapana. ‘Kwahiyo kuanzia leo Amini Mungu yupo ndani yako.’ ‘Roho Mtakatifu anaishi ndani yako.’ ‘Umebeba utukufu wa Mungu;’  ‘Na una Mamlaka ya Kiungu ndani yako.’

8/1/19, 14:49 - +255 686 361 1**: Prophet nina swali, Mtume Paulo alituma kitambaa cha nguo yake Kwa wagonjwa, je, hapo ilikuaje; hebu tufafanulie…

8/1/19, 14:52 - Prophet:  Watu walikuwa ni wengi… Na alishindwa kuwafikia wote. Kwa hiyo, ikabidi vipande vya vazi lake ndiyo vitumike kuwafikia watu. Alifanya hivyo kwa sababu hakuwa na jinsi; ilibidi watu wasaidiwe...ila hakuuza hivyo vitambaa wala haikuwa ibada ya kugusa vitambaaa…

8/1/19, 15:12 - +255 686 361 1**: He-he-he-he… ibada ya kugusa kitambaaa daaa Mungu tusamehe tuliangamia kwa kukosa maarifa!

8/1/19, 15:35 - Pasta Kinuka: Kwa kuongezea ni kwamba, Mungu Roho Mtakatifu akikupa maelekezo ya kutumia vitu hata kiatu chako tumia kwa maelekezo na baada ya hapo usigeuze mtaji wa kupiga pesa; hayo maelekezo,Yesu alikoroga tope na kumpaka mtu ili aone...hakuanzisha ibada ya tope au kuuza tope la upako no...siku zote tunapaswa kumsikiliza Mungu na kumtii bila wasiwasi, Mungu anakaa ndani yetu na Ufalme wake wote hushuka kwa wale wanao mwamini tu...ukiwa na Yesu Haina haja ya kutembea na mizigo. Tena Kama alivyosema Nabii Joachim…

8/1/19, 15:36 - Pasta Kinuka: Kuabudu vitu ni ibada ya sanamu, na Mungu anachukia Sana...

God bless you all!

8/1/19, 15:38 - +255 686 361 1**: Ameeen!

8/1/19, 15:38 - +255 686 361 1**: Umesema...

1/19, 16:55 - Vesta: Kweli kabisa, Mungu hutoa maagizo mara 1 tu!  Lakini Watumishi wengine wanafanya mtaji…

8/1/19, 20:37 - Prophet: Shalom!

8/1/19, 20:38 - +255 719 513 9**: Shalom!

8/1/19, 20:39 - +255 719 513 9**: Asante sana prophet Mungu akubariki na azidi kukuinua!

8/1/19, 20:39 - Prophet: Aminaaaaa!! Kwa hiyo, nimefundisha mafundisho ya awali. Hayo yalikuwa yakukulia wokovu. Bado yapo mengine ila KWA SASA TUJIFUNZE NAMNA YA ‘KUISHI ROHONI.’

8/1/19, 20:47 - +255 719 513 9**: Amen!

8/1/19, 20:50 - +255 686 361 1**: Asante

8/1/19, 20:52 - Prophet: Ili tuwe washindi katika maisha yetu ya kila siku lazima tuwe washindi kwanza kiroho. Ili tuelewe namna ambavyo mtu anaweza kuishi kiroho, tuangalie maana ya ulimwengu wa roho.

8/1/19, 21:47 - Prophet: Mtandao hapa nilipo…

8/2/19, 01:13 - +255 713 626 4**: Duuu… Ujue nipo macho, nilikuwa nasoma nondo zako, barikiwa sanaaa…

8/2/19, 01:26 - +255 686 361 1**: Yaani hata mimi sasa hivi naelewa Sana, sijui kama kuna Pastor atanidanganya tena…

8/2/19, 01:27 - +255 713 626 4**: Hamna

8/2/19, 01:43 - +255 654 333 5**: …barikiwa mno Mtumishi wa Mungu!

8/2/19, 07:07 Prophet: Aminaaa!

8/2/19, 07:07 - Prophet:  Karibuni

8/2/19, 19:17 - Prophet:  Shalom Mungu!

8/2/19, 19:21 - +255 785 918 6**: Shalom

8/2/19, 19:21 - +255 719 513 9**: Shalom my prophet.

8/2/19, 19:22 - +255 654 333 5**: Shalom

8/2/19, 19:23 - +255 686 361 1**: Shalom

8/2/19, 19:27 - Prophet:  Naendelea​​​

/2/19, 19:36 - +255 719 513 9**: Sawa haina shida tunasubiri...

8/2/19, 19:38 - Vesta: Shalom!

8/2/19, 20:13 - +255 654 333 5**: Tupo tunasubiri kwa shauku…

8/2/19, 20:25 - +255 686 361 1**: Sana!

8/2/19, 20:25 - +255 686 361 18**: Can't wait!

8/2/19, 20:32 - Prophet: Naendelea

8/2/19, 20:34 - Prophet: NATAKA NIFUNDISHE KUHUSU ‘KUISHI ROHONI!’ 

8/2/19, 20:35 - Prophet: LAKINI TUTAZAME MAANA YA ULIMWENGU WA ROHO ili tuweze kuelewa maana ya kuishi rohoni. Ulimwengu wa roho kwa watu wengi walivyofundishwa ni tofauti kidogo na uhalisia ulivyo; ndio maana utasikia mtu anasema nilikua rohoni kana kwamba kwa muda huo ametoka.

8/2/19, 20:46 Prophet: Ulimwengu wa roho haujatenganishwa na ulimwengu wa mwili au hauwezi sema unatoka rohoni na unaingia mwilini kinachokufanya uwe wa kiroho au wa kimwili ni UFAHAMU na sio maombi au kunena kwa lugha ndio kunakufanya kuwa upo rohoni.

8/2/19, 21:09 - Prophet: Kuwa rohoni ni swala la kupata maarifa sahihi yatakayokupa hekima ya namna ya kuishi rohoni na hii hekima ndiyo inayoitwa ‘HEKIMA ITOKAYO JUU.’ Yakobo 3:13,15 [13] ‘Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.’

[15] ‘Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.’

8/2/19, 21:15 - Prophet: Kinachokuwakilisha kuwa wewe ni wa kiroho au siyo ni mwenendo au tabia inayojidhihirisha kutoka kwako. Na tabia hiyo ni matokeo ya UFAHAMU uletao HEKIMA fulani inayoanza kukufundisha namna ya kuenenda. Tambua kuwa akili yako jinsi ilivyo ndivyo inavyoamua. Tabia utakayo kuwa nayo na tabia hiyo ni zao la UFAHAMU ulionao, yaani inategemeana na ulichobeba kwenye akili zako...fikra zako ndizo zinaamua tabia yako ni ya namna gani. Ukiwa na akili ya kumwazia mtu vibaya lazima utapata HEKIMA ya kuwa na fitina juu ya huyo mtu. Vivyo hivyo, ukimuwazia mtu mema utapata HEKIMA ya kumtendea huyo mtu jambo jema. Tabia njema ni zao la mawazo mema. Tabia mbaya ni zao la mawazo mabaya.

8/2/19, 21:21 - Prophet: ‘Kwa hiyo, UFAHAMU wa mambo mema huleta HEKIMA ya kutenda mambo mema na hekima hiyo huzaa mwenendo wa Mambo MEMA.’ Kwa hiyo, kila kitu huanzia katika namna unavyo waza na kufikiri. Methali 23:12 ‘Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa…’ Sasa kuna HEKIMA za aina mbili:

  1. ‘HEKIMA YA MWILINI’
  2. ‘HEKIMA YA KIROHO’

Kumbuka nimesema chanzo cha Hekima ni MAARIFA yaletayo UFAHAMU / MTAZAMO. Kwa hiyo, mtazamo wako unategemeana na unachojua. Na nimesema tabia ni zao la hekima uliyoipata na kinachomfundisha mtu awe na tabia fulani ni hekima aliyoipata, KWA HIYO, HEKIMA YA MWILINI NA HEKIMA YA ROHONI NI ZIPI?

8/2/19, 21:35 - Prophet: Wagalatia 5:16-17 [16] ‘Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.’ [17] ‘Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.’

8/2/19, 21:38 - +255 754 650 6**: Shalom…

8/2/19, 21:42 - Prophet:  Hekima ya mwilini na hekima ya rohoni inaweza tafsiriwa kama tamaa za mwili na tamaa za rohoni. Nikisema TAMAA ZA MWILINI na TAMAA ZA ROHONI namaanisha hivi, chochote utakachotamani kufanya ili kujinufaisha wewe na nafsi yako ni tamaa ya mwilini. Na chochote utakachotamani kufanya usijiridhishe wewe au kujinufaisha nafsi yako ni tamaa ya kiroho. Na hii inatokana na aina ya hekima uliyonayo inayotokana na maarifa unayopata haianzii tu kutamani kujinufaisha wewe au kutamani kutojinufaisha wewe inaanzia kwenye maarifa unayoyapata. Kumbukumbu 30:15,19 [15] ‘Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;’ [19] ‘Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;’…

8/2/19, 21:55 - Prophet: Mungu anavosema amekuwekea mbele yetu uzima na mema, mauti na mabaya ana maanisha ametupa uwezo wa kuwa na ujuzi wa mema au mabaya kulingana na uchaguzi wetu wa kupenda kuyafahamu mema au mabaya na matokeo ya kuwa na ujuzi wa mema ni uzima na ujuzi wa mabaya ni mauti

8/2/19, 21:59 - Prophet: Mwanzo 2:17 [17] ‘walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.’ Nimefundisha nikasema MAARIFA/UJUZI huleta HEKIMA na hekima huzaa TABIA / MATENDO; kwa hiyo, biblia ikisema Mti wa Ujuzi wa mema na mabaya inamaanisha kitu hiki - Inamaanisha HEKIMA danganyifu. Huwezi changanya maarifa ya mambo mema na mabaya au naweza sema kwa lugha rahisi; huwezi tamani mambo yako na mambo ya kimungu wakati mmoja.

Warumi 8:5-8[5] ‘Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.’ [6] ‘Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.’ [7] ‘Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.’ [8] ‘Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.’

8/2/19, 22:16 - Prophet:  Kwa hiyo, ukisema wewe ni wa kiroho inamaanisha nia yako NI KUMPENDEZA MUNGU KWANZA na sio kujipendeza wewe au kupendeza wengine. Nia ya kumpendeza Mungu ndio chanzo cha matendo au tabia njema. Wagalatia5:16 ‘Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.’

TUNAENDAJE ROHONI?

unaenenda rohoni kwa kutamani kumpendeza Mungu katika kila jambo tunalofanya. Ukiwa na UFAHAMU huu utapata HEKIMA itakayokusaidia kutenda mema na hapo ndipo utakapo ongozwa na Roho Mtakatifu. Romans 8:5 [5For they that are after the flesh do mind the things of the flesh; but they that are after the Spirit the things of the Spirit. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.

Warumi 8:9,13-14 [9] ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.’ [13] ‘kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.’ [14] ‘Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.’ Kwa hiyo,  tufahamu ya kuwa kumpendeza Mungu ni mashindano na siyo jambo rahisi kwa sababu kuenenda rohoni ni kwenda kinyume na tamaa za mwilini; yaani, ‘UBINAFSI’/ ‘UMIMI’;  na huwezi sema wewe ni wa kiroho ukiwa umejaa ubinafsi ndani yako na umimi; hapo hauna Roho wa Mungu kama maisha yako yamekomalia kujinufaisha wewe tu.  Hapo ndipo tunajua tofauti kati ya wanaomtumikia Mungu na wanaomtumikia Shetani au kutumikia matumbo yao na ukitaka kupata ishara ya kwanza ya watu wanaotumikia matumbo yao utaona hizi dalili:

Yakobo 3:14-16 [14] ‘Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu... [15] ‘Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.’ [16] ‘Maana, hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.’

8/2/19, 22:47 - +255 686 361 1**: Daaaah heeeee   aise neno la Mungu ni jipya kila siku, na  linakuja kutuponya na maangamizi yoooteee!!

8/2/19, 22:51 - Prophet: Kujisifu...chuki ...uongo...ugomvi yote hayo ni dalili ya kwanza ya kuwa mwilini…

8/2/19, 22:51 - Prophet: Nitaendelea, Shalom!

8/2/19, 22:51 - +255 686 361 1**: Shalom!

8/2/19, 22:52 - +255 754 650 6**: Shalom!

8/3/19, 10:01 - Prophet: Shalom

8/3/19, 10:33 - +255 754 650 6** Shalom!

8/3/19, 11:03 - +255 686 361 18**Shalom!

8/3/19, 11:49 - +255 719 513 9**: Shalom!

8/3/19, 12:06 - Vesta: Shalom!

8/3/19, 12:40 - +255 654 333 5**: Shalom!

8/3/19, 16:57 - Prophet: Changed this group's icon

8/3/19, 21:09 - Prophet: Shalom!

8/3/19, 21:11 - Prophet:  Mnaendeleaje!

8/3/19, 21:13 - +255 754 650 6**: Shalom, tunaendelea vizuri mtumishi!

8/3/19, 21:31 - Prophet: Nimebanwa kidogo na mambo ya ibada kwa ajili ya kesho…nitafundisha halafu nitaendelea na somo nililoacha…

8/5/19, 09:45 - +255 713 626 4**: Sawa!

8/5/19, 20:26 - Prophet: Naendelea. Na nilichoahidi nitafundisha kwa leo…

8/5/19, 20:55 - Prophet: Kuhusiana na Ezekiel Sura ya 13: Na ni jambo ambalo nataka tuzungumze leo. Kuna changamoto kubwa ndani ya mwili wa Kristo katika namna ya kutumia vitu ama "spiritual materials" au "vifaa vya kiroho" kwa namna vinavyotumika kusaidia watu. Sasa niseme kitu kimoja, hakuna ubaya katika mimi kuombea kitu na kukupa utumie. Kwa mfano, naombea kitambaa halafu ninakupa kupitia hicho jambo fulani litokee; yaani nguvu za Mungu zikuguse ila nia yangu siyo katika kukutengeneza mazingira ya wewe kuweka imani juu ya mimi na hicho kitu nilichokupa.

Changamoto kubwa ipo hapa na jinsi ambavyo hivi vitu vinaaamishwa juu ya watu. Sasa twende kwenye maandiko husika: Ezekiel 13:17-18 [17] ‘Na wewe, mwanadamu, kaza uso wako juu ya binti za watu wako, watabirio kwa akili zao wenyewe; ukatabiri juu yao, [18] ‘useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?’

Hapa Ezekiel alipewa huu ujumbe aseme na Watabiriao yaani "Manabii" Watumishi wa Mungu ambao walianza kutengeneza vitu na kuwapa watu kama ishara ya utabiri wao juu ya hao watu.: Na vitu walivyokuwa wakiwapa siyo kwamba waliwapa kwa nia ya kuwa kupitia hivyo vitu Mungu awaguse watu wake;  hapana, bali kwa nia ya kujipatia "faida!" Kwa sababu kati ya vitu walivyowapa watu ni "vitu vya kuvaa mikononi"  na "vitambaa" vya upako kwa wakati huo - ndio hirizi za mikononi na leso zinazotajwa hapo.

Hirizi hizo zinazozungumziwa, unaweza ukalinganisha na "wrist bands" wanazovaa watu siku hizi ambazo zinauzwa makanisani...ambazo kwa mujibu wao ukivaa unalindwa na Mungu...pamoja na leso hapo ambazo sasa hivi zinaweza kuwa vitambaa vya upako au sticker ambazo pia zinapatikana makanisani; ambazo unaweza ukaweka kwenye gari...biashara yako au ukawa unatembea nazo kwa imani kuwa umembeba Mungu kupitia hizo ‘zana za upako!

8/5/19, 21:15 - Pasta Kinuka: Duu...

8/5/19, 21:15 - Pasta Kinuka: Kweli hakuna jipya chini ya dunia...kwa kifupi, hakuna kitu kisichofanywa huko nyuma na kinafanywa siku hizi… Ni kipya...yote yalishafanyika…

8/5/19, 21:16 - Prophet: Sasa mstari wa 18, Mungu anawaonya kuwa, wanaofanya hayo, "Wanawinda nafsi za watu na kuzifunga nafsi za watu."

KUZIFUNGA NAFSI ZA WATU KIVIPI?

8/5/19, 21:19 - Prophet: Kufanya mtu awe mawindo maana yake ni kumweka mtu katika hali ya tegemezi kwa kitu au mtu na siyo Mungu. Yaani ni hali ya kuteka akili ya mtu katika kutegemea kitu au mtu na katika hali hiyo uweze kujipatia faida kutoka kwake. Kwa sababu nia ya wale Manabii ilikuwa ni kutengeneza hizo hirizi na leso ili wajipatie faida. Ezekiel 13:19 [19] ‘Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.’

kwa uwazi kabisa huwezi ukaenda kwenye makanisa ya wanaogawa hivyo vifaa vya upako ukavipata bure tu...vinauzwa!

Sasa Mungu akaweka wazi kuwa yupo KINYUME NA HAYO MAMBO kwa sababu Manabii hao wanawafanya watu watoe imani yao kwa Mungu na kuwa na IMANI TEGEMEZI ambayo haimhusishi Mungu moja kwa moja bali inamhusisha mwanadamu au kitu fulani cha kushikika; na kwakufanya hivyo, unajitenga na Mungu aliye kweli na unakuwa unamtegemea mwanadamu na ukishafikia hiyo hatua unakuwa mateka au mawindo wa huyo mtu uliyeamua kumtegemea na kumwamini kupitia hivyo vifaa vya kiroho unavyotumia.

Na imeandikwa amelaaniwa anaye mtegemea au kumwamini mwanadamu zaidi ya Mungu ...inamaana unakuwa unajilaani mwenyewe. Yeremia 17:5 [5] ‘BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.’

Unapotumia picha ya Mtumishi au kuomba kwa jina la huduma ya huyo Mtumishi au chochote alichokupa kama kitu cha kujiambatanisha na yeye ukakitegemea ili kupata ulinzi au kupitia hicho Mungu ajibu haja zako; umejilaani na moyoni umeacha kumtegemea Mungu moja kwa moja na huna imani; unaabudu sanamu!

8/5/19, 21:32 - Prophet:  Kwa hiyo, ni rahisi sana kwa mtu wa aina hii kushambuliwa na kuuawa na mapepo kwa sababu amejitenga na Mungu; amejitenga na imani kwa sababu imani siyo bayana na mambo yanayo onekana. Hivyo, huwezi niambia unaamini katika kitambaa ili Mungu akuguse, hapana!

Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ‘ni bayana ya mambo yasiyoonekana.’

8/5/19, 22:23 - +255 654 333 5**: Aisee, nami leo ndo nafunguka macho...kumbe hivi vilishafanywa nyuma...duh!

8/5/19, 22:24 - Prophet: Sasa hivi...

8/5/19, 22:28 - +255 686 361 1**: Tuzidi kushukuru Mungu tunajua ukweli, ili tukiona wenzetu wanategemea hivyo vifaa tutawafundisha.

8/5/19, 22:30 - Pasta Kinuka:!

8/5/19, 22:30 - +255 654 333 5**: Kwa hiyo, ni jinsi gani watoto wa Mungu tunavyoangamia kwa kukosa ijua Kweli…kama wote hao wanaojaa makanisani wakifuata miujiza na vifaa vya kiroho wangeijua kweli, wasingeangamia…

8/5/19, 22:30 - Pasta Kinuka: Haswaa…

8/5/19, 22:31 - +255 654 333 5**: Na huko makanisa ya namna hii yasingejaa!!

8/5/19, 22:33 - +255 686 361 1**: Mimi nilikuwa navaa na attack napata kama kawaida, jamani acha tu!

8/5/19, 22:37 - +255 654 333 5**: Mimi sasa kuna mtu alienda kanisa fulani la kinabii akaniletea mafuta na maji eti niyapulize ndani sasa ajabu unayapuliza huku ukinukuu mistari ya biblia na bado mauzauza unayapata kama kawaida...kha!

8/5/19, 22:41 - +255 679 078 61**: Khaaaa amin ikwamba imani ya mtu ndiyo inayothibitika kwa matendo yako so ukiamua hata kuchukuwa kucha yako ukaifanya kama ndiyo uponyaji wako utakapopitia, siyo mbaya…

8/5/19, 22:42 - Prophet:  Hahahahahaha!

8/5/19, 22:45 - +255 679 078 6**: Hahahah usikute ulikuwa unapulizia umaskini utapakae kwenye kila kona ya nyumba yako bila ya kufahamu nini unafanya. Sasa tuwe makini kwa haya tuliyofundishwa wapendwa!

8/5/19, 22:45 – Prophetit’s possible!

8/5/19, 22:51 - +255 679 078 6**: Mtumishi endelea kutupa matunda yaliyo bora tupate kuboresha akili zetu na ufunue nyoyo zetu tupate kuimarika katika Yesu kristo kwan bado twastahili mafundisho kutoka kwenye bible tujue nn twapaswa kufanya kama watumish wa kristo Yesu.

8/6/19, 04:33 - Vesta: Sasa naanza kuelew vizuri, nilikuwa na mdogo wangu anaota usiku anapiga makelel nikampa rist band avae sticker alale nayo, wapii ndio kwanza alizidi kuota akawaanasema hakuna kitu watumishi hawamuwezi, wote waongo.

8/6/19, 06:47 - +255 714 414 1**: Namshukuru sana Mungu maana nilikuwa nimeshapewa kitabu chenye maombi ya kushindana; nakushukuru mno Mtumishi umeniokoa kwenye mdomo wa mamba.

8/7/19, 22:16 - +255 654 333 5**: Shalom....

8/7/19, 22:16 - +255 654 333 5**: Mafundisho?

7/19, 22:16 - Prophet: Kesho!

8/7/19, 22:18 - +255 654 333 5**: ...naamini ibada ilienda vizuri. Yesu Bwana!

8/7/19, 22:18 - Prophet: Ibada ilikuwa nzuri…

8/7/19, 22:19 - +255 654 333 5**: Mungu Mwema!

8/7/19, 22:19 - Prophet: Sana!

8/8/19, 09:32 - Prophet: Added +255 754 082 2**

8/8/19, 09:42 - Prophet:  Added +255 718 485 9**

8/8/19, 09:59 - Prophet: LEO NAENDELEA NA MAFUNDISHOJiandaeni kula na kunywa mezani kwa bwana!

8/8/19, 10:24 - Pasta Kinuka: Shalommiss, Sana!

8/8/19, 10:25 - +255 754 082 2**: Nashukuru …

8/8/19, 10:44 - +255 686 361 1**: Sisi tunataka kunywa maziwa na asali bana!!

8/8/19, 10:44 - +255 686 361 1**: Can't wait!!

8/8/19, 10:46 - Prophet: !

8/8/19, 10:47 - +255 686 361 1**: Hahahhahhaha!

8/8/19, 15:34 - Prophet: Amina muda si mrefu!

8/8/19, 15:34 - +255 755 543 988: Amina.

8/8/19, 15:39 - +255 686 361 1**: Sawa

8/8/19, 16:55 - Prophet: Shalom!

8/8/19, 16:56 - +255 654 333 551: Shalom!!

8/8/19, 16:56 - Prophet: TUNAENDELEA SASA… Niliishia kufundisha somo la kuishi rohoni. Kwa hiyo, ni rahisi sana kwa mtu wa aina hii kushambuliwa na kuuawa na mapepo kwa sababu amejitenga na Mungu;  amejitenga na imani,  kwa sababu imani siyo bayana ya mambo yanayo onekana;  kwahiyo, huwezi niambia unaamini katika kitambaa ili Mungu akuguse, hapana!

Waebrania 11:1 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ‘ni bayana ya mambo yasiyoonekana.’

8/8/19, 17:04 - Prophet: Niliishia

8/8/19, 17:05 - +255 686 361 188: Sawa!

8/8/19, 17:05 - Prophet:  TUNAENENDAJE ROHONI?   

Tunaenenda rohoni kwa kutamani kumpendeza Mungu katika kila jambo tunalofanya. Ukiwa na UFAHAMU huu utapata HEKIMA itakayokusaidia kutenda mema na hapo ndipo utakapo ongozwa na Roho Mtakatifu.

Romans 8:5 [5] For they that are after the flesh do mind the things of the flesh; but they that are after the Spirit the things of the Spirit. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatayo roho huyafikiri mambo ya roho.

Warumi 8:9,13-14 [9] ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamuufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.’ [13] ‘kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.’ [14] ‘Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.’

8/8/19, 17:05 - +255 785 918 6**: Ok, Pastor!

8/8/19, 17:06 - Prophet: Kwa hiyo, tufahamu ya kuwa kumpendeza Mungu ni mashindano na siyo jambo rahisi. Kwa sababu, kuenenda rohoni ni kwenda kinyume na tamaa za mwilini, yaani ‘UBINAFSI’ / ‘UMIMI’ na huwezi sema wewe ni wa kiroho ukiwa umejaa ubinafsi ndani yako na umimi hapo hauna roho wa Mungu; kama maisha yako yamekomalia kujinufaisha wewe tu; hapo ndipo tunajua tofauti kati ya wanaomtumikia Mungu na wanaomtumikia Shetani au kutumikia matumbo yao na ukitaka kupata ishara ya kwanza ya watu wanaotumikia matumbo yao utaona hizi dalili: Yakobo 3:14-16 [14] ‘Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.’ [15] ‘Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.’ [16] ‘Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.’

8/8/19, 17:07 - Prophet:  Nakumbushia kidogo mahali tulipo ishia ili tujue tunaelekea wapi…

8/8/19, 17:08 - Prophet:  Nilichoishia kufundisha ni kuwa ili tuwe rohoni inabidi tuwe na HEKIMA itokanayo na MAARIFA / UJUZI sahihi utokao kwa Mungu na siyo wa kibinadamu. Kuna tofauti kati ya kuwa wa kiroho na kuwa rohoni.

8/8/19, 17:09 - Prophet: Wachawi Ila Ili uwe rohoni inatakiwa uwe na ROHO WA MUNGU na ili uwe na Roho wa Mungu unatakiwa uwe  na HEKIMA YA KIMUNGU. Hekima hii huja kwa kupata UJUZI / MAARIFA SAHIHI YA KIMUNGU. Yaani kuomba hadi kutetemeka haimaanishi wewe upo rohoni. Kuomba ukanena kwa lugha haimaanishi upo rohoni. Waweza fanya hayo ila ukawa mbea na mtukanaji, mzinifu tu wa kawaida kwa sababu huna HEKIMA YA MUNGU kukuzuia usifanye hayo.

8/8/19, 17:11 - +255 719 513 9**: Preach man of God!

8/8/19, 17:12 - +255 719 513 9**: Mwenye masikio na asikie!

8/8/19, 17:13 - Prophet:  Sasa tatizo la Wakristo wengi leo hatuna HEKIMA YA KIMUNGU. Ila tunajua kuomba sana.

8/8/19, 17:13 - +255 686 361 1**: Kwa

8/8/19, 17:13 - Prophet: Tunatafuta utatuzi wa matatizo badala ya kupata HEKIMA YA KIMUNGU. Na ndio kitu nataka nielezee leo kwa upana kidogo. Ukisema umempokea ROHO MTAKATIFU; maana yake ni kwamba, umepokea HEKIMA NA MAARIFA YA KIUNGU ndani yako. He-he!  Usifikiri kujazwa na roho ni kuanza kububujika kwenye maombi. Ndiyo maana wengi wanabubujika ila hawaoni matokeo ya bubujiko hilo katika maisha yao.  ‘Kwa hiyo, kanuni ya kwanza ya kuwa rohoni ni KUJIKANA WEWE NA MAISHA YAKO; yaani liwe ni kusudi lako kumtumikia Mungu kabla ya mipango yako wewe.’

8/8/19, 17:20 - +255 719 513 9**: Amen!

8/8/19, 17:20 - Prophet: Amua kumpendeza Mungu katika kila maamuzi unayotaka kufanya katika maisha yako. Chunguza nia ya kufanya hilo jambo unalotaka kufanya ukikuta nia haiendani na nia ya kumpendeza Mungu, ujue umeshapishana na Mungu kitambo sana. Na ndiyo maana hatuoni udhihirisho wa nguvu za Mungu au msaada wake mara nyingi katika changamoto tunazopitia sababu tunapishana na Mungu mara zote. Watu wengi wanalalamika kuwa hawasikii sauti ya Mungu au kupata mafunuo ya Mungu, ndiyo maana wanakimbilia kwa Manabii na wengine wanaishia kwa Matapeli kwa sababu hawana mahusiano na Mungu kwa namna ya kutaka kumpendeza.

8/8/19, 17:23 - Prophet:  Kama una mpenzi wako…Baby wako…Darling…Utataka kumpendeza aridhike, sasa kwa nini isiwe hivyo kwa Mungu? Unaona sasa unapopishana na Mungu? Ila unataka upige maombi hapo ujibiwe haraka sana. Upo tayari hata kuchanganya maziwa na asali unywe ili uone matokeo. Sikiliza, usipo kuwa na kiu, shauku ya kutaka kumpendeza Mungu au kumfurahisha, hutaona udhihirisho wake katika jambo lolote unalofanya; hapa ndio HEKIMA YA MUNGU INAPOANZIA.

8/8/19, 17:25 - Prophet:  Katika Mungu…

8/8/19, 17:27 - +255 686 361 1**: Inachomaaa kama pasi jamaniii!

8/8/19, 17:28 - Prophet:  Proverbs 1:7 [7] ‘Kumcha BWANA chanzo cha

8/8/19, 17:28 - +255 754 082 2**: Kweli

8/8/19, 17:29 - +255 654 333 551: …amina tupe madini hayo yatuingie akilini...

8/8/19, 17:30 - Prophet:  Methali 1:7 ‘Kumpendeza BWANA ni chanzo cha maarifa,’ Ukitaka Mungu aanze kukupa maarifa, weka nia ya kutaka kumpendeza katika kila jambo unalofanya. Maarifa yanayozungumzwa hapo ni maelekezo ya Kiungu katika namna utakavyo ishi hapa chini ya jua.

Mungu anaweza kukuelekeza mwenyewe lakini maarifa hayo yanafanya kazi kivipi?

Maarifa yanayozungumzwa hapo ni kutambua kuwa na nia au kutambua au kumkumbuka Mungu katika kila hatua; ukifanya hivyo, utapata HEKIMA ya kuweza kufanya maamuzi yatakayo kupa faida hapa duniani.

8/8/19, 17:33 - +255 686 361 1**: Amen!

8/8/19, 17:36 - Prophet: Methali 15:32-33 [32] ‘Akataaye maelekezo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.’ [33] ‘Kumpendeza BWANA ni maelekezo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.’ Sasa nisikilize kwa makini:

8/8/19, 17:36 - +255 686 361 1**: Sawa!

8/8/19, 17:39 - Prophet:  Nafundisha namna ya kuwa rohoni kabla hujaanza kutembea rohoni. Kuwa rohoni ni kuwa katika nafasi moja na Roho wa Mungu. Kutembea rohoni ni kufuata maelekezo ya Roho wa Mungu na kuyafuata hayo maelekezo inahitaji ‘UTII’ na ‘USIKIVU.’  Na kunaviwango vya usikivu na namna ya kuwa msikivu ila kwa leo nazungumzia namna ya kujiweka kwenye nafasi ya kuweza kuongozwa na Roho wa Mungu.

8/8/19, 17:41 - Prophet: Na nafasi ya kuweza kuongozwa na Roho wa Mungu ni kwa kuwa na NIA YA KUMPENDEZA NA KUMFURAHISHA MUNGU hapa ndipo unapoweza kujenga mahusiano ya moja kwa moja na Mungu kupitia Roho wake na Roho wake nimesema ni HEKIMA itokanayo na MAARIFA YA KIUNGU.

Ukiamua kujenga nia ya kumpendeza Mungu ndani yako moja kwa moja moyo wako unajenga mawasiliano usiyoweza kuyaelezea pamoja na Roho Mtakatifu bila wewe kujua. Ghafla kuna kiu kubwa ndani yako itakuja ya kutaka kumjua Mungu zaidi na kuwa karibu na Mungu. Kiu hiyo ikija ujue tayari una uhusiano na Mungu kama Baba.

Hapo ndio Roho Mtakatifu ataanza kukupa maelekezo; sasa maelekezo unayopewa ndiyo HEKIMA ya kukuwezesha kuishi maisha ya ushindi hapa duniani. Na hayo maelekezo ndio Mapenzi ya Mungu juu ya maisha yako binafsi jinsi Mungu anavyotaka uwe na hapo hautakuwa unaishi katika kiwango tena cha maombi utakuwa unaishi katika kiwango cha ukaribu na Mungu. 1 yohana 5:14-15 [14] ‘Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.’ [15] ‘Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.’ Kiwango cha ukaribu na Mungu ni kiwango cha ‘USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU.

Hapa ndio Wakristo wengi tunachangamoto. Kwa hiyo: 

UNAWEZAJE KUANZA KUMPENDEZA MUNGU?    

Ni ‘Usifanye kitu bila kujihakikisha katika hilo jambo nia yako ni kumpendeza Mungu na kumfurahisha.’

8/8/19, 17:54 - Prophet:  Fanyia jambo hili mazoezi… Utajiona unaanza kupata maelekezo ya Kimungu;  sasa hapa ndiyo nataka nifafanue muelewe maelekezo haya yanakuja kwa njia gani hasa.  Maelekezo ya Kimungu ni ya kiroho;  ya nakuja kwa njia ya rohoni na kwa sababu umeshaweka nia fahamu zako za kiroho zitaanza kufunguka ili kupokea maelekezo hayo kwa sababu upo katika nafasi ya ushirika na Roho Mtakatifu.

8/8/19, 17:58 - Prophet: Na nimekueleza ya kuwa sehemu husika inayotumika kuleta mawasiliano hayo na Roho Mtakatifu ni ‘MOYO’ au kwa lugha nyepesi zaidi ‘FIKRA’ zako. Kuna namna ambavyo utaanza kusemeshwa kupitia ‘MAWAZO YAKO’; hili ndiyo eneo la kwanza kabisa; utaanza kupokea maelekezo, tatizo ni kwamba, watu wengi hawaamini na hawana ujasiri wa kujitia moyo kuwa hili wazo ni la Mungu na Mungu ananisemesha hapa. Na kwa sababu hawaamini Mungu huwa anathibitisha yale mawazo kupitia mazingira uliyopo; hapa namaanisha matukio yatakayo anza kutokea na watu wanao kuzunguka wataleta taarifa au kufanya vitu ambavyo vitathibitisha lile wazo ulilokuwa nalo kichwani lililotoka kwa Mungu.

8/8/19, 18:03 - Prophet:  Sasa, kama wewe siyo mtu mfuatiliaji, utaona ni mambo ya kawaida au ni mawazo yako tu; ila ni Mungu huyo alikusemesha ila hukuamini!

Eneo la Pili Mungu ataanza kukupa maelekezo ni Eneo la Ndoto. Hapa  mara nyingi watu wanaota ndoto na kusemeshwa sana mara nyingine ni ndoto za wazi na mara nyingine ndoto zilizojificha kwa mafumbo; lakini hapa ndiyo mara nyingi Mungu huzungumza na watu wake. Ingawa mara nyingi ndoto nyingi huhitaji ufafanuzi kama huelewi, ila pia unaweza ukadai ufafanuzi wake kwa kumuambia Roho Mtakatifu akufafanulie kwa uwazi.

Namna ya Tatu ni kupitia Neno lake, mahubiri na mafundisho. Sasa hapa muelewe kitu kimoja…siyo kila mahubiri na mafundisho ni kwa ajili yako...hapana, ila yale yatakayokugusa moyoni.  Maana kuna mafundisho yanayoweza kugusia hali yako lakini hayajatoka kwa Mungu; mfano, naweza gusia eneo la uchumi hapa litamhusu kila mmoja ila siyo la Mungu.  Lakini yale yatakayogusa moyo wako kwa msisitizo ndiyo yametoka kwa Mungu. Kugusa, yaani kuleta namna ya mabadiliko moyoni mwako.  Hizi ndiyo namna pekee Mungu anaweza kusema na wewe.

8/8/19, 18:15 - Prophet:  Namna zingine ni namna za uthibitisho tu…Hapo ndiyo kuna unabii unahusika....siku zote ukipokea unabii wa jambo usilolijua ujue wewe na Mungu mlishapotezana siku nyingi sana. Hili pia nitalizungumzia siku nyingine. Hizo ndiyo njia Mungu anaweza kukuletea maelekezo yake. Ukiwa unaanza kupokea maelekezo ya Roho Mtakatifu binafsi inamaana tayari unaushirika naye lakini ushirika huo umetokana na nia yako ya kutaka kumpendeza Mungu na hapo inamaanisha upo rohoni...sasa, kuenenda rohoni au kutembea rohoni kunategemeana sana na uwezo wako wa ‘USIKIVU’ yaani umakini wako katika ‘KUYAPOKEA’  hayo maelekezo na  ‘UTII’ wako yaani umakini wako katika KUTEKELEZA maelekezo hayo.

8/8/19, 18:30 - +255 686 361 1**: Heeee!

8/8/19, 18:32 - Pasta Kinuka: Yes!

8/8/19, 18:34 - Pasta Kinuka: Mimi iko siku bwana akinipa kibali nitakuja na somo la ‘KUISHI MAISHA YA KUMTEGEMEA YESU KUNA FAIDA KUBWA SANA!’

8/8/19, 18:44 - Prophet:  Sasa ili uweze kuendelea kuishi na kukaa rohoni unatakiwa uendelee kuwa na ile ‘HEKIMA’ ya Kimungu itakayoendelea kufanyakazi ndani yako; unatakiwa ulinde sana ‘MOYO’ wako au ‘NIA’ yako katika ushirika wako na Mungu kupitia Roho Mtakatifu...sisi wanadamu wote tunamahusiano na Mungu tuwe tunajua au hatujui kupitia Damu ya Yesu; yaani, hata Mpagani au Muislamu wana  mahusiano na Mungu ila ‘USHIRIKA’ na Mungu unategemeana na Roho Mtakatifu pamoja na moyo wako au nia yako binafsi...kwa hiyo, ili uendelee kubaki na nafasi yako unatakiwa ujue kulinda moyo wako kwa kukataa tabia yako ya asili ya ‘UBINAFSI’ ndiyo ambayo itakuweka mbali na Mungu.

Wagalatia 5:24 ‘Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.’ Methali 4:23 ‘Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.’ Ukiweza kulinda moyo wako hivyo umeyalinda maisha yako...na unalinda moyo wako kwa kuendelea kuitendea kazi hekima uliyoipokea ya kimungu kwa sababu hekima hiyo ndio mafanikio yako! Methali 16:1 ‘Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua maarifa kuliko fedha.’

8/8/19, 18:45 - Prophet: Shalom . Mwenye maswali anaweza Kuuliza.

8/8/19, 18:57 - +255 719 513 9**: Amen!

8/8/19, 18:57 - +255 719 513 9**: Asante sana aisee somo zuri hili…

8/8/19, 19:14 - +255 785 918 6**: Amen pasta

8/8/19, 19:14 - +255 686 361 1**: Asante!

19, 19:15 - +255 785 918 6**: Ubarikiwe mtumishi kwa somo zuri!

8/8/19, 19:29 - +255 654 333 5**: Barikiwa sana Mtumishi wa Mungu!

8/8/19, 19:47 - Pasta Kinuka: Asante Sana Mage!

8/8/19, 20:50 - +255 754 650 6**: Barikiwa sana mtumushi, tumebarikiwa na somo zuri sana…

8/8/19, 20:55 - Prophet: Aminaaaaa!

8/9/19, 11:12 - +255 686 361 1**: Shalom Wanafunzi wa Kristo, nawapenda ipo siku tutakutana…

8/9/19, 11:16 - +255 686 361 1**: Prophet as soon as possible!

8/9/19, 17:29 - +255 712 090 9**: Barikiwa Pastor

8/9/19, 18:59 - Vesta: Asante,kwa mafundisho itabdi prophet utengeneze kitabu tuwe tunasoma kama biblia maana akili inafunguka kwakweli…

8/9/19, 19:00 - Prophet: Haya yote 'documentation.'    

8/9/19, 19:01 - Vesta: Merci beaucoup my `!

8/9/19, 19:01 - Laura: Utatufaaa saaana Prophet maana madishi yaliyumba saaana, chanel zilikata kabisaa!

8/9/19, 19:03 - Prophet: Channel

8/9/19, 19:04 - Vesta: Channel KRISTO!

8/9/19, 19:05 - Laura: Tulidanganywa saaana sasa wakatuvuruga tukawaamini kuliko kusoma Biblia, sasa akili unaziweka sawaaa…

8/9/19, 19:06 - Prophet: Inabidi

8/9/19, 19:06 - Laura: Kunawatumishi wanajua kusimamia uongo kama kweeeli duuuh ila Mungu anawaona …

8/9/19, 19:07 - +255 754 650 6**: Kabisa!

8/9/19, 19:08 - Laura: Sawa Prophet, tunashukuru saana kwa kutufundisha; maana ni wachache saana wenye moyo huu ulionao. .

8/9/19, 19:09 - +255 686 361 1**: Kwa kweli jamani kaaaa walituchezea akili Ila na Sisi sababu ya matatizo yetu wakatupata!

8/9/19, 19:10 - +255 686 361 1**: Au na wao walimezeshwa uongo??? Jamani wana roho ngumu sana!

8/9/19, 19:11 - Laura: Ila kwa sasa tumewapata na sisi, hawatudanganyi tena…

8/9/19, 19:12 - +255 686 361 1**: Kabisaaa, Mimi siku hizi mtu akihubiri hata Kwa TV tu, namchekiiiiii; nachambua mwenyewe hapa chenga; hapa sawa!

8/9/19, 19:12 - Laura: Na wao wakisimama wanajidai wanatoa madini na sie tunashangilia nakupanda mbeguuu …wametula aiseeee!

8/9/19, 19:13 - Laura: Haswaaaa!

8/9/19, 19:14 - Prophet: Mbegu

8/9/19, 19:14 - +255 686 361 1**: Wametulaaa mpaka tukawa hata nguo hatununui mpya, mpaka tunajuana kila mtu nguo anarudia zile zile; jamani, hata viatu tu tulishindwa kununua…

8/9/19, 19:15 - Vesta: Alafu wanatuambia sisi nimajinga, Mungu anawaona, hawaijui siku wala saa watapigwa vibaya na Mungu, tumepeleka sana hela kwnye madhabahu zao!

8/10/19, 09:15 - +255 713 626 4**: Swali unatambuaje kuwa una hekima?

8/10/19, 17:14 - Prophet:  Utatambua kuwa unahekima katika namna yako ya kufanya maamuzi.

8/10/19, 17:16 - +255 713 626 4**: Ok!

8/12/19, 14:03 - Prophet: Shalom Mungu…

8/12/19, 14:14 - +255 789 893 6**: Shalom!

8/12/19, 14:20 - +255 785 918**: Shalom!

8/12/19, 14:26 - +255 714 414 104: Shalom!

8/12/19, 14:32 - Vesta: Shalom!

8/12/19, 15:30 - +255 719 513 9**: Shalom!

8/12/19, 15:31 - +255 719 513 9**: We miss

8/12/19, 15:31 - +255 719 513 9**: Tuna

8/12/19, 15:44 - +255 679 078 6** left!

8/12/19, 17:47 - Prophet: Tunaendelea

8/12/19, 17:52 - Prophet: NAFUNDISHA – ‘NAMNA YA KUWA ROHONI KABLA HUJAANZA KUTEMBEA ROHONI’... 

Kuwa rohoni ni kuwa katika nafasi moja na Roho wa Mungu. Kutembea rohoni ni kufuata maelekezo ya Roho wa Mungu na kuyafuata hayo maelekezo inahitaji ‘UTII’ na ‘USIKIVU’.  Na kunaviwango vya usikivu na namna ya kuwa msikivu ila kwa leo nazungumzia namna ya kujiweka kwenye nafasi ya kuweza kuongozwa na roho wa Mungu. Na nafasi ya kuweza kuongozwa na Roho wa Mungu ni kwa kuwa na ‘NIA’ ya ‘KUMPENDEZA’ na ‘KUMFURAHISHA MUNGU’  hapa ndipo unapoweza kujenga mahusiano ya moja kwa moja na Mungu kupitia Roho wake na roho wake nimesema ni ‘HEKIMA’ itokanayo na ‘MAARIFA’ ya Kiungu.

8/12/19, 17:57 - Prophet: Nakumbushia kidogo pale tulipo ishia ili niweze endelea… Ukiwa unaanza kupokea maelekezo ya Roho Mtakatifu binafsi inamaana tayari unaushirika naye lakini ushirika huo umetokana na nia yako ya kutaka kumpendeza Mungu na hapo inamaanisha upo rohoni...sasa kuenenda rohoni au kutembea rohoni kunategemeana sana na uwezo wako wa ‘USIKIVU’ yani umakini wako katika ‘KUYAPOKEA’  hayo maelekezo na  ‘UTII’ wako yani umakini wako katika ‘KUTEKELEZA’ maelekezo hayo. Somo la Leo litazungumzia namna ya ‘KUENENDA AU KUTEMBEA ROHONI’ yaliyopita yalikua yanaelezea namna ya KUISHI ROHONI AU KUWA ROHONI…

8/12/19, 18:04 - Prophet: Kwa hiyo, mambo mawili makubwa:

    1. ‘USIKIVU’
    2. ‘UTII’

8/12/19, 18:06 - Prophet: Unaweza kuwa msikivu kiroho...hilo ndiyo jambo nitakalo lifundisha leo…

Watu wengi ni wa kiroho ila hawapo rohoni...wanaiga mambo ya kiroho na kwa kuiga huko wanadhani kuwa wao wapo rohoni na la kushangaza ni kuwa wanapoendelea kufanya hivyo, hawaoni matokeo wanayotaka kuyaona kwa sababu mambo wanayoyafanya ni zao la hekima za kibinadamu na siyo hekima za Mungu.  Sasa, haitoshi tu kuwa rohoni bali tunahitaji pia kuenenda rohoni...kuenenda rohoni maana yake ni kukubali ‘KUONGOZWA’ na Roho wa Mungu kwa ‘KUYASIKIA NA KUYATII MAELEKEZO’ ya Roho Mtakatifu...hilo ndio kusudi kuu la sisi kuachiwa Roho Mtakatifu.

5:25 [25} If we live in the Spirit, let us also walk in the Spirit. ‘Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.’ Warumi 8:12, 14, 21 [12] ‘Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,’ [14] ‘Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio Wana wa Mungu.’ Niseme hivi, sasa ili mpate ufahamu ulio bora. Kusikia sauti ya Mungu ni ‘kusikia maelekezo ya Roho Mtakatifu’...najua wengi wanataka wasikie sauti ikiwasemesha kama mtu (haha) hilo linawezekana kabisa ila linawezekana ukiwa umelala; kwenye ndoto....lakini ukiwa macho...unachopokea ni maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu na hiyo ndiyo kazi moja wapo ya Roho Mtakatifu.

Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, 'atawaongoza awatie kwenye kweli yote.'

Kukuongoza hapo maana yake ni kwamba utapewa maelekezo na hayo maelekezo ni 'KWELI YA MUNGU' / 'NENO LA MUNGU  yaani HEKIMA ya MUNGU' kuhusiana na maisha yetu binafsi

1Wakorinto 2:6-7

[6] 'Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;' [7] 'bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ...neno la Mungu sio haya ninayo wafundisha sasa hivi hapana neno la Mungu ni hekima inayokujia kwa kupitia roho mtakatifu pale unapofundishwa 'NJIA ZA BWANA' Kwahiyo ninachowafundisha hapa ni kuzijua njia za Bwana Zaburi 119:27 'Unifahamishe njia ya mausia yako.' Zaburi 119:33 'Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hata mwisho.' ...kwa sababu lengo la Mungu ni kutuongoza sisi na hatua zetu za kila siku katika maisha Zaburi 119:105 'Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.' Zaburi 37:23 'Hatua za mtu mwenye haki zaongozwa na BWANA, Naye aipenda njia yake.'

8/12/19, 18:47 - Prophet: Kwahiyo sisi walimu au wahubiri tunachokifanya ni kuwapa maagizo ya njia za Bwana na kufanya hivyo tunafungua mioyo yenu ama fahamu zenu kupokea maelekezo/kweli ya Mungu kupitia roho wake...ndio maana unatakiwa uwe makini sana na unachofundishwa...ukifundishwa mafundisho potofu au yasiyo ya neema na kweli unafungua fahamu zako zishambuliwe na roho chafu na zidanganyazo Zaburi 119:32 'Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponikunjua moyo wangu.'

8/12/19, 19:03 - Prophet: Tunapataje kuwa wasikivu ili tusikie sauti ya Mungu kupitia roho wake? Tunakuwa wasikivu kwa 'KUTAFAKARI MAAGIZO YA NJIA ZA BWANA' / kutafakari mafundisho ya kweli na neeam unayofundishwa. Zaburi 119:15 'Nitayatafakari mausia yako,' Nami nitaziangalia njia zako.

Kama ninavyowafundisha hivi, unatakiwa utafakari na sio kutafakari kwa kawada, hapana, kutafakari kwa 'BIDII!'

119:1-7,9-12

[1) 'Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.' [2] 'Heri watiio maelekezo  zake, Wamtafutao kwa moyo wote.' [3] 'Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake.' [4] 'Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana.' [5] 'Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.' [6] 'Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.' [7] 'Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako' [9] 'Jinsi gani mtu awezae kuisafisha njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.' [10] 'Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.' [11] 'Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.' [12] 'Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.'

8/12/19, 19:20 - Prophet: Kupitia kutafakari mafundisho kwa kurudia kusoma unafungua fahamu zako kusikia na kupokea maelekezo ya roho mtakatifu kama ukifanya kwa bidii

119:4

Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii kwa bidii.

1:2-3

[2] 'Bali sheria(maagizo) ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.' [3] 'Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.'

1:8

[8] Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, 'bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.'

Usipo jenga tabia na bidii ya kutafakari mafundisho ya neno la Mungu kama haya...utaomba sana ila utakua huoni matokeo ya maombi yako...kwa sababu mafanikio yako yapo katika kusikia na kutii maelekezo Mungu anayokupa kupitia roho wake na huwezi kusikia kama haupo rohoni na huwezi kuwa rohoni kama hauna nia ya kumpendeza Mungu....kwahiyo uwezo wa kusikia sauti au maelekezo ya Mungu huja kwa kuzijua 'NJIA ZA BWANA' kupitia 'NENO LAKE.' Kama hutaujaza ufahamu wako na Maarifa ya Kiungu hautamskia Mungu akikusemesha hata siku moja. Uwezo wa usikivu wako ndio kiwango cha 'IMANI YAKO.'

(Warumi 10:17)

'Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo.' Na Mungu hutenda kulingana na kiwango cha imani aliyonayo mtu na sio kwa uweza wa nguvu zake! Ukitaka uone Mungu anatenda ongeza imani yako; yaani usikivu wako katika kuyapata Maarifa ya Kiungu kupitia Neno lake.

Warumi10:2

'Kwa maana nawashuhudia kwamba wanajuhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.' Yaani uzijue njia za Bwana binafsi kwa kusemeshwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu!

8/12/19, 19:28 - Prophet: Shalom!

8/12/19, 19:29 - Prophet: Kwa leo naishia hapa katika kueleza namna ya KUENENDA ROHONI kwa KUSIKIA sauti ya Mungu.

8/12/19, 19:30 - Prophet: Nitaendelea kueleza njia ya Pili ya KUENENDA ROHONI kwa 'KUTII' sauti au maelekezo unayopewa na Mungu.

ENDELEA DARASA  UK.5

 

"In teaching teach ourselves"  - Proverb

Have Fun!
The Team at Educator Pages